"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, August 26, 2010

Anamuomba mume wangu jioni na usiku tu!

SWALI
Hapa kwa jirani yangu kuna mwanamke mrembo sana ambaye ameachwa na mume wake na kubaki mwenyewe kwenye hiyo nyumba.
Kitu cha ajabu ni kwamba kila mara kukiwa na tatizo la kuhitaji msaada wa kutengenezwa kitu nyumbani kwake (kama kuweka bulbu nk ) basi huja kumuomba mume wangu akasaidie.
Nimeanza kuwa na wasiwasi na mume wangu kuwa na uhusiano usio wa kawaida na huyo mwanamke kwani kila akiitwa anaenda bila kuniuliza au kukataa hata kama alikuwa anafanya kitu cha msingi hapa nyumbani, mbaya zaidi huyu dada figure yake si utani ameumbika na kikubwa zaidi matatizo yake ya kutengenezewa vitu hutokea jioni na usiku tu na si mchana.

Najisikia wivu sana.
Je, nifanyeje ili kuondokana na hii hali na ikiwezekana mume wangu kuachana kabisa na kutoa msaada wa aina hii kwa mwanamke huyu?

MAJIBU
Kiukweli hata ningekuwa mimi kwa kweli ningejisikia wivu kama unavyojisikia wewe na una haki ya kujisikia wivu kwani inaonesha huyo mwanamke jirani yako anatumia advantage ya wema na huruma za mume wako kutimiza mahitaji yake na pia namna anafanya inaleta maswali ambayo mwanamke yeyote ambaye anampenda mume wake na kumlinda lazima ajisikie wivu.

Huyo mwanamke ameshafahamu kwamba mume wako ni mtu rahisi na mtu wa watu na kwamba anakuwa tayari kusaidia muda wowote (Pleaser) na kutokana na huo wema wake huyo mwanamke anaamini (anafahamu anachokifanya) kiasi cha kumvuta na mwishowe kutimiza malengo yake.
Ingawa hatuna ushahidi kwamba kitendo cha mume wako kuwa mkarimu kwa huyo dada kina maanisha uhusiano usio wa kawaida, bado unatakiwa kuwa makini kulinda kilicho chako kabla ya mambo kuharibika, nimefurahi kwa uwezo wako wa kugundua kwamba huo uhusiano unaweza kuleta shida kwani ni vizuri kuwa mtu wa kabla ya tukio kuliko kuwa mtu wa baada ya tukio.

Jambo la msingi ni wewe kuwa na mpango kamili (kumpa darasa mume wako kwa upendo na heshimu) ambao utasaidia mume wako kujisikia vile wewe unajisikia kwani huyo mwanamke inaonekana amewasha moto na dawa ya moto wakati mwingine ni moto, hivyo na wewe mwambie mumeo wazi na bayana vile unajisikia kwa kumpa mfano kama ifuatavyo.

Muulize yeye mumeo atajisikiaje ikitokea kuna mwanaume hapo mtaani ambaye ameachana na mke wake na akawa anakuja hapo kwenu kukuomba wewe mwanamke kwenda kumsaidia kuonja chakula alichopika kama kimeiva au ukamsaidie kumwelekeza kama sabuni anayotumia kufua nguo inaweza kutakatisha nguo au la huko nyumbani kwake saa za jioni na usiku.

Mpe hiyo picha na muulize atajisikiaje.
Ndipo umwambie ndivyo wewe unajisikia kwa kile anaanya na yule mwanamke jirai yenu, hii ndiyo njia pekee ya kumsaidia mume wako asiwe handyman hadi chumbani kwa huyo mwanamke.

Vinginevyo, tafuta simu ya fundi (handyman) yeyote unayemjua au tafuta fundi na nenda naye moja kwa moja kwa huyo mwanamke na ukifika mwambie “Nimeona hapa nyumbani kwako unahitaji fundi mara kwa mara na nimeamua kukutafutia fundi wa kudumu ambaye muda wowote, siku yoyote ukitaka msaada atakusaidia na unaweza kupanga naye ni namna gani awe anakuja kukusaidia kwani mimi na mume wangu tunahitaji muda pamoja kushughulia masuala ya familia”
Mwache fundi hapo na wewe nenda nyumbani na mwambie mumeo tukio zima.

Kama huyo mwanamke ana mishipa ya fahamu basi atafahamu umempa ujumbe gani.
Lazima umuoneshe mume wako na huyo mwanamke kwamba na wewe una backbone.

Be strong!

Ukaribu

Ukaribu (intimacy) ni kumilikiana kwa undani sana katika asili ya binadamu (the deepest nature).
Intimacy hutokea kati ya watu wawili ambao huamua ku-share siri za ndani kabisa ambazo hawawezi kumwambia mtu mwingine hapa duniani; ni siri za ndani katika mawazo na hisia. Hivi vitu vinaweza kuwa ni maumivu, mahitaji, mafanikio, kushindwa au siri yeyote.

Kimsingi, ili kuwa intimate na mtu ni muhimu sana kuwa na trust ya hali ya juu sana kwani bila trust unaweza kuumizwa ikitokea mmoja akaamua kumuacha mwenzake (abandon). Hii ina maana kwamba si jambo la busara kujiingiza haraka na kumpenda mtu kwa speed ya ajabu na kuwa intimate kabla hujamfahamu vizuri.

Pia ni hatari kubwa kwa wanandoa kukosa kuwa intimate kwani style kama hiyo ni sawa na kuishi na mgeni; mtu ambaye humjui.

Je; una siri ambazo mume wako au mke wako hazijui ila rafiki zako wanazijua?
Je; linapokuja suala la fedha mume wako au mke wako anafahamu kiasi unapokea kama mshahara au kipato?
Je, kuna kitu unamficha mke au mume wako?
Wewe ndiye shahidi mwaminifu wa maisha yako mwenyewe?

Monday, August 2, 2010

Je, Ni Special Kid?

Mimi ni "First Born" Napenda kuwa Kiongozi.
Emmanuel Lazarus Mbilinyi

Kuna jambo moja ambalo watu wengi hulichukulia mzaha, masihara au utani wakati wa kutafuta mwenzi wa maisha (mke au mume) nalo ni suala la mtoto wa kwanza kuzaliwa na mtoto wa mwisho kuzaliwa.

Swali la kujiuliza je, kuna matokeo yoyote au athari zozote kuoa au kuolewa na mtoto wa mwisho au kwanza kuzaliwa katika familia yao?

Jibu la kweli ni NDIYO KUBWA,

Kuna athari kubwa kama ni kweli unayeoana naye ni mtu wa kwanza au wa mwisho kuzaliwa ingawa kuna exceptions.

Kama una mchumba ambaye kwao ni mtoto wa mwisho kuzaliwa jambo la msingi ambalo naweza kukushauri ni wewe kuwa tayari for adventures, na kama ni mtoto wa kwanza kuzaliwa basi jiandae kuwa audited kila kitu au kukaliwa au kuongozwa bila kujali ni mwanaume au mwanamke period.

Mtoto wa kwanza kuzaliwa kawaida hujikuta ni kiongozi mahali popote na hupenda kuongoza, kupenda kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri na kama kilivyopangwa maana ndivyo alikuwa anaagizwa na wazazi kwake kuhakikisha wadogo zake wanatii kile ameagizwa;

“Hakikisha wadogo zako wamekula, wametandika kitanda, waosha vyombo, wamefagia uwanja, wamelala mapema nk”.

Mtoto wa mwisho kuzaliwa hujikuta ni mtoto hata akiwa mtu mzima kwa kuwa kwao bado ni mtoto na huwa hana shida na kitu chochote kwani kwake kila kitu ni rahisi na anapenda raha, sherehe na life is easy.

Kila kitu nyumbani kilikuwa ni kwa ajili yake kwa kuwa yeye ndiye mtoto hata baada ya kuwa mtu mzima bado anajiona ni mtoto Ndiyo maana huchelewa hata kuongea, kufanyia vitu mwenyewe kama vile kujua muda wa kula, sehemu ya kuweka nguo, kutandika kitanda, kuoga nk, yeye hujiona ni special kid, ni mtoto wa baba na mama na amekua wakati wazazi wamezoea maisha.

Kwa ujumla tabia za watoto wa kwanza kuzaliwa huwa ni kukaliwa wenzao (controlling, bossy, leading, perfectionist, auditors, no fun, firm and rigid) wengi ni viongozi na watoto wa mwisho kuzaliwa hujiona ni special kid, hujiona mtoto miaka yote, watu wa sherehe, don’t care, easy wengi ni comedians.

Je, inakuwaje wakioana mtoto wa kwanza na mtoto wa mwisho kuzaliwa?

Kama mmoja ni wa kwanza kuzaliwa na mwingine ni wa mwisho kuzaliwa (au mmoja ana tabia ya mtoto wa kwanza kuzaliwa na mwingine tabia ya mtoto wa mwisho kuzaliwa basi ndoa itakuwa nzuri kwani tabia zitawafanya wa-balance.

Uzembe wa mtoto wa mwisho utakomeshwa na mtoto wa kwanza kuzaliwa ambaye hupenda kuongoza na kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa haijalishi ni mke au mume.

Hujasikia mwanamke analalamika kwamba mume wake hakustahili kuoa au kuishi na mke, maana yake ni mtoto wa mwisho na haijalishi amesoma au hajasoma watoto wa mwisho tabia hufanana.

Je, inakuwaje wakioana wote ni watoto wa mwisho au wote watoto wa kwanza kuzaliwa?

Ukweli ni kwamba match ya ndoa ya aina hii huwa inakera sana kwani kama wote ni watoto wa kwanza kuzaliwa kila mmoja atapenda kuwa kiongozi na sidhani kama hiyo meli haitazama. Na wakikutana wote watoto wa mwisho basi ni balaa kwani ndoa itakuwa haina kiongozi na itakuwa ni adventures.

Watoto wengi wa kwanza Ndiyo marais, wachungaji na viongozi mbalimbali na watoto wengi wa mwisho ni ma-MC na comedians.

Watoto wa kwanza kuzaliwa likija suala la sex wanachagua sana na kuwa na utaratibu ambao huchosha (routine sex), pia hufanya sex kama wakaguzi kama vile lazima kuoga kabla ya sex, taa zizimwe, kusiwe na mtu hajalala usingizi within 100m, piga mswaki, usiku tu tena baada ya saa tatu na si baada ya saa nne nk, ni usumbufu.

Bila watoto wa mwisho sherehe huwa hazinogi ingawa wao tatizo lao si kawaida yao kuwahi na kufika on time kwenye sherehe, ingawa watoto wa kwanza kwao ratiba ni muhimu.

Likija suala la siasa first born wengi ni wagombea na wanapenda kuwa viongozi wakati last born ni viongozi wa kuwasemea au kushabikia first born.

Watoto wengi wa kwanza kuzaliwa ni selfish, wachoyo, hawatoi vitu kirahisi bila maelezo ya kutosha, wakati wale wa mwisho ni easy, ni rahisi, hugawa ovyo si wachoyo ni watu wa to have fun.

Kumbuka kama unaoana na mtoto wa mwisho kuzaliwa hakikisha huweki matarajio makubwa sana kwani kwake ndoa ni jambo la kawaida tu naamini wale ambao tayari mpo kwenye ndoa mnafahamu hili kwani mmmeshakutana na maajabu ya kutosha.

Pia mimi ni mmoja ya watoto wa katikati (middle) hivyo sisi ni waasi (rebels) hatutaki tabia zenu ninyi watoto wa mwisho (don’t care) na ninyi watoto wa kwanza kuzaliwa (controlling) Ndiyo maana tunajua kuboko cha mtoto wa mwisho kuzaliwa ni mtoto wa kwanza kuzaliwa ingawa mkioana na sisi watoto wa mwisho hatuna shida ndoa inaenda tu maana tunawajua sana.

Anyway ninyi watoto wa kwanza kuzaliwa ni muhimu sana kwetu maana bia ninyi ndoa zingekuwa za kizembe sana, na ninyi watoto wa mwisho ni muhimu sana maana bia nyingi ndo haziwi na sherehe wala “to have fun”, ila mmezidi yaani hata kumaliza kupaka nyumba rangi unalilia sherehe?