"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, July 7, 2010

Siwezi Kumwambia

SWALI

Tunashukuru sana kwa kutuelimisha katika suala zima la mahusiano.

Mimi nimezaliwa katika familia ambayo suala la sex halikuwa topic ambayo inaweza kuongelewa kwa namna yoyote ile.

Kutokana na hayo malezi (Christian) inakuwa ngumu sana kwangu kuwa wazi kumueleza mume wangu kwamba nahitaji tendo la ndoa hii ina maana hata kama ninahitaji huwa namsubiri yeye aanze hata hivyo katika kusoma blog hii nimejifunza kwamba ni vizuri kwa mke wakati mwingine kulianzisha (naamini umeelewa nina maana gani).

Je, nifanyeje ili niweze kujisikia rahisi kumwambia au kumweleza!

Dada Jesca

MAJIBU

Asante kwa swali zuri dada Jesca, ukweli suala hili ni suala la kawaida sana katika jamii zetu hasa kutokana na malezi ambayo yanatufanya kuona ni kitu kigumu sana kujadili masuala ya sex kabla ya kuoa na hata baada ya kuoa au kuolewa; hii topic huwa ngumu sana kuijadili kati ya mke na mume mahali popote, kinachofurahisha ni kwamba wakati mwingine huhitaji kuongea kwa maneno kuonesha kwamba unamhitaji mume wako kimapenzi kama siku hiyo unajisikia upo horny.

Kila ndoa ipo tofauti hata hivyo kabla ya kusema chochote hebu tuangalie mtakafitu Paulo anasemaje kuhusiana na suala la sex katika ndoa.

“Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe, naye vivyo hivyo mke kwa mumewe. Mwanamke hana mamlaka juu ya mwili wake bali mumewe, wala mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe.

Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.

Nasema haya kama ushauri na si amri.

Laiti watu wangekuwa kama mimi nilivyo.

Lakini kila mtu amepewa kipawa chake kutoka kwa Mungu, mmoja ana kipawa cha namna hii na mwingine ana cha namna ile.”

(1Wakorintho 7:3-7)

Sasa ngoja tu Mbilinyilize haya maandiko (tufafanue kwa maana ya leo), anachosema mtakatifu Paulo ni kwamba anatuhitaji sisi wanandoa kufanya sex mara kwa mara. Na kama mnahitaji kutofanya kwa sababu ya maombi, hakuna tatizo ni jambo zuri.

Jambo ambalo linanifurahisha zaidi kuhusu huyu mtakatifu ni kwamba baada ya maombi mnaruhusiwa kuendelea kufanya tena na tena, hii ndiyo aina ya watakatifu ambao hata mimi naipenda.

Kwa nini andiko hili lipo?

Andiko hili lipo kwa sababu sex ni jambo la msingi sana katika ndoa na hii ni kuthibitisha kwamba Mungu ana ongea kuhusu umuhimu wa sex kwa wanandoa.

Sex haikuumbwa na shetani bali ni zawadi special kwa binadamu, mke na mume kupitia ndoa.

Jambo la msingi kama mke ni kuonesha mtazamo wa kuwa wazi na huru kuonesha upo tayari kwa tendo la ndoa (sex). Pia ina maana kwamba unatakiwa kumtimizia mume wako hitaji la sex wakati mwingine hata kama hujisikii vizuri au haijalishi mahusiano yapo katika hali gani.

Unauliza kwamba je, nifanyeje; kumbuka ndoa ni watu wawili ambao wanaunganika na kuwa kitu kimoja hivyo si suala la wewe peke yako bali ni suala la ninyi wote wawili kama mke na mume hivyo basi ni muhimu sana kujadili na mume wako namna mnaweza kuimarisha ndoa yenu katika mahusiano ya kimapenzi kuwa katika kiwango ambacho kila mmoja atajisikia huru na wazi kusema kile anahitaji.

Kila ndoa ipo tofauti, kuna wanandoa ambao kawaida huwa na sex secrete codes ambazo mume au mke akiona au kuhisi au kuambiwa basi anajua leo mwenzangu ananihitaji kimapenzi na si lazima uongee au kumshika na kumpeleka chumbani. Baadhi ya codes ni kwa mwanamke kuvaa Khanga, au wakati wa kulala anakuwa naked, au anatumia pafyum ambayo hujiweka siku akitaka sex tu.

Pia wapo ambao hutumia hata maneno kumwambia mume au mke kwamba sasa ni wakati wa kwenda chumbani kupeana haki yao kama vile mke anaweza kumwambia mume;

Kuna bills za kulipa tukazijadili, au kuna homework ukanisaidie au leo nina desserts ipo upstairs au kichwa kinaniuma naomba ukanipe dawa au vipi leo tuna ice cream? Au kusini mwa afrika wana njaa nk

Ni ubunifu tu!

Bottom line:

Jitahidi kuwa huru, wazi na ongea lolote unapenda linapokuja suala la sex na mume wako. Roma haikujengwa wa siku moja polepole itafika siku na wewe utakuwa mwanamke ambaye haoni aibu kusema au kumwambie mume wake kile anahitaji linapokuja suala la sex.

No comments: