"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, October 12, 2010

Hivi ni Mara Ngapi?

SWALI:

Samahani sana kwa swali langu, ila kwa kweli napenda kufahamu hivi ni mara ngapi wanandoa wanatakiwa kuwa na tendo la ndoa (sex) kwa wiki au mwezi ?

Kwani kila mtu ninayemuuliza ananipa jibu lake na kidogo inanichanganya, na wakati huohuo mume wangu kuna siku anakuwa mkali na mchungu hata kama sijakosea kitu chochote.

Msaada wako kaka Mbilinyi!

____________________________

MAJIBU:

Dada asante sana kwa swali zuri ambalo linawakilisha wanawake na wanaume wengi katika ndoa hasa wale ambao hufika mahali wakajikuta hawaridhiki na mwenendo mzima wa suala la sex katika ndoa zao.

Naamini umeuliza hili swali kwa sababu ni swali muhimu linalohusu ndoa yako.

Kumbuka jambo la msingi katika swali lako (bottom line) ni kwamba kawaida (mara ngapi sex iwe kwa siku, wiki au mwezi) ni suala la wewe na mume wako kuzungumza, kuelewana na kukubaliana au wewe mwenye binafsi kufika mahali ukafahamu kwamba mume wako na wewe kila mmoja ana hamu ya kimapenzi kiasi gani kwa siku au wiki au mwezi kwa maana kwamba kumfahamu mwenzako uhitaji wake na kila ndoa duniani ipo tofauti kwa maana kwamba wengine hufanya sex kila siku, wengine kwa wiki mara 1 au 2 au 3 na wengine kwa mwezi mara 1 au 20 na wengine hata wakifanya sex kwa mwaka mara 1 wanaona sawa tu.

Unanikumbusha mama mmoja aliyelalamika kwamba mume wake anamtaka sex mara 10 hadi 15 kwa siku iwe mchana au usiku hadi akaomba kujirudi nyumbani kwao kwa wazazi kwani amechoka na mwanaume wa aina hiyo, tuache hayo!

Kujihusisha na sex mara kwa mara kwa wanandoa hutokana na afya, emotions, kubadilika kwa maisha, stress, depressions, migogoro, kufiwa na kazi na uchumi hata watoto nk na kiwango cha kuhitaji sex hakiwezi kuwa sawa au juu maisha yote kwani kuna uhusiano mkubwa sana kati ya sex na akili.

Kama mume wako ni mkali (grouchy/irritable) inawezekana hormones zake za testosterones zimepanda sana zinahitaji release na njia muafaka kwake ni wewe kuwa available (kumpa sex).

Inawezekana huko kazini boss anamkalia sana mume wako kiasi kwamba akirudi nyumbani anahitaji mwanamke ambaye anaweza kumfariji na kumpa caring na attention kubwa kwake.

Ndoa ni kufanya kila kitu pamoja, kuelewana, kuzungumza na kuwasha moto wa kimapenzi ili kila mmoja aridhishwe kimapenzi na wewe ni mwanamke ambaye ni halisi kwa ajili yake.

Hivyo unahitaji kuwa mwangalifu kusoma namna upepo unavuma hapo nyumbwani, ukiona ana dalili kwamba anakuhitaji kimapenzi unahitaji kuwa available bila kujali mnafanya sex mara ngapi kwa wiki, kwani suala la msingi si mara ngapi kwa siku au wiki bali kunaridhika au kuridhishwa kiasi gani na mume au mke wako.

Wewe ni mwanamke na una advantage kubwa kwani ni rahisi sana kumsoma mume wako na pia hata kama alikuwa hataki sex na wewe unahitaji bado ni rahisi sana kuwasha umeme (kumfanya awe stimulated) na kuhakikisha Mr. happy wake anashawishika kukubali ombi lako kwani kwa urembo wako na uzuri wako hakuna kisichowezekana.

You are a woman beautifully and masterfully created.

Siku njema

4 comments:

Anonymous said...

habari kaka

Hapo kakangu nakupa tano, ni kweli sex haina muda wala mara ngapi, nimuda wowote kila mtu anapo muhitaji mwenzie, hata kama mke anapika, mme akimuhitaji na mke akaridhia mambo shwari.hata kama mnaoga inawezekana pia, sex inahitaji mazingira tofauti tofauti

Labda kama ni wagonjwa na mmeshauriwa na daktari hayo ni mambo mengine.

ubarikiwe sana.

Lazarus Mbilinyi said...

Asante kwa maoni mazuri,

Ni kweli kwa wanandoa sex ni muda wowote mahali popote jambo la msingi ni privacy (msije dakwa na polisi).

Pia ni kweli raha ya sex katika ndoa ni kuwa na mazingira tofauti.

Ukweli ni kwamba mahali popote ambapo binadamu amefika basi sex inawezekana kufanyika!

Have fun!

Anonymous said...

Helw! Kaka mi nna tatizo kaka ni mwanafunzi na ttzo langu kubwa ni kupiga punyeto! Nimekua nikipoteza mda wangu wa kusoma kwa kupiga nyeto! Kwa cku naeza piga hata mara 6! Naomba nisaidie nifanyeje! Pia hali hii imenifanya nipoteze mda mwingi kutafuta sex materials instead ya kusoma coz mwakani mwezi wa pili nafanya mtihani! Af pia nimekua msahaulifu sanaaaa! Cjui ni madhara amaa!! Nilianza mchezo huo nikiwa mdogo sielew ulitoka wapiii! Nisaidie coz nimekua addicted! nifanyeje... Nikiangalia unanipotezea mda mwingi na nina malengo ya kufaulu mtihani!! Love... Liz

Lazarus Mbilinyi said...

Liz,

Pole sana kwa tatizo ulilonalo, ni kweli addiction yoyote ina tatizo na madhala makubwa (kama vile sigara, pombe, pornography nk)
Pia Inawezekana kuacha na kubadilika kabisa jambo la msingi ni kufuata maelezo na yale nitakayo kwambia.

Kwa kuanza naomba nitumie email kwa lazarusmbilinyi@gmail.com ili tuweze kusaidiana kwa kujua tatizo limeanzia wapi na iweje.

Tuwasiliane kwa Mungu hakuna lisilowezekana

Laz