"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, July 27, 2010

Wanapenda Vitu Tofauti


Watu wengi hujiuliza kwa nini likija suala la nguo na viatu wanawake au mke huwa na nguo nyingi na viatu vingi na aina tofauti kwenye closet tofauti na mwanaume.
Mfano; ames anakiri kwamba mke wake ana zaidi ya pair 50 za viatu wakati yeye ana pair tatu tu, na linapokuja suala la nguo basi atahitaji calculator ili kujua idadi ya nguo za mke wake wakati yeye atatumia vidole vya mikono yake miwili kuhesabu ili kufahamu nguo alizonazo.
Swali la kujiuliza hivi hili suala linatufundisha kitu gani kuhusiana na mwanamke katika ndoa?
Hasa linapokuja suala la sex?
Linatufundisha kwamba katika yote hana nguo muhimu ambazo ni rasmi kwa ajili ya sex; si kweli.
Ukweli ni kwamba mwanamke au mke hupenda vitu tofauti (variety) linapokuja suala la sex. Ndiyo maana hawezi kuvaa nguo ile ile moja kila jumatatu au jumanne au jumatano au jumatatu inayofuaata anahitaji kitu kitofauti (variety).
Hata hivyo linapokuja suala la sex kwa mwanaume mara nyingi tunafanya bila kuhitaji utofauti wowote, tunajua nini tunaenda kufanyia, namna tunaenda kufanyia na tutaishia wapi.
Tatizo ambalo hujitokeza ni kwamba mke huwa bored na huo utaratibu (routine). Inafika mahali mke anafahamu au predict nini mume atafanya kwa sekunde tu, mke anaweza kutabiri mume atatumia muda gani huko upstairs kabla ya kwenda down stairs; mke wako anahitaji zaidi ya hapo anahitaji kitu kipya baada ya muda ndo maana havai nguo zilezile na viatu vilevile kama wewe.
Ukweli ni kwamba kama wewe ni mwanamke ni muhimu sana kufahamu kwamba mke wako alivyokuwa jana sivyo atakavyokuwa kesho linapokuja suala la sex, anavyojisikia jumamosi si vile atajisikia jumatatu au jumatano kila siku ni tofauti na mood tofauti.
Usiku mmoja anaweza kukuhitaji wewe umkumbatie tu usiku mzima, siku nyingine atataka muwe na adventure au just for quickie, usiku mwingine slow sex, usiku mwingine atatamani kurukia kila anachooa kina move chumbani pamoja na wewe nk.
As husband; your job is to figure out which direction the wind is blowing each particular day.
Siku njema

3 comments:

Anonymous said...

Many a true word is spoken in jest..................................................................

Anonymous said...

Ni kweli nimejifunza kwamba mke huhitaji vitu tofauti.
TN

Anonymous said...

UKWELI umenigusa saaana mana wangu hhalielewi hili sasa nimemwambia nae asome ili twende sawa. Asante sana unaimarisha ndoa zetu.