"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, July 14, 2010

Wanaume bwana!


Kwa nini wanaume wanahitaji sex na wanawake wanahitaji upendo.
wanaume huwa frustrated na wanawake kwa kuwa hawapendi sex na wanawake huwa frustrated na wanaume kwa kuwa kila mara wao ni sex tu.
Wanawake wanawalaumu sana wanaume kwa kuwa hawajui kupenda na wanaume wanawalaumu sana wanawake kwa kuongea tu kuhusu upendo lakini hawataki kuonesha vitendo (kufanya mapenzi).

Sababu inayofanya binadamu kujihusisha na sex ni kutokana na hormone ya testosterone, ambayo kwa kiwango kikubwa ni hormone ya wanaume.
Mwili wa kawaida wa mwanaume huzalisha mara 20 zaidi ya mwili wa mwanamke.
Kwa maneno mengine, hamu ya sex kwa mwanaume katika siku moja ni sawa na hamu ya sex kwa mwanamke baada ya kukosa sex kwa siku 20 au hamu ya kuhijitaji sex kwa mwanaume katika siku 20 ni sawa na hamu ya mwanamke kukosa sex kwa mwaka mzima.

Kwa kufahamu hizo tofauti hadi hapa unaweza kufahamu maumivu ambayo jinsia nyingine inayapata.
Kumbuka wanaume kuhitaji sex hadi kupitiliza hawajasababisha wao au ni kitu wanajitakia bali ndivyo wameumbwa na hizi ni sababu zinazofanya mwanaume kuwa mwanaume na mwanamke kuwa mwanamke.
Wanaume na wanawake ni tofauti.
+++++++++++++++++++++++

Mwanaume anaweza kuzalisha au kusababisha mimba kwa mwanamke kila anapofanya sex, lakini mwanamke anaweza kuzaa mtoto kila baada ya miaka 2; hii ina maana mwanamke lazima awe makini kuchagua sana (picky) mwanaume wa kuoana naye ili kuzaa naye watoto.
Lazima achague the best seed.
Kwa miaka mingi (generations) wanawake wamekuwa wakilipa gharama (price) kutokana na kuchagua wanaume wasiofaa (mbegu dhaifu); kwani wanawake waliochagua wanaume wenye udhaifu wa genes wamesababisha kuwa na watoto (offspring) ambao imekuwa si rahisi kuishi (survive); wanawake waliochagua wanaume wenye genes imara wamezaa watoto imara ambao waliishi, na hawa ndio wanabeba genes za mama zao za kuwa wachaguaji wa kupitiliza (picky) linapokuja suala la kuoana hadi leo, na moja ya hao offspring ni wewe.

Kwa asili wanaume huhitaji sex mara kwa mara ili kusambaza kizazi wakati wanawake huhangaika kutafuta the best seed ili kuwa na maamuzi bora ya kupata mbegu bora ya kuwa na kizazi bora.

“Men seek quantity - women seek quality”
Ndiyo maana wanaume wanahitaji sex na wanawake wanahitaji upendo.

Upendo ni uhakika ambao wanawake huhitaji kwa mwanaume ili kuhakikisha atashikamana naye kusaidia kulea watoto na kuhakikisha wanakua, na sex kwa mwanamke ni kitu cha ziada anachotoa kwa mwanaume ili awe committed kwake.

Kwa mwanaume sex ni kitendo cha kimwili ambacho husaidia kupunguza msukumo wa hormone ya testosterone ndani ya mwili wake na baada ya kufanikisha ndipo mwanaume huanza kuhisi upendo kwa mwanamke au hujikuta mwanamke huyo hana thamani tena kama hakuna commitment (ndoa)
Ndiyo maana wanaume wengi hupotea baada ya kukipata kile walikuwa wanakitafuta kwa mwanamke kwa kuwa issue nzima ilikuwa ni testosterone na si upendo.
Ndiyo maana mwanamke kumpa mwili mwanaume mapema kabla ya ndoa ni hatari sana kwani wanawaume wengi huwa hawajawa tayari kupenda (huwa anakuwa bado hajampenda mwanamke bali ni msukumo wa testosterone).
Mwanaume huhitaji muda ili feelings zake ziwe developed na njia sahihi ambayo mwanamke anaweza kufanya ni kukaa mbali na maombi yake ya sex.
Kama ataweza kujizua kufanya sex maana yake ataweza kujenga upendo wa kweli ambao ndiyo msingi wa mahusiano, kinyume na hapo baada ya sex ataishia na mwanamke atajikuta anakuwa mtumwa.

