"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, November 19, 2010

Kosa Lilelile; Why?

Kuna usemi wa kingereza usemao “The more mistakes one makes in life, the smarter one gets in life” ingawa huu usemi hukubalika katika baadhi ya maeneo ya maisha, linapokuja suala la mapenzi au mahusiano huwa kitu kigumu.

Kwenye mapenzi na mahusiano makosa mengi huendelea kujirudia kila leo, wapo wanawake hujikuta kila wanapotafuta wapoenzi huangukia kwa wanaume ambao huishia kuwatesa na kuwaumiza kwa style ile ile. Na wapo wanaume ambao huangukia kwa akina dada walewale ambao huishia kutafuna pesa zao na kuishia.

Wengi tunaamini kwamba mahusiano yanapoenda vibaya yanaweza kusaidia kufungua macho ya muhusika ili siku akimpata mpenzi mpya aweze kujifunza na kutorudia kosa lilelile.

Hata hivyo imekuwa tofauti Kwenye mapenzi kwani wanaume na wanawake wenye njaa ya kupendwa hujikuta wamenasa Kwenye mtego uleule ambao waliukimbia kwa wapenzi wa zamani na kuendelea kuumizwa zaidi.

Mbaya zaidi ni pale ambapo tumeona wanandoa ambao wametoka familia zenye tatizo (wazazi kupigana, kuachana nk) nao wamejikuta wanandoa za aina hiyohiyo.

MFANO:

Jane anaelezea kwamba “John ni mwanaume smart, mwenye mafanikio na ambaye akiingia mahali popote si rahisi usishtuke kwa namna anavyovutia, anasema alikutana naye katika sherehe za ofisi yao na haikuchukua muda wakawa wapenzi hata hivyo baada ya miezi 3 alimuona John ni mwanaume mwenye wivu kupindukia na anaweza kukudhalilisha hata mbele za watu, akaamua kuachana naye.

Baada ya miezi sita akampata kijana mwingine mwenye sifa kama za John na wakapendana na kuwa wapenzi hata hivyo baada ya miezi 2 akajikuta amenