"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, October 4, 2010

Ni Uamuzi wako

Ikitokea mchanga ukaingia kwenye jicho basi jicho litauma na kama halitatafutiwa ufumbuzi basi jicho linaweza kupoteza uwezo wa kuona na unaweza kuwa kipofu.

Hata hivyo huo mchanga ukiwekwa kwa kombe (oyster/shell-fish) husababisha usumbufu ambao humfanya atoe mng’ao kama wa lulu (pearly).

Suala muhimu la kujiuliza ni je, mchanga ni kisababishi cha msingi cha jicho kuuma au kwa kombe kutoa rangi nzuri za kung'aa kama lulu?

Kama mchanga ni kisababishi basi matokeo yangekuwa sawa kwa jicho na kombe.

Kilichofanyika ni kwamba mchanga umetumika kama ni wakala (agent) wa kudhihirisha tabia za ndani za jicho na Kombe.

Linapokuja suala la mahusiano hii ina maana unapoona mke wako au mume wako anafanya maisha kuwa magumu, machungu (irritable) unaweza kuamua kuwa kama mchanga kwenye jicho au mchanga kwenye kombe.

Kama hujaelewa basi nikupe mfano mwingine!

Unajua nini kitatokea kama utaweka udongo wa mfinyanzi na ice cream kwenye jua kali la mchana?

Udongo wa mfinyanzi utakuwa mgumu kama jiwe na ice cream itayeyuka na kuwa maji.

Je, hii ina maana gani?

Hii ina maana kwamba joto la jua hudhihirisha tabia za ndani za udongo wa mfinyanzi na icecream.

Inawezekana mume wako au mke wako ni mtu irritant muda wote, ni kweli hiyo haipingiki (it is given) maana yake hapo una maamuzi mawili tu

Kwanza ni kuitikia kwa busara (njia ya kimungu) na pili kuitikia kwa ujinga na kipuuzi zaidi ukawa kama mchanga na jicho au jua na udongo wa mfinyanzi nah ii kamwe si njia sahihi.

Kumbuka ni rahisi sana kulaumiana au kumlaumu sana mwenzako kwenye ndoa. Hata hivyo kupitia njia ya lawama utaishia kuwa victim na utakosa dhawabu kwa Mungu.

Jambo la msingi la kukumbuka kwamba unapoona Mume wako au mke wako anapandisha joto, anakuwa irritant, mtu wa blaming, critical; lazima ukumbuke kwamba

Kama mtu mzima mwenye uhuru kamili ndani yako na unafahamu wazi kabisa unawajibika kumjibu majibu mawili la kujenga na kubomoa, la kufurahisha na la kuudhi la amani au vita.

Jibu la kumpa Mungu utukufu au kumchukiza nk.

Kumbuka unao uamuzi wa kufanya vizuri au vibaya, kuchukia au kufurahi bila kujali mwenzio wako amefanya vibaya namna gani kwani yeye ni wakala tu wa kusaidia wewe kuonesha true colours ulizonazo.2 comments:

Ruth said...

Habari kaka Mbilinyi,
Labda mimi sikukupatavizuri, unamaanisha nini uliposema uamuzi ni wako katika kufanya nini? kuwa mchanga au kuwa icecream?sijakupata tafadhari. Ruth

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Ruth,

Kwanza hongera kwa kupita hapa na kusoma hii post.

Ni UAMUZI WAKO kujibu kwa jeuri au kwa upendo pale mpenzi wako anapoonesha tabia ya kuudhi au matendo ya kuudhi kwani maudhi yake ni wakala (agent) tu wa kuonesha wewe una busara au ujinga kiasi gani.
Mtu mwenye busara anapoona mpenzi wake amemuudhi hujibu kwa hekima na wakati mwingine yeye ndo huomba msamaha ili kujenga ndoa au mahusiano.
Mara nyingi ni rahisi sana kulaumu mpenzi wako kwa jambo hata dogo au kwa vile anakufanyia hata hivyo wewe unao uamuzi kuwa mchanga kwenye jicho (kusumbua) au mchanga kwenye Kombe (oyster) kiasi cha kutoa rangi za kuvutia kama lulu.

Kama hujaelewa basi nitarudia kwa namna nyingine tena.

Ubarikiwe