"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, October 15, 2010

Kufika huko!

Wapo wanawake wambao huamini suala la kufika kileleni (orgasm) huja automatically bila juhudi yoyote. Ingawa kwa mwanaume suala la kufika kileleni ni tofauti na sidhani kama kuna mwanaume anaweza kufanya sex bila kufika kileleni.

Katika ndoa suala la kufika kileleni kwa mwanaume ni suala la kujizuia ili asimalize mapema zaidi ya mke kuridhika.

Kwa upande mwinginewanawake wengi hawajawahi kufika kileleni na wapo ambao hata hawajui kufika kileleni ni kitu gani.

Pia kiwango cha kufika kileleni kutofauti kati ya mwanamke na mwanamke .

Ni jambo la msingi kwa mwanamke kujua kipimo halisi cha kufahamu amefika kileleni au la kwani mwanamke ambaye amefika kileleni katika tendo la ndoa hujisikia tofauti zaidi na yule ambaye hakuweza kufika.

Wakati mwanaume na mwanamke wanafanya maandalizi ya tendo la ndoa (foreplay) ili kusisimuana na kila mmoja kuwa tayari kwa ajili ya tendo la ndoa (intercourse) na wakati wanaendelea na tendo la ndoa huwa anatengeneza nguvu au msukumo (tension) ambayo hupanda kiasi cha kutaka kulipuka (explode) kama namna mwili unajiandaa kupiga chafya.

Na baada ya hiyo nguvu kuwa released awe mwanamke au mwanaume hujisikia relaxed na satisfied na kama hawajafika mmoja hasa mwanamke huweza kujisikia frustrated na bored kama vile alitaka kupiga chafya na ikashindikana.

Suala la kujiuliza haivi kwa nini wanawake wengi hushindwa kufika kileleni?

Kuna mambo mengi yanayochangia mwanamke kushindwa kufika kileleni na mojawapo ni kama ifuatavyo

1. MALENGO

Kama mwanamke na mwanaume wote kwa pamoja wanaingia chumbani kufanya mapenzi lengo likiwa kufika kileleni basi ni vigumu sana kufika kileleni kwani lengo la tendo la ndoa ni kuridhishana, kuonesha upendo kwa matendo kila mmoja kumtanguliza mwenzake, kutoa na kupokea, siyo kuulizana

“je, umefika kileleni?

Hili ni illegal question chumbani.

Bottom line:

Jambo la msingi ni kupeana raha na kila mmoja kuhakikisha anampa mwenzake raha zaidi ya kawaida na matopkeo yake ni mwanamke kufika kileleni.

2. NI SUALA LA KUJIFUNZA

Wapo wanawake ambao ni very lazy hata katika issues muhimu sana za maisha yao. Wapo wanawake wanaamini suala la kufika kileleni ni suala na wajibu wa waume zao, labda uwe mwanamke mwenye bahati kubwa kimaumbile kwamba unaweza kufika kileleni kila Mr happy anapokugusa tu ila ukweli ni kwamba unahitaji kujifunza, kuwa na uzoefu na inachukua kazi na kujizoesha na pia kujivumbua mwenyewe kujua ni namna gani mume wako anaweza kukufikisha kileleni huku ukisaidiana naye.

Huwezi kuendesha gari bila kujifunza, huwezi kuwa mwanasheria bila kujifunza na kufika kileleni Je?

3. KUJIFAHAMU MWENYEWE

Mwanamke anahitaji kujifahamu mwenyewe namna mwili wake unaweza kusisimuliwa na kujifahamu wapi na namna gani kila kiungo kinaweza kumpa raha nk.

4. MAZOEZI YA KEGEL

Imethibitishwa bila wasiwasi na shaka kwamba mwanamke ambaye anafanya mazoezi ya misuli ya PC huweza kufika kileleni kirahisi kuliko yule ambaye hiyo misuli imelegea.

Zaidi soma hapa

5. KUWAJIBIKA

Mwanamke unahitaji kuwa active participant wa sex na mume wako si suala la kulala tu kama furushi na kusubiri mume wako afanye kila analoweza kukupa raha hadi ufike kileleni. Kama unataka mume akuone ovyo na boring basi kaa kimya muda wote usifanye chochote.

Kujifunza zaidi soma hapa

Tutaendelea!

Tuesday, October 12, 2010

Hivi ni Mara Ngapi?

SWALI:

Samahani sana kwa swali langu, ila kwa kweli napenda kufahamu hivi ni mara ngapi wanandoa wanatakiwa kuwa na tendo la ndoa (sex) kwa wiki au mwezi ?

Kwani kila mtu ninayemuuliza ananipa jibu lake na kidogo inanichanganya, na wakati huohuo mume wangu kuna siku anakuwa mkali na mchungu hata kama sijakosea kitu chochote.

Msaada wako kaka Mbilinyi!

____________________________

MAJIBU:

Dada asante sana kwa swali zuri ambalo linawakilisha wanawake na wanaume wengi katika ndoa hasa wale ambao hufika mahali wakajikuta hawaridhiki na mwenendo mzima wa suala la sex katika ndoa zao.

Naamini umeuliza hili swali kwa sababu ni swali muhimu linalohusu ndoa yako.

Kumbuka jambo la msingi katika swali lako (bottom line) ni kwamba kawaida (mara ngapi sex iwe kwa siku, wiki au mwezi) ni suala la wewe na mume wako kuzungumza, kuelewana na kukubaliana au wewe mwenye binafsi kufika mahali ukafahamu kwamba mume wako na wewe kila mmoja ana hamu ya kimapenzi kiasi gani kwa siku au wiki au mwezi kwa maana kwamba kumfahamu mwenzako uhitaji wake na kila ndoa duniani ipo tofauti kwa maana kwamba wengine hufanya sex kila siku, wengine kwa wiki mara 1 au 2 au 3 na wengine kwa mwezi mara 1 au 20 na wengine hata wakifanya sex kwa mwaka mara 1 wanaona sawa tu.

Unanikumbusha mama mmoja aliyelalamika kwamba mume wake anamtaka sex mara 10 hadi 15 kwa siku iwe mchana au usiku hadi akaomba kujirudi nyumbani kwao kwa wazazi kwani amechoka na mwanaume wa aina hiyo, tuache hayo!

Kujihusisha na sex mara kwa mara kwa wanandoa hutokana na afya, emotions, kubadilika kwa maisha, stress, depressions, migogoro, kufiwa na kazi na uchumi hata watoto nk na kiwango cha kuhitaji sex hakiwezi kuwa sawa au juu maisha yote kwani kuna uhusiano mkubwa sana kati ya sex na akili.

Kama mume wako ni mkali (grouchy/irritable) inawezekana hormones zake za testosterones zimepanda sana zinahitaji release na njia muafaka kwake ni wewe kuwa available (kumpa sex).

Inawezekana huko kazini boss anamkalia sana mume wako kiasi kwamba akirudi nyumbani anahitaji mwanamke ambaye anaweza kumfariji na kumpa caring na attention kubwa kwake.

Ndoa ni kufanya kila kitu pamoja, kuelewana, kuzungumza na kuwasha moto wa kimapenzi ili kila mmoja aridhishwe kimapenzi na wewe ni mwanamke ambaye ni halisi kwa ajili yake.

Hivyo unahitaji kuwa mwangalifu kusoma namna upepo unavuma hapo nyumbwani, ukiona ana dalili kwamba anakuhitaji kimapenzi unahitaji kuwa available bila kujali mnafanya sex mara ngapi kwa wiki, kwani suala la msingi si mara ngapi kwa siku au wiki bali kunaridhika au kuridhishwa kiasi gani na mume au mke wako.

Wewe ni mwanamke na una advantage kubwa kwani ni rahisi sana kumsoma mume wako na pia hata kama alikuwa hataki sex na wewe unahitaji bado ni rahisi sana kuwasha umeme (kumfanya awe stimulated) na kuhakikisha Mr. happy wake anashawishika kukubali ombi lako kwani kwa urembo wako na uzuri wako hakuna kisichowezekana.

You are a woman beautifully and masterfully created.

Siku njema

Thursday, October 7, 2010

Ni Mafumbo

Suala la mawasiliano ktk ndoa limeelezwa na kujadiliwa na maelfu ya vitabu vya masuala ya ndoa na mahusiano.

Hata hivyo swali bado linakuwa kwa nini ni vugumu sana kwa mke na mume kuwasiliana vizuri na kuongea na hata kuelewana?

Tatizo kubwa ni kwamba pande zote mume na mke huongea ua kupeleka ujumbe kwa namna ya mafumbo (codes) bila yeye mwenye kutoa huo ujumbe kufahamu kwamba anaongea kwa mafumbo.

Hii ina maana kwamba kile mmoja anaongea si kile mwenzake anakisikia na yule aliyesikia anaamini kile amesikia ni kile mwingine ana maanisha kitu ambacho si kweli.

MFANO

Baada ya kuamka na kujiandaa na kuwa tayari kwenda kazini sasa wakati wanavaa nguo asubuhi wawahi kazini, Jane anamwambia mume wake aitwaye James;

“Sioni nguo ya kuvaa leo”

Huku akiwa na maana kwamba hana nguo mpya kwa muda mrefu.

Siku ya pili yake james naye asubuhi anamwambia mke wake jane kwamba;

“Sioni nguo ya kuvaa”

Huku akimaanisha haoni nguo safi ya kuvaa.

Kutokana na aina hii ya mawasiliano ni wazi kwamba kunaweza kutokea mgogoro mkubwa sana kwani kama suala la “sina nguo ya kuvaa” huwa na maana tofauti kwa kila mmoja je masuala mengine?

Kumbuka kuwasiliana kati ya mke na mume ni pamoja na kufahamu tofauti zilizopo kati ya Mwanamke na Mwanaume katika kuwasiliana kwani kila gender ina namna yake.

Wednesday, October 6, 2010

Muhimu sana Kufahamu!

KWA WANAWAKE TU:

Nini cha kutarajia kutoka kwa mpenzi wako mkiwa na faragha chumbani kwenu?

MOJA

Haijalishi ni handsome kiasi gani au msomi kiasi gani hadi anaitwa Dr. au Professor; haijalishi ni diplomat au businessman au mbunge au tajiri linapokuja suala la sex wanaume wengi (siyo wote) ni zero wa kufahamu nini kinaweza kumfanye mwanamke asisimke na kufurahia sex.

MBILI

Usijidanganye kwamba anajua mapenzi hata kama huko nyuma aliwahi kuwa na mpenzi.

Ukiwauliza wanaume wengi kisimi (clitoris) ni kitu gani katika mwili mwanamke, wanakuuliza kwa mshangao “Unasema kitu gani?”

TATU

Usijidanganye kwamba anajua ramani ya kupita (roadmap) katika kukufikisha kwenye raha ya mapenzi (kileleni) kama unavyohitaji bila wewe kumwambia; Ukweli ni kwamba unahitaji kumwambia si mara moja tu bali mara kwa mara vile unapenda akufanyie ili ufurahie sex na yeye kama vile;

Mpenzi huwa najisikia raha sana unapofanya hivi au vile”

“Nilipenda sana na kiujisikia raha sana jana ulipoanza kwa kufanya hivi ila leo ningtependa uanze hivi”

“Huwa najisikia raha unavyochezea ………………….. namna hivi”

Baada ya hapo relax na mwache aendee kukupa raha!


KWA WANAUME TU:

Nini mpenzi wako (mke wako) anahitaji kutoka kwako mkiwa faragha!

MOJA

Usifikirie sex ni bingo, sex ni sehemu ya mahusiano na ni kitu ambacho ni ziada baada ya kuimarisha na kutimiza mambo mengine katika mahusiano hata kama ni madogo madogo lakini kwa mke wako ni mambo muhimu kama vile kumsaidia kazi, kumwambia “nakupenda” kupiga naye story mbalimbali za maisha kwa upendo, kupeana zawadi nk.

Mwambie Mr Happy awe mtulivu.

MBILI

Jitahidi kutimiza mahitaji ya mpenzi wako kwanza ndo yaje yako kila eneo la maisha yenu ya mahusiano.

TATU

Fahamu kwamba mpenzi wako anahitaji mazingira ya kimapenzi romantic, kujisikia unamjali (caring), unamwamini (trust) , kiasi cha kujisikia salama (safe/protected) na si kukimbilia sex.

Baada ya hapo hayo mengine utazidishiwa na atajituma kukupa kile unahitaji.Monday, October 4, 2010

Ni Uamuzi wako

Ikitokea mchanga ukaingia kwenye jicho basi jicho litauma na kama halitatafutiwa ufumbuzi basi jicho linaweza kupoteza uwezo wa kuona na unaweza kuwa kipofu.

Hata hivyo huo mchanga ukiwekwa kwa kombe (oyster/shell-fish) husababisha usumbufu ambao humfanya atoe mng’ao kama wa lulu (pearly).

Suala muhimu la kujiuliza ni je, mchanga ni kisababishi cha msingi cha jicho kuuma au kwa kombe kutoa rangi nzuri za kung'aa kama lulu?

Kama mchanga ni kisababishi basi matokeo yangekuwa sawa kwa jicho na kombe.

Kilichofanyika ni kwamba mchanga umetumika kama ni wakala (agent) wa kudhihirisha tabia za ndani za jicho na Kombe.

Linapokuja suala la mahusiano hii ina maana unapoona mke wako au mume wako anafanya maisha kuwa magumu, machungu (irritable) unaweza kuamua kuwa kama mchanga kwenye jicho au mchanga kwenye kombe.

Kama hujaelewa basi nikupe mfano mwingine!

Unajua nini kitatokea kama utaweka udongo wa mfinyanzi na ice cream kwenye jua kali la mchana?

Udongo wa mfinyanzi utakuwa mgumu kama jiwe na ice cream itayeyuka na kuwa maji.

Je, hii ina maana gani?

Hii ina maana kwamba joto la jua hudhihirisha tabia za ndani za udongo wa mfinyanzi na icecream.

Inawezekana mume wako au mke wako ni mtu irritant muda wote, ni kweli hiyo haipingiki (it is given) maana yake hapo una maamuzi mawili tu

Kwanza ni kuitikia kwa busara (njia ya kimungu) na pili kuitikia kwa ujinga na kipuuzi zaidi ukawa kama mchanga na jicho au jua na udongo wa mfinyanzi nah ii kamwe si njia sahihi.

Kumbuka ni rahisi sana kulaumiana au kumlaumu sana mwenzako kwenye ndoa. Hata hivyo kupitia njia ya lawama utaishia kuwa victim na utakosa dhawabu kwa Mungu.

Jambo la msingi la kukumbuka kwamba unapoona Mume wako au mke wako anapandisha joto, anakuwa irritant, mtu wa blaming, critical; lazima ukumbuke kwamba

Kama mtu mzima mwenye uhuru kamili ndani yako na unafahamu wazi kabisa unawajibika kumjibu majibu mawili la kujenga na kubomoa, la kufurahisha na la kuudhi la amani au vita.

Jibu la kumpa Mungu utukufu au kumchukiza nk.

Kumbuka unao uamuzi wa kufanya vizuri au vibaya, kuchukia au kufurahi bila kujali mwenzio wako amefanya vibaya namna gani kwani yeye ni wakala tu wa kusaidia wewe kuonesha true colours ulizonazo.