"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, July 8, 2010

Uwe Makini!

Siamini kama wewe ndiye yule kabla hatujaoana!

Inawezekana baada ya kuishi katika mahusiano ya uchumba sasa umeoa au kuolewa, Karibu sana kwenye chama kubwa, chama la ndoa, ulimwengu mpya kabisa, ambako mapenzi huchukua sura mpya ya uhalisia.
Sasa kila kile uliona si tatizo kwa mchumba wako unajikuta kinakuudhi, namna anavyotafuna chakula sasa inaudhi, namna anaweka muziki katika sauti ya juu sasa inaudhi, namna anaacha nywele kwenye sink bafuni sasa inaudhi, namna anaacha taulo lenye maji bila kulitundika ukutani inaudhi.
Namna anaacha kitanda bila kutandika inaudhi, namna anavyokoroma akilala usiku sasa inaudhi, namna anavyoacha drawer za makabati bila kuzifunga inaudhi sana, namna anavyoacha kuweka nguo na makoti kwenye hanger sasa inaudhi mno, namna anavyoongea bila break sasa inakuudhi sana, list inaendelea ..............................
Kumbuka wakati wa uchumba hivi vitu uliviona vidogo sana na kwamba hakuna tatizo!
Swali la kujiuliza je, nini kimetokea kwa ule upendo (fall in love)?
Ilikuwa ni illusions kukusababisha ujipeleke mwenyewe hadi kusaini mkataba wa ndoa na kukiri kwamba hadi kifo, katika raha na shida, katika afya na ugonjwa na inawezekana wewe ni mmoja ya wale ambao wanalaani sana ndoa walizonazo kwani wale ambao kwanza waliwaambia NAKUPENDA NA NITAKUPENDA wamewadanganya na sasa unajikuta upo kwenye ndoa ambayo kila siku hali ni mbaya.
Una haki ya kukasirika kwani ni kweli ulidanganywa na tatizo lilikuwa ulipokea information ambazo hazikuwa sahihi. Na hizo information zilikuwa ni ile hali ya kupendana (fall in love) ambayo katika ukweli si upendo wa kweli bali ni illusions.
Kale kakichaa ka kuamini kwamba tutapendana milele bila kuumizana wala kukwazana kangedumu na kuwa hivyo siku zote.
Katika asili “fall in love” ni mating character ya binadamu kuhakikisha mke na mume wanavutiana ili kuhakikisha species inaendelea (survival) na si upendo wa kweli.
Ulikuwa tayari kuacha kusoma kwa ajili ya mitihani ili kuwa na mpenzi wako maana yeye alikuwa muhimu mno.
Uliacha kwenda kwa rafiki zako hata ndugu zako kwa kuwa ulimpenda sana mchumba wako.
Uliacha hata kwenda kusoma au kwenda kazini ili kuhakikisha unampa mpenzi wako kile moyo wake unakipenda (to make her/him happy)
Kijana mmoja alikiri kwamba
Tangu nimekutana na huyu binti, nimempenda, siwezi kufanya kitu chochote tena, siwezi kuwaza kuhusu kazi kwani kila wakati nawaza na kuota kuhusu yeye.
Hamu niliyonayo ni kumfanya yeye awe na furaha muda wote, nipo tayari kufanya jambo lolote kuhakikisha anakuwa na furaha”.
Yaani mtu akili inahama hadi unajiona wewe ni Mama Theresa kwa maana ya kutoa kila kitu ili kuonesha upendo kumbe ni illusions.
Kumdondokea mtu (fall in love) ni hali ambayo hudanganya na kumfanya mtu ajione kweli yupo katika upendo wa kweli. Huamini kwamba hakuna tatizo linaweza kuwepo kila kitu ni shwari.
Baada ya hali ya kudondokeana (in love) kuchuja (kawaida baada ya miaka 2) ndipo mtu huanza kurudi kwenye ulimwengu halisi.
Ndipo unaanza kugundua yale unayapenda na kuona kumbe ni tofauti na yeye anayoyapenda.
Unajikuta wewe unapenda sex na yeye anajisikia kuchoka na hapendi.
Unapenda kununua gari kwanza na yeye anapenda mjenge nyumba kwanza.
Unapenda kutembelea wazazi wako yeye anasema hapendi mtumie muda mwingi kwa wazazi wako.
Unapenda kwenda kuangalia match ya mpira wa miguu (soccer), anakwambia unapenda mpira kuliko yeye.
Kidogo kidogo ule moto wa mapenzi ya kwanza (fall in love) huanza kuyeyuka na kila mmoja sasa anaanza kujikita kwenye kujipenda yeye na mambo yake, kujihisi na kuwaza kivyake na sasa mnazidi kuwa watu wawili tofauti.
Bila kufahamu namna mapenzi yanapanda na kushuka mnaweza kuishi kuachana.

No comments: