"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, July 16, 2010

Unanipendaje Hasa?

Tukubaliane kwamba kuna vitu ambavyo mke au mume ukifanyiwa na mume wake au mke wake hujisikia anapendwa au kwamba mke wake au mume wake anakujali.

Wote tunapenda kupokea zawadi kutoka kwa wapenzi wetu ila kuna wengine akipokea zawadi hujisikia anapendwa zaidi na mwingine huona ni kawaida, wote tunapenda kukaa na wapenzi watu na kutumia muda pamoja (quality time) hata hivyo kuna wengine bila kukaa na kuongea na mume wake au mke wake anajisikia hapendwi hata kama amenunuliwa gari nk.

Wengine kupendwa ni kusaidiwa kazi au kufanya kazi pamoja, wengine kupendwa ni mguso (touch) bila kukumbatiwa, busu au sex kwake hajapendwa.

Kwa maelezo zaidi soma hapa.

MFANO

Jane amezaliwa katika familia ambayo mama yake alikuwa anapika chakula kitamu sana kiasi kwamba baba yake alikuwa anamsifia mama yao kila wakati kwa huo uhodari wa kuandaa misosi ya nguvu, baada ya Jane kuolewa naye hutumia muda mwingi kuandaa chakula cha nguvu ili mume wake James afurahi kama alivyokuwa anafurahi baba yake kutokana na mapishi mazuri ya mama yake.

Hata hivyo James yeye anasema hajali sana suala la chakula kwani kwake chakula chochote sawa tu na anamshangaa sana mke wake Jane ambaye hutumia muda mwingi kupika badala ya kutumia huo muda kufanya mambo mengine.

Jane hujisikia vibaya kwa sababu pamoja na kupika chakula kitamu na cha uhakika mume wake James huwa hatoi sifa zozote wala kumtia moyo na badala yake anakatishwa tamaa na kujiona hapendwi.

James naye anaona mke wake hana heshima kwa kuwa anapenda kupika tu na hilo haligusi moyo wake na kujiona kweli ana mke anayemjali.

Tatizo ni kwamba Jane hajaolewa na baba yake bali ameolewa na James, linapokuja suala na kupendwa kwa mume wake misosi haina maana yoyote bali kukumbatiana, kupeana busu na kukaa chumbani na kufurahia raha ya kuwa mke na mume.

James anakiri kwamba mke wake anapokuwa active kimapenzi na kuwa karibu kimapenzi hujisikia anapendwa na mke wake kuliko suala la chakula kitamu.

++++++++++++++++++++++++

Jacqueline na John sasa ni miaka 35 kwenye ndoa yao; Jacqueline anajisikia afadhari kuachana na John kwa kuwa hakuna jipya kwani moto wa mapenzi katika ndoa umezima kabisa.

Jacqueline anakiri wazi kwamba yeye na mume wake hawana tatizo lolote la kifedha wala hakuna siku wamejikuta wanagombana hata hivyo anajisikia hakuna upendo wowote kutoka kwa mume wake.

John alipoulizwa unafanya kitu gani kuhakikisha mke wako Jacqueline anafurahi na kujisikia anapendwa.

John alieleza kwa mshangao kwamba hamuelewi mke wake anataka kitu gani kwani amejitahidi kufanya kila kitu ambacho mwanaume anaweza kufanya ili mke ajisikie happy lakini mke anaendelea kulalamika kwamba anajisikia hapendwi.

John anasema anajitahidi kuhakikisha anapika chakula cha usiku (dinner) mara 4 kwa wiki, siku mbili zinazobaki wanaenda out na rafiki zao, anaosha dishes hizo siku nne kwa wiki, anasafisha nyumba kila siku kwani mke wake analalamika kwamba mgongo unamatatizo, anajitahidi kusafisha mazingira nje ya nyumba na pia kufua nguo na kuzinyosha nk

Unaweza kujiuliza sasa huyu mwanamke analalamika kitu gani kama mwanaume anaweza kujishusha na kufanya hayo yote na bado mwanamke anaendelea kulalamika.

Jacqueline alipiulizwa je, ulitaka mume wako afanye kitu gani ili ujisikie unapendwa akajibu kwamba angefurahi kama ingetokea siku moja mume wake akaketi kwenye kochi na yeye na wakakaa na kuanza kuongea pamoja, kusikilizwa huku wakiongea mambo mbalimbali yanayohusu ndoa na maisha yako hapo Jacqueline angejisikia kupendwa kwani kila wakati mume wake ni kuzunguka huko na huko mara kupika mara kusafisha nyumba mara nje (yard) yaani yeye na kazi tuu na mke hana nafasi.

Jacqueline anasema anachotaka ni mume wake kukaa chini na yeye angalau dakika 20 kwa siku, waangaliane usoni, waongee mambo yanayowahusu wao na maisha kwa ujumla, huko ndo Jacqueline anaona ni kupendwa (quality time)

Hii ina maana kwamba kwa John kubwa busy hata kama ni kumsaidia kazi mke wake bado hakuweza kutimiza hitaji la emotions kwa mke wake.

Bado love tank la mke wake lilikuwa empty na kujazwa ni pale wakiwa pamoja, kukaa pamoja, kuongea pamoja.

Sasa John anakiri kwamba kwa miaka yote 35 alikuwa hajajua kwa nini mke wake alikuwa analalamika kwamba hawaongei, anakiri aliamini akimuuliza mke wake umeamkaje basi huko ndo kuongea, hakujua kuongea ni kukaa chini, kutazamani na kuongea na mmoja akisikiliza kwa dakika 20 au 30 na ndicho mke wake alikihitaji.

Mara nyingi wanaume tunapoona nyumbani kuna chakula, kuna fedha kuna kila kitu tunaamini basi mke atakuwa ameridhika kihisia kitu ambacho si kweli kwani kila mwanamke ana aina yake hasa ambayo kwake ni kupendwa.

No comments: