"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, August 26, 2010

Anamuomba mume wangu jioni na usiku tu!

SWALI
Hapa kwa jirani yangu kuna mwanamke mrembo sana ambaye ameachwa na mume wake na kubaki mwenyewe kwenye hiyo nyumba.
Kitu cha ajabu ni kwamba kila mara kukiwa na tatizo la kuhitaji msaada wa kutengenezwa kitu nyumbani kwake (kama kuweka bulbu nk ) basi huja kumuomba mume wangu akasaidie.
Nimeanza kuwa na wasiwasi na mume wangu kuwa na uhusiano usio wa kawaida na huyo mwanamke kwani kila akiitwa anaenda bila kuniuliza au kukataa hata kama alikuwa anafanya kitu cha msingi hapa nyumbani, mbaya zaidi huyu dada figure yake si utani ameumbika na kikubwa zaidi matatizo yake ya kutengenezewa vitu hutokea jioni na usiku tu na si mchana.

Najisikia wivu sana.
Je, nifanyeje ili kuondokana na hii hali na ikiwezekana mume wangu kuachana kabisa na kutoa msaada wa aina hii kwa mwanamke huyu?

MAJIBU
Kiukweli hata ningekuwa mimi kwa kweli ningejisikia wivu kama unavyojisikia wewe na una haki ya kujisikia wivu kwani inaonesha huyo mwanamke jirani yako anatumia advantage ya wema na huruma za mume wako kutimiza mahitaji yake na pia namna anafanya inaleta maswali ambayo mwanamke yeyote ambaye anampenda mume wake na kumlinda lazima ajisikie wivu.

Huyo mwanamke ameshafahamu kwamba mume wako ni mtu rahisi na mtu wa watu na kwamba anakuwa tayari kusaidia muda wowote (Pleaser) na kutokana na huo wema wake huyo mwanamke anaamini (anafahamu anachokifanya) kiasi cha kumvuta na mwishowe kutimiza malengo yake.
Ingawa hatuna ushahidi kwamba kitendo cha mume wako kuwa mkarimu kwa huyo dada kina maanisha uhusiano usio wa kawaida, bado unatakiwa kuwa makini kulinda kilicho chako kabla ya mambo kuharibika, nimefurahi kwa uwezo wako wa kugundua kwamba huo uhusiano unaweza kuleta shida kwani ni vizuri kuwa mtu wa kabla ya tukio kuliko kuwa mtu wa baada ya tukio.

Jambo la msingi ni wewe kuwa na mpango kamili (kumpa darasa mume wako kwa upendo na heshimu) ambao utasaidia mume wako kujisikia vile wewe unajisikia kwani huyo mwanamke inaonekana amewasha moto na dawa ya moto wakati mwingine ni moto, hivyo na wewe mwambie mumeo wazi na bayana vile unajisikia kwa kumpa mfano kama ifuatavyo.

Muulize yeye mumeo atajisikiaje ikitokea kuna mwanaume hapo mtaani ambaye ameachana na mke wake na akawa anakuja hapo kwenu kukuomba wewe mwanamke kwenda kumsaidia kuonja chakula alichopika kama kimeiva au ukamsaidie kumwelekeza kama sabuni anayotumia kufua nguo inaweza kutakatisha nguo au la huko nyumbani kwake saa za jioni na usiku.

Mpe hiyo picha na muulize atajisikiaje.
Ndipo umwambie ndivyo wewe unajisikia kwa kile anaanya na yule mwanamke jirai yenu, hii ndiyo njia pekee ya kumsaidia mume wako asiwe handyman hadi chumbani kwa huyo mwanamke.

Vinginevyo, tafuta simu ya fundi (handyman) yeyote unayemjua au tafuta fundi na nenda naye moja kwa moja kwa huyo mwanamke na ukifika mwambie “Nimeona hapa nyumbani kwako unahitaji fundi mara kwa mara na nimeamua kukutafutia fundi wa kudumu ambaye muda wowote, siku yoyote ukitaka msaada atakusaidia na unaweza kupanga naye ni namna gani awe anakuja kukusaidia kwani mimi na mume wangu tunahitaji muda pamoja kushughulia masuala ya familia”
Mwache fundi hapo na wewe nenda nyumbani na mwambie mumeo tukio zima.

Kama huyo mwanamke ana mishipa ya fahamu basi atafahamu umempa ujumbe gani.
Lazima umuoneshe mume wako na huyo mwanamke kwamba na wewe una backbone.

Be strong!

2 comments:

Anonymous said...

Hii kali kuliko zote. Ni kweli kabisa wanawake wa aina hii wako wengi ila kwa haya maelezo uliyotoa lazima majibu yapatikanee tu.

Barikiwa kamanda.

Anonymous said...

1.Sikunyingine msindikize au katengeneze mwenyewe.
2.Ukimwakia mumeo watatafuta kitu kingine mbali na nyumbani kwani mapenzi hayana dawa.
3.Ikinyamaza ataendelea kuenjoy kama kawaida.
4.Usimchukie hata kidogo huyo jirani yako.Mpende kwa moyo wako wote.
5.Huu ndio wakati wa kumpenda huyo mumeo. mapenzi yanyeshe kama mvua. Jibidishe, tafuta hata mambo usiyo yajua ambayo yanaweza mfanya mumeo aone umuhimu wako.
asante.