"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, October 7, 2010

Ni Mafumbo

Suala la mawasiliano ktk ndoa limeelezwa na kujadiliwa na maelfu ya vitabu vya masuala ya ndoa na mahusiano.

Hata hivyo swali bado linakuwa kwa nini ni vugumu sana kwa mke na mume kuwasiliana vizuri na kuongea na hata kuelewana?

Tatizo kubwa ni kwamba pande zote mume na mke huongea ua kupeleka ujumbe kwa namna ya mafumbo (codes) bila yeye mwenye kutoa huo ujumbe kufahamu kwamba anaongea kwa mafumbo.

Hii ina maana kwamba kile mmoja anaongea si kile mwenzake anakisikia na yule aliyesikia anaamini kile amesikia ni kile mwingine ana maanisha kitu ambacho si kweli.

MFANO

Baada ya kuamka na kujiandaa na kuwa tayari kwenda kazini sasa wakati wanavaa nguo asubuhi wawahi kazini, Jane anamwambia mume wake aitwaye James;

“Sioni nguo ya kuvaa leo”

Huku akiwa na maana kwamba hana nguo mpya kwa muda mrefu.

Siku ya pili yake james naye asubuhi anamwambia mke wake jane kwamba;

“Sioni nguo ya kuvaa”

Huku akimaanisha haoni nguo safi ya kuvaa.

Kutokana na aina hii ya mawasiliano ni wazi kwamba kunaweza kutokea mgogoro mkubwa sana kwani kama suala la “sina nguo ya kuvaa” huwa na maana tofauti kwa kila mmoja je masuala mengine?

Kumbuka kuwasiliana kati ya mke na mume ni pamoja na kufahamu tofauti zilizopo kati ya Mwanamke na Mwanaume katika kuwasiliana kwani kila gender ina namna yake.

2 comments:

Anonymous said...

Habari kaka Mbilinyi,
Hapo umetuonea akina dada wala sio kweli kwamba ukisema sioni nguo ya kuvaa leo inamaanisha unahitaji nguo mpya, hapana. Ni kwamba mtu anakuwa anamanisha kabisa kuwa haoni nguo ya kuvaa ndio kwani labda hazijanyoshwa au ni chafu lakini si kwamba anakuwa anahitaji nguo mpya.
Na kama anahitaji nguo mpya kwanini azunguke asiseme kwa mwenza wake kuwa nahitaji nguo mpya?

Ur sister

Lazarus Mbilinyi said...

Pole sana dadangu, huo ulikuwa ni mfano tu sina maana ni kweli kwamba mwanamke akisema sina nguo ya kuvaa maana yake ni kwamba hana nguo mpya. jambo la msingi ni kwamba namna mwanamke anawasiliana mara nyingi ni tofauti sana na mwanaume na ni vizuri kufahamu hivyo kwani mwanaume ni logical zaidi wakati mwanamke ni feelings kwanza na mahusiano ( anahusanisha na kuzunguka kimaongezi)

Upendo daima