sababu ya wewe kuwepo hapa leo ni kwa vile ancestors, wanaume na wanawake walifanya maamuzi sahihi na wakaweza kuvutia partner sahihi (best seed) ambaye leo wewe upo.
Hivyo haina haja kujisikia uchungu sana kwa mume kuhitaji sex mara kwa mara na mke kuhitaji upendo au kupendwa mara kwa mara.

7 comments:

Anonymous said...

sasa anamaana sisi ambao tuna wachumba zetu na tulalala nao ndoa tusahau?maana tayari tumeshafanya mistake hiyo mbona unatukatisha tamaa kiasi hicho?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Pole sana,
sikukatishi tamaa kwan wewe kulala na mchumba ukiamini ndo unasafisha njia ya kuolewa na mwanaume.
Mwanamke yeyote mwenye busara na maadili mema na ambaye anajitahidi kuhakikisha anapata "the best seed" kwa watoto wake, mwanaume ambaye hatamwacha na atawajibika kutunza watoto hufuata taratibu zinazotakiwa nazo ni kukaa mbali na kutojirahisisha kulala na mchumba, kichwani na moyoni amejiandika "No sex before marriage" na mwanaume ambaye hataweza kuvumilia basi ni "weak seed"
Nikikwambia kulala na mchumba kabla ya kuolewa ni mtindo wa kisasa nitakuwa nakudanganya, lazima niseme ukweli ambao mara zote huuma kama msumari kwenye kidonda kibichi, anyway ni ujinga sana kuamini kumpa mwili mchumba wako ni kujihakikishia kwamba atakuoa, ukweli ni kinyume chake, kwani akishakuchambua kama karanga kinachofuata ni kutafuta mwingine kwani kwako ilikuwa ni testosterones tu na si upendo wa kweli.
Mbona wapo mamilioni ya wanawake hujitunza na kujilinda na huo upuuzi.
Jilinde, kitunze na Mungu atakubariki na utaishi kwa amani na furaha.

Upendo ni pamoja na kutii sheria za Mungu.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Pole sana,
sikukatishi tamaa kwan wewe kulala na mchumba ukiamini ndo unasafisha njia ya kuolewa na mwanaume.
Mwanamke yeyote mwenye busara na maadili mema na ambaye anajitahidi kuhakikisha anapata "the best seed" kwa watoto wake, mwanaume ambaye hatamwacha na atawajibika kutunza watoto hufuata taratibu zinazotakiwa nazo ni kukaa mbali na kutojirahisisha kulala na mchumba, kichwani na moyoni amejiandika "No sex before marriage" na mwanaume ambaye hataweza kuvumilia basi ni "weak seed"
Nikikwambia kulala na mchumba kabla ya kuolewa ni mtindo wa kisasa nitakuwa nakudanganya, lazima niseme ukweli ambao mara zote huuma kama msumari kwenye kidonda kibichi, anyway ni ujinga sana kuamini kumpa mwili mchumba wako ni kujihakikishia kwamba atakuoa, ukweli ni kinyume chake, kwani akishakuchambua kama karanga kinachofuata ni kutafuta mwingine kwani kwako ilikuwa ni testosterones tu na si upendo wa kweli.
Mbona wapo mamilioni ya wanawake hujitunza na kujilinda na huo upuuzi.
Jilinde, kitunze na Mungu atakubariki na utaishi kwa amani na furaha.

Upendo ni pamoja na kutii sheria za Mungu.

Anonymous said...

okay ni ukweli uliowazi kaka,lakini tayari mimi nimelala nae,ina maana niachane kwa sababu hanifai tena?nitafute mwingine ambaye sitalala naye mpaka ndoa ambapo anakuwa strong seed,sasa huoni kuwa nitaingia kwenye list ya kuwapanga wanaume katika maisha yengu?siogopi kuambiwa ukweli lakini nitamani niapte mtu ambaye ataniambia nifanye nini mara baada ykufanya kosa hili<kutokana na maelezo yako yanamfaa yule ambaye hajawahi kujihusisha na mahusiano

Lazarus Mbilinyi said...

Dada hongera kwa kufahamu ukweli, kama ni dhambi umeshafanya na jambo la msingi ni kutubu na kuacha.

Jambo la msingi ni kwamba umefahamu kwamba kumpa mwili mwanaume kabla ya ndoa si ticket ya yeye kukuoa na kwamba si mpango wa Mungu, imeshatokea na umefahamu ukweli, jiulize mwenyewe je, ni kweli huyo kijana anakupenda kwa sababu ana upendo wa kweli au anataka kukuchezea tu?
Pili, ukishatembea na mwanaume ambaye unategemea kuoana naye unakuwa tayari ni second hand marriage material na anaweza akakuacha kwani anahitaji brand new marriage material kuoa so hapo ulifanya jambo ambalo ni risk huwezi kulazimisha akupende au akuoe inatokana na huyo mwanaume alikuwa na malengo gani kama kiwango chake cha testosterone kilipanda na alihitaji release basi umeumia.
Sikushauri uachane naye kwani wewe ndiye unajua urafiki wenu upoje na unaelekea wapi, pia kumbuka unapozidi kumpa mwili ndivyo anazidi kukuona huna jipya so amua mwenyewe uchukue uamuzi gani.
Tunaweza kukushauri uachane naye hata hivyo ukapata mwingine naye akafanikiwa kumrudisha ng'ombe zizini kama yule wa kwanza ikawa ni aibu kwako, so jiangalie mwenyewe kama huyo mwanaume anakupenda na ni kweli kuna mipango ya ndoa na si kupasha mashuka joto tu.

Ubarikiwe

Anonymous said...

kaka Mbilinyi ni kweli mwanaume hawezi kuishi bila sex kwa mda mrefu?ninamahusiano ya 2yrs bila sex inamaana mpenzi wangu atakuwa na mtu mwingine wa kumridhisha?

Lazarus Mbilinyi said...

Si kweli kwamba mwanaume hawezi kuishi bila sex kwa muda mrefu hata kama yeye anauhitaji wa sex kuliko mwanamke.

Mimi mwenyewe ni mwanaume mwenye sifa zote, baada ya kuoa nilienda nje ya nchi na kukaa mwaka mzima bila kujihusisha na sex na kila kitu kilienda vizuri hadi mke wangu na mtoto waliponifuata.

Linapokuja suala la uaminifu hata kama ni kweli mwanaume anauhitaji mkubwa wa sex kuliko mwanamke hiyo si ticket kwamba anatakiwa kutembea ovyo na wanawake wengine pia hii haina maana kwamba uwe na hofu kwa kuwa mpenzi wako yupo mbali na wewe na sasa ni miaka 2.

Mwanaume anaweza kuishi miaka yoyote anayotaka bila sex na kila kitu kikawa vizuri tu, sex ni akili na namna mtu amelelewa na pia maisha yake yalivyo.

Tunachosema kwenye makala ni kujaribu kueleza namna mwanaume na mwanamke wanatofautiana katika hitaji la sex ili kila mmoja afahamu namna anaweza kumsaidia mwenzake kwa maana kwamba mwanamke akiwa kwenye ndoa afahamu kwamba anahitaji kufahamu kwamba sex kwa mume wake ni hitaji la msingi sana na mwanaume anatakiwa kufahamu kwamba katika ndoa upendo ni hitaji la msingi sana kwa mwanamke.

Hivyo dadangu mwamini mpenzi wako na naamini akiamua anaweza na haina haja kutishika kwani mwanaume anaweza kuishi miaka yoyote anayotaka bila sex na akawa mwanaume wa ukweli.

Zaidi mapenzi nje ya ndoa na kabla ya ndoa ni dhambi.

Upendo daima