"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, July 13, 2010

Tatu Bora kwa Mke!


Happy wife; happy life
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba usemi wa hapo ni kitu cha kweli; pia tafiti nyingi zinaonesha kwamba unapomchagua partner wa kuoana naye maana yake unachagua tatizo la kudumu nalo au raha ya kudumu nayo miaka 10, 20 au 30, 40, 50 ijayo.
“You can run; but you can’t hide”
Hata hivyo pamoja na hayo suala la kuwa na ndoa inayoridhisha haliji automatic ni suala la kuwekeza kujitoa na kufanyia kazi kuanzia mambo madogo madogo ambayo mwenzi wako anahitaji kutimiziwa.
Mume anapotoa maisha yake kwa mke wake maana yake ni hawi selfish na kutokuwa selfish ni jambo zuri ambalo linaweza kumfanya mke kuwa na furaha katika maisha na ndoa kwa ujumla.
Pia mume anapoishi vibaya na mke wake, hata akiomba maombi yake hayana maana, hii ina maana ili mume apate kibali cha maombi yake ni muhimu kuishi vizuri kwa kumpenda mke wake.
Je, ni mahitaji gani ya msingi kwa mke katika ndoa?
1. MAWASILIANO
Ni muhimu mno kwa mume kuamua au kuchagua kuwasiliana na mke wake, kuwasiliana na mke maana yake kumpa muda wa kuongea naye (quality time).
Pia si ustaarabu kwa mume kutumia neno “safi tu” au “fine” pale akiulizwa kuhusiana na kazi au vile anajiskia.
Fikiria mume unarudi kazini na ile kufika nyumbani mke wake anamuuliza
vipi honey habari za kazi?”
Na mume anajibu “safi tu
then anaendelea na ratiba zake za kusoma gazeti au kuangalia TV.
Kumbuka mwanamke hahitaji headlines au bottom lines; anahitaji full story, anahitaji habari kamili.
Ndiyo maana wanawake wengi huonekana ni the noisiest human being (vuvuzelas) kwa kuuliza maswali mengi huku wakijua mume hana hamu na kuongea, hata hivyo kwao ni kilio cha kutaka kusikilizwa, mtu wa kuwasiliana naye ambaye ni wewe mume.
Ni kweli wanaume wengi baada ya kazi na mihangaiko ya maisha kwa siku nzima anaporudi nyumbani huwa ameishiwa maneno ya kuongea hata hivyo ni muhimu sana kumpa mke angalau dakika 15 kuongea naye tu habari za kazi na maisha kwa ujumla kwani anahitaji connections kutoka kwa mume.
Mke anahitaji neno kwa neno kila kile unafikiria, mke anahitaji connections na mume wake angalau dakika thelathini kwa siku; mawasiliano kati ya mke na mume ni hitaji la msingi la mke katika ndoa.
Kuwasiliana ni feelings na wanawake wanapenda neno feelings ndiyo maana hujikuta wana-fall in love.
Kawaida wanaume wengi wakiulizwa na wake zao wanajisikiaje kutokana na kuonesha felings za kuwa kunaatizo, chakushangaza ni kwamba wanaume wengi hujibu “hawajui”. Wanaume wengi hawajui vile wanavyojisikia kwa sababu siyo watu wa hisia.
“Men came from the factory emotionally unassembled; all emotional wires are not connected”
Wanaume hutoka nje ya ndoa zao, kwa sababu hao wanawake huwapa heshima hao wanaume kwa kuwapa sex.
Wanawake hutoka nje ya ndoa kwa sababu hao wanaume huwajali kwa kuwasikiliza ku-connect na hisia zao.
2. KUONGOZA
Ndoa nyingi zimeharibika kwa sababu mwanandoa mmoja anakuwa amemkalia mwenzake (dominate); kuongoza maana yake kuanzisha jambo lolote katika ndoa ili kulifanyia kazi na kuwajibika (initiate).
Wanawake katika ndoa hulalamika kwamba waume zao wanashindwa kuongoza nyumba zao matokeo yake wanawake wengi wamekuwa ni watu wa kulaumu na kulalamika.
Mke huitaji mume kuwa kiongozi katika maswala ya kiroho (maombi, kusoma neno), watoto (shule, michezo, nidhamu), mahaba (birthday, tendo la ndoa, anniversary) nk.
Pia mume anahitajika kuwa kiongozi mzuri linapokuja suala la pesa (pia ni vizuri kukumbuka kwamba maamuzi ya fedha ni mahesabu [math) siyo hisia ambapo Mr. Bajeti hupewa kipau mbele).
3. UHAKIKA (SECURITY)
Mke anahitaji kuwa na uhakika kwamba mume wake anampenda anamjali, ni yeye peke yake na anasikilizwa.
Mke anahitaji kuwa na uhakika kwamba mume hatamuacha atakuwa na yeye siku zote.
Mke ambaye hana uhakika na upendo wa mume wake anakuwa hajiamini, anajiona hana thamani, anajiona hapendezi na anakuwa hasikii vizuri kwa kuwa kila wakati anajawa na mawazo.
Ubarikiwe!

1 comment:

Anonymous said...

It is GREAT post, i appriciate ur work brother.