"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, September 16, 2010

Je, Mvulana au Msichana?

Nimekuwa naletewa maswali ambayo yamekuwa yakinipa picha tofauti kuhusu wafanyakazi wa ndani (house maids) hasa kwa wanawake kulalamikia waume zao au ndugu zao wa kiume kutembea na wafanyakazi wao wa ndani wa kike (house girls) na pia wanaume kulalamika kwamba wake zao hutembea na wafanyakazi wao wa ndani wa kiume (house boy)

Je, ni kweli kwamba hawa wafanyakazi ni hatari kwa ndoa zetu pia kama wanandoa wanakuwa hawapo makini?

Baada ya kupita mtaani na kuwauliza baadhi ya akina mama walikuwa na haya ya kuchangia na swali lilikuwa:-

Je, Ungependa kuwa na mfanyakazi wa nyumbani mvulana( house boy) au msichana (house girl)?

Majibu:

Binafasi napeda mfanyakazi wa ndani ambaye ni msichana kutokana na kazi ya kutunza mtoto na pia kwa usalama kwani ni rahisi kumthibiti msichana kuliko mvulana.

Wasichana ni wazuri zaidi kwa masuala ya ndani (domestic chores) ingawa nitakuwa makini kumbadilisha kabla hajaanza kufaya vitu vyake ( to have funny)

Debora – Ubungo Dar es Salaam

Mimi nitapenda kuwa na mfanyakazi wa ndani mvulana tena awe na umri wa miaka 13 hadi 16 kwani mvulana wa umri huu hawezi kuleta kasheshe ukilinganisha na wasichana wa siku hizi. Pia kuwa na mfanyakazi wa ndani msichana ni kama kuweka tangazo kwamba mume wako sasa amepata mke mwingine.

Leo maadili yameshuka sana na hawa mabinti ni hatari sana na wanaweza kufanyia lolote kuhakikisha ndoa yako inaweza kuwa tofauti kukiwa na hiyo nafasi.

Nimeshuhudia msichana wa kazi wa miaka 20 akisababisha mama mwenye nyumba kuachana na mume wake na yeye kuchukua usukani hivihivi. Hii ina maaa wasichana wa kazi wa leo wanahitaji usimamizi mkali sana hasa kutokuwa na nafasi ya kuingia chumbani hasa ukiwa hupo nyumbani na mume akiwa nyumbani peke yake na huyo binti.

Mama Robert – Ilala Dar es Salaam

Mimi napenda kuwa na mfanyakazi wa kiume kwani wapo imara na hakuna longolongo kazi ni kazi, mabinti sana sana itakuwa ni kukuzunguka ili mume wako anaswe na hata kukuibia mali zako na wakati mwingine kiburi na hata kuhakikisha mambo yako hapo nyumbani hayaendi na kukufanya mume akuone hufai na yeye anafaa na unajua nini kitafuata....

Jane – Kimara Dar es Salam

Naona hapa inabidi kuwa makini, binafsi kama nitakuwa na msichana wa kazi msichana jambo la msingi ni kuhakikisha umri wake si zaidi ya miaka 14 kwani ukiwa na msichana wa kazi ambaye ameshakua (mature) hapo unacheza na ndoa yako kwani wanaume hushawishika na kile wanaoana, wapo dhaifu sana wanapoona mabinti wanaojiremba siku hizi (matiti na mwili nusu uchi) na huyo house girl anaweza kumjaribu mume wako na anaweza kufanyia kile ambacho hakuwa nacho akilini.

Ukweli usipokuwa makini na haya mambo unaweza kujuta.

Pia sidhani kuna kitu kitaweza kunizuia kuwa na mfanyakazi mvulana hata hivyo lazima awe mvulana mdogo na si mwanaume mtu mzima kwani tumesikia wengine wameishia kubaka, kuwapa mimba wanafamilia wa kike na hata kuiba mali na kuondoka nazo, Ukweli hawa wanaume wanaopewa kazi za kufanyia ndani ya nyumba zetu ni hatari zaidi kuliko mabinti.

Mama Jenifer – Magomeni Dar es Salaam


Kwa ushauri wangu nitapenda kuwa na mfanyakazi wa ndani mwanaume kwa kuwa wao ni hodari na wapo rahisi kuliko wasichana.

Pia kama ni mwanamke ukisafiri huna wasiwasi kwa kuwa wanakuwa makini na kazi zao na si sawa na mabinti ambao unaondoka huku nyumba hujui mume wako itakuwaje na hao wasichana ambao siku hizi ni homa ya jiji.

Joyce mgaya – Sinza Dar es Salaam

Kwa upande wangu nitapenda kuwa na msichana chini ya miaka 11 kwani yeye ana upendo wa mama kwa watoto wangu na pia kazi za ndani kitu kimoja ambacho lazima niweke wazi ni kwamba hataruhusiwa kufua nguo za mume wangu au kwenda chumbani Kwangu na mume wangu.

Mvulana hapa kwani nina mabinti nyumbani na anaweza kuleta shughuli nzito kwa mabinti zangu na nikajuta.

Mama Yuster Kimara Dar es Salaam

Kwa upande wangu sihitaji mfanyakazi yeyote awe msichana au mvulana kwani mabinti zangu ni wakubwa sasa na pia naziweza kazi zangu zote za hapa nyumbani na hata kama ni nyingi watoto wangu hunisaidia.

Mama James Mbezi Dar es Salaam


Mimi nitatafuta mwanamke mtu mzima ambaye anaweza kufanyia kazi na atakuwa anafanya kazi na kurudi kwake, siwezi kuchukua wasichana wadogo ambao wamekua tayari kwani napenda mume wangu abaki wangu mwenyewe na si vinginevyo.

Mama Helena – Kimara Dar es Salaam

Je, wewe msomaji unasemaje?6 comments:

Anonymous said...

Habari kaka Mbilinyi. Mimi ni mpenzi sana wa blog yako. Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa kike na ninampenda sana mtoto wangu. Ila tatizo liko kwa mume wangu hampendi cause ni wa kike. Naomba msaada wako ili nitakapofikia kipindi nataka mtoto mwingine nipate wa kiume na hapa nilipo sina amani na ndoa yangu ila sijakata taamaa mbali na maelekezo na ushauri utakaonipa namwomba sana Mungu nipate mapacha watatu wote wa kiume au wawili wa kiume na wa kike mmoja ili niinusuru ndoa yangu na pia nimridhishe mume wangu kwani nampenda sana na ninapenda awe na amani sitaki kumkwaza. Nitafurahi sana endapo nitajibiwa

Lazarus Mbilinyi said...

Pole sana dadngu,

Ukweli ni kwamba mume wako anahitaji kuelimishwa kwamba awe mtoto wa kike au wa kiume wote wanathamani sawa mbele za Mungu na binadamu, aachane na mtazamo uliopitwa na wakati kwamba mtoto wa kiume ni muhimu kuliko wa kike.

Pia hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuamua awe na mtoto wa kike au kiume hadi Mungu mwenyewe aamue, pamoja na sayansi inavyoweza kutusaidia kupata au kutambua au kuweza kupanga kupata mtoto wa kike au kiume hata hivyo mwamuzi ni Mungu na kupata mtoto wa kike au kiume ni suala lililo nje ya uwezo wa binadamu.

Pole sana na hata hivyo kuna somo huko nyuma tulishajadili namna ya kuweza kupata mtoto wa kike au kiume ingawa bado nakazia kwamba mwamuzi wa mwishi ni Mungu mwenyewe hivyo ukipata binti sherehekea na ukipata kaka sherehekea.

Upendo daima

Anonymous said...

Nashukuru kwa ushauri wako hata mimi naamini kwa Mwenyezi Mungu kila kitu kinawezekana ni kuwa na Imani.

Hivyo naomba unikumbushe hilo somo uliliweka mwaka gani na tarehe ngapi ili niweze kufanya marejeo. Maana hata katika maandiko imeandikwa jisaidie nami nitakusaidia hivyo bado namwomba Mungu anisaidie na pia ni vyema nikafuata na ushauri nitakaousoma katika somo husika nami nikaonyesha nimefanya jitiada. Naamini Mungu atanijibu maombi yangu sijawahi ona mwenye haki ameachwa. Jina la bwana libarikiwe.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada asante sana kwa maoni yako na uelewa wako kuhusu watoto ni kweli awe mtoto wa kike au kiume wote ni watoto mbele za Mungu.

Kwa ufupi hii post inayohusu kupata mimba na kuzaa mtoto wa kike au kiume ilitoka Ijumaa ya tarehe 13 February, 2009 au unaweza copy and paste kwa hiii link http://mbilinyi.blogspot.com/2009/02/kupata-mimba.html

Anonymous said...

Nashukuru sana kaka, ubarikiwe nitafuatilia huku nikizidi kumwomba Mungu.

i think your wife is very happy with you. Mungu aibariki familia yako

Thanks

Lazarus Mbilinyi said...

Asante sana dadangu.
Mungu akusaidie ili uweze kupata watoto wa kiume mapacha.

Upendo daima