"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, October 15, 2010

Kufika huko!

Wapo wanawake wambao huamini suala la kufika kileleni (orgasm) huja automatically bila juhudi yoyote. Ingawa kwa mwanaume suala la kufika kileleni ni tofauti na sidhani kama kuna mwanaume anaweza kufanya sex bila kufika kileleni.

Katika ndoa suala la kufika kileleni kwa mwanaume ni suala la kujizuia ili asimalize mapema zaidi ya mke kuridhika.

Kwa upande mwinginewanawake wengi hawajawahi kufika kileleni na wapo ambao hata hawajui kufika kileleni ni kitu gani.

Pia kiwango cha kufika kileleni kutofauti kati ya mwanamke na mwanamke .

Ni jambo la msingi kwa mwanamke kujua kipimo halisi cha kufahamu amefika kileleni au la kwani mwanamke ambaye amefika kileleni katika tendo la ndoa hujisikia tofauti zaidi na yule ambaye hakuweza kufika.

Wakati mwanaume na mwanamke wanafanya maandalizi ya tendo la ndoa (foreplay) ili kusisimuana na kila mmoja kuwa tayari kwa ajili ya tendo la ndoa (intercourse) na wakati wanaendelea na tendo la ndoa huwa anatengeneza nguvu au msukumo (tension) ambayo hupanda kiasi cha kutaka kulipuka (explode) kama namna mwili unajiandaa kupiga chafya.

Na baada ya hiyo nguvu kuwa released awe mwanamke au mwanaume hujisikia relaxed na satisfied na kama hawajafika mmoja hasa mwanamke huweza kujisikia frustrated na bored kama vile alitaka kupiga chafya na ikashindikana.

Suala la kujiuliza haivi kwa nini wanawake wengi hushindwa kufika kileleni?

Kuna mambo mengi yanayochangia mwanamke kushindwa kufika kileleni na mojawapo ni kama ifuatavyo

1. MALENGO

Kama mwanamke na mwanaume wote kwa pamoja wanaingia chumbani kufanya mapenzi lengo likiwa kufika kileleni basi ni vigumu sana kufika kileleni kwani lengo la tendo la ndoa ni kuridhishana, kuonesha upendo kwa matendo kila mmoja kumtanguliza mwenzake, kutoa na kupokea, siyo kuulizana

“je, umefika kileleni?

Hili ni illegal question chumbani.

Bottom line:

Jambo la msingi ni kupeana raha na kila mmoja kuhakikisha anampa mwenzake raha zaidi ya kawaida na matopkeo yake ni mwanamke kufika kileleni.

2. NI SUALA LA KUJIFUNZA

Wapo wanawake ambao ni very lazy hata katika issues muhimu sana za maisha yao. Wapo wanawake wanaamini suala la kufika kileleni ni suala na wajibu wa waume zao, labda uwe mwanamke mwenye bahati kubwa kimaumbile kwamba unaweza kufika kileleni kila Mr happy anapokugusa tu ila ukweli ni kwamba unahitaji kujifunza, kuwa na uzoefu na inachukua kazi na kujizoesha na pia kujivumbua mwenyewe kujua ni namna gani mume wako anaweza kukufikisha kileleni huku ukisaidiana naye.

Huwezi kuendesha gari bila kujifunza, huwezi kuwa mwanasheria bila kujifunza na kufika kileleni Je?

3. KUJIFAHAMU MWENYEWE

Mwanamke anahitaji kujifahamu mwenyewe namna mwili wake unaweza kusisimuliwa na kujifahamu wapi na namna gani kila kiungo kinaweza kumpa raha nk.

4. MAZOEZI YA KEGEL

Imethibitishwa bila wasiwasi na shaka kwamba mwanamke ambaye anafanya mazoezi ya misuli ya PC huweza kufika kileleni kirahisi kuliko yule ambaye hiyo misuli imelegea.

Zaidi soma hapa

5. KUWAJIBIKA

Mwanamke unahitaji kuwa active participant wa sex na mume wako si suala la kulala tu kama furushi na kusubiri mume wako afanye kila analoweza kukupa raha hadi ufike kileleni. Kama unataka mume akuone ovyo na boring basi kaa kimya muda wote usifanye chochote.

Kujifunza zaidi soma hapa

Tutaendelea!

2 comments:

Piencia said...

Habari kaka mbilinyi, naona umetusahau kabisa ndugu yangu kwani umekuwa kimya muda sasa.

nina swali,mme wangu hajatahiriwa, na mimi naogopakumwambia akatahiriwe kwani tuna miaka 22 ya ndoa sasa,nayeyendie aliye nifundisha mapenzi,niliwahi kutoka nje ya ndoa na kukutana na kijana mwenzngu nikakuta ametahiriwa nilifurahia sana zana yake kuliko ya mme wangu, yeye ana miaka 50 amenizidi miaka 12, sasa nifanyeje? samahani sana kwa swali hili.

wako dada Piencia

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Piencia,

Asante sana kwa swali zuri, ni kweli kujadilia masuala la sex kwa mke na mume ni moja ya topic ngumu sana duniani kwa wanandoa wengi. Inakuwa ngumu zaidi kwa kuwa jambo unalotaka kujadilia ni jipya na anaweza kukuuliza kwa nini usingeniuliza miaka 19 iliyopita leo imakuwaje nani kakufundisha?

Hata hivyo huyo ni mume wako na jambo la msingi ni wewe kukaa naye na kuongea naye kwa upendo kwamba unapenda atahiriwe unaweza kuanza kuongea topic tofauti za mapenzi ili kuzoea na baadae ukamuomba kama anaweza kutahiriwa kwani unampenda na unapenda afanye hivyo kwani ni moja ya kampeni za kitaifa kwa wanaume kutahiriwa kwa ajili ya afya yao na kuondokana na magonjwa ( unaweza kuelezea kwa namna yako wewe ni mwanamke tumia kipaji chako au kamuulize Delilah atakusimulia alivyomuhadaa Samson hadi akatoboa siri, kama inawezekana pia muuliza Hawa (eve) alivyomshashiwishi Adam akala tunda, sembuse huyo wako, uwezo unao na unaweza jambo la msingi jipange).
Hakikisha unapoongea naye unaongea kwa upendo na ujanja kwani wanaume huwa hawapendi kupokea ushauri wa wanawake hasa topic ya sex.

Hakuna njia nyngine kama hiyo ya kukaa naye na kuongea naye kwani bado mna safari ndefu ya kufurahia mapenzi pamoja.

Hongera sana kwa kuishi miaka 20 na huyo mwanaume na Mungu akubariki sana ila nakushauri uache hako kamchezo ka kuchepuka nje kwani huko nje si salama.

Ubarikiwe