"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, September 13, 2010

Je, Utakubali?


Fikiria wewe ni binti (au mzazi wa binti) ambaye unataka kuolewa na mwanaume ambaye hajasoma (illiterate) utakubali?

Ni kweli elimu ni kitu kizuri hata hivyo elimu si kigezo cha upendo.
Naamini kitu cha msingi kwa mahusiano yoyote ni upendo wa kweli, kujali, kufanana na kuelewana.
Ukweli binafsi nitakubali kuolewa na mwanaume illiterate kwani inawezekana ana sababu za msingi za yeye kutokwenda shule na baada ya kuoana tunaweza kushauriana ajiendeleakimasomo.
Joyce M.

Ukweli nitaolewa na yule nimeamua na nimempenda na angalau awe ameelimika.
Sidhani kama nitaweza kukubali ombi la mwanaume yeyote kunioa wakati hana elimu yoyote na hajaelimika, je itakuwaje kwa watoto tutakao wazaa? Je anaweza kupata kazi nzuri kwa ajili ya kuleta kipato cha familia huku hajasoma?
Pia kwa kuwa mimi mwanamke nimesoma na yeye hajasoma maana yake hatufanani na kutokuwa na gap kubwa sana katika uelewa wa mambo kitu ambacho sikipendi.
Margaret S.

Nimeona mfano halisi wa dada ambaye alikuwa na elimu ya kidato cha sita na akaoewa na kaka mwendesha pikipiki ambaye alikuwa hana shule na hajaelimika kwa lolote.
Baada ya dada kuolewa kilichofuata ni kulea mtoto mmoja baada ya mwingine hadi ndoto zake za kuwa lawyer zikafutika.
Pia huyu mwanaume illiterate huwa hana shukurani kwa namna yule dada anavyojitahidi kuhakikisha anaanya kila analoweza familia iwe na mkate wa kila siku na kusomesha watoto.
Sitakubali binti yangu ajiingize kwenye ujinga kama huo hata siku moja na pia nitajitahidi kuelimisha mabinti wasije ingia katika matatizo kama hayo.
Mrs Christina B.


Kama kuna upendo na kuna kufahamiana na kuelewana na kama ni kweli huyu mwanaume ana sifa ninazohitaji Ukweli nitakubali tuoane na nitaomba Mungu aniongoze.
Julieth M.

Kwangu kuwa illiterate si kizuizi hasa linapokuja suala la mahusiano pale tu kukiwa na kuelewana kati yangu mimi binti na huyo mwaname na kama ana sifa zile niahitaji. Najua kuna matatizo na watu watasema sana kwa kumkubali huyo kaka ambaye hana shule kabisa hata hivyo kama kuna kujitoa na kumuomba Mungu hakuna lisilowezekana.
Esther L.

Binafsi siwezi kujiingiza kwenye jaribu la kijinga kama hilo na kuona na mwanaume ambaye hajaenda shule.
Anne K.
Na Je, wewe msomaji ungekubali? Au unasemaje ?

6 comments:

Anonymous said...

bwana asifiwe kaka,nashukuru kuwa umerudi likizo.kuhusu hii mada mimi niko pamoja na julieth,nitakubali kuolewa na mwanaume ambaye hajasoma,ninachoangalia ni upendo,tabia,imani,jinsi gani anampenda Mungu,haya mengine tutajadili tukiwa tayari wachumba tufanyeje ili tuwe tunafanana kielimu,Mungu akubariki kwa mada hii,watu wengi wamekuwa wakienda sana kimwili badala ya kiroho matokeo yake wakiingia ndani wanaanza kushindana kwa sababu hawakumtanguliza mungu.Ek

Anonymous said...

Elimu ina nafasi yake katika mahusiano ila sidhani kama ni kigezo kikubwa sana cha msingi ni kuangalia uelewa wa mtu pamoja na upendo alionao maana kuna mtu unakuta kuwa hakupata nafasi ya kusoma hadi kufikia level ya juu ila ni mwelewa na hata kama atarudi darasani anauwezo wa kufika mbali.Ila kama binti una Degree ya kwanza basi mwanaume at least awe amefika form four.Zaidi ya yote UPENDO wa kweli ndilo jambo la msingi.

auguzburg said...

mimi mwenyewe ni mfano,elimu yangu ni ya chuo lakini mpenzi wangu yeye kaishia form two na tupo kwenye mkakati wa ndoa. elimu kwangu si kikwazo kwani nampenda sana,pia ni muelewa sio kwamba alikimbia shule bali uwezo wa familia ndio ulimkwamisha. UPENDO NDO MUHIMU

Lazarus Mbilinyi said...

Asante kwa maoni mazuri ingawa wengine wanasema wapenzi wao wameishia kidato cha pili kitu ambacho kinawafanya wawe wamesoma, hapa tunaongelea mtu ambaye hajawahi kwenda shule kabisa hajui a, e, i, o u zinasomwaje au mwanaume au mwanamke je, utakubali kuoana naye?

Anonymous said...

Kuoana na mwanaume ambae hajui kabisa hata kusoma itakuwa ngumu kwangu maana hata hesabu kama anafanya biashara zitamshinda. kwa hilo siwezi mshauri mtu. Mungu ni mwaminifu siku zote kama tukiomba na ameahidi kutupa watu wa kufanana nao.

Anonymous said...

Mmmh huu mtihani
Mimi binafis kwanza nitamuuliza Mungu.

HATA KAMA HUYU MWANAUME HAJASOMA unaweza kukuta ana pontential kubwa kimaisha so kuna vitu vingi vya kuangalia hadi kufikia kuona.

A.MTAZAMO WAKE
B.MAISHA YAKE.
C.MIPANGILIO YAKE.
D.JE ANA HOFU YA MUNGU
E.UKOO WAKE.
F.HISTORIA YAKE/YAO UKOO MZIMA
G.MAWAZO YAKE NI YA KUJENGA AU KOBOMOA?
H.UKWELI / UONGO
I.UPENDO WA DHATI

Yote hayo hapo juu yanahitaji muda wa kuyapatia majibu.

ANITHA M.