"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, September 6, 2010

Malezi ya Mtoto


Wazazi wote yaani baba na mama wana mchango sawa katika malezi na maendelea ya mtoto katika familia.
Kihistoria na hata globally kazi au jukumu la kulea mtoto hupewa mwanamke na nchi nyingi zilizoendelea kama Canada na USA mwanamke hupewa jukumu la kuwa ndiye mwenye jukumu la kulea mtoto (primary care giver) hii ina maana hata ikifika siku mke na mume wakatengana watoto ni wa mama na si baba na mama atasaidiwa na serikali kuhakikisha watoto wanalelewa na kupata mahitaji ya msingi na si baba labda kuwe na uthibitisho kwamba mama anawatenda vibaya (abuse) watoto ndipo baba huchukua watoto.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba mwanamke na mwanaume hutofautiana katika misingi, imani na namna ya kulea mtoto.
MFANO
Wanaume mara nyingi katika mawasiliano kwa watoto hutoa amri (instruct) wakati wanawake hupendekeza; lugha ya mwanaume ni ya nguvu (powerful), moja kwa moja (direct), wazi, na mara nyingi wanaume hujikuta ni watawala (dominant/authority)
Wanaume huangalia saa na wanawake huangalia watoto, wanaume hupenda kutoa ushauri unaoendana na saa, ratiba, orodha, scale na kalenda wakati wanawake hujikuta wanahangaika na kuwaza jambo badala ya kutoa solutions za tatizo
Wanaume wengi huwa huru na stress wakati wanawake wengi hukumbwa na stress za maisha hasa katika suala la kulea watoto.
HII INA MAANA GANI?
Kama mtoto amepanda juu ya mti; mama atamwambia mtoto shuka juu ya mti na inatosha unaweza kuanguka, wakati baba atamsifia na kumwambia mtoto apende juu tawi moja zaidi.
Kama mtoto amefaulu mtihani; baba atamwambia mtoto ahakikishe anaendelea kuishinda na mitihani ijayo wakati mama mara nyingi atamwambie pamoja na kufualu mitihani ni muhimu ahakikishe anakuwa na tabia njema kwani kwa mama tabia njema ni muhimu sana katika kumfanya mtoto afaulu vizuri.
HATA HIVYO
Hawa wanaume hawajawahi kubeba mimba, hawajawahi kuzaa, hawjawahi kunyonyesha hata hivyo tafiti nyingi zinaeonesha kwamba wanaume ndiyo wataalamu wa kutoa ushauri na wametandika vitabu vingi vya malezi ya watoto kuliko wanawake.
Kijamii, ushauri kuhusu mimba, kuzaa na kulea watoto imekuwa inarithishwa (handed) kutoka mwanamke hadi mwanamke au kutoka kwa mama kwenda kwa binti yake kwa misingi ya hisia, mbinu na uelewa wao na mwanaume hakuhusika kwa lolote katika hayo hata hivyo sasa mambo yanabadilika kiasi kwamba mwanaume ameingilia masuala ya ushauri wa mimba, kuzaa na malezi ya watoto.
Ni vizuri baba na mama kushirikiana katika malezi ya watoto kwani kila moja ana sehemu yake katika kumuandaa mtoto na pia mtoto ajifunze namna baba na mama wanafanya (treat each other) na zaidi wazazi kuwa role model.
Wazazi kuwa model maana yake ni kumpa mtoto tabia halisi (genuine, consistency, desirous of imitation) ambayo anaweza kuichukua kwa ajili ya maisha yake ndoa yake baadae

No comments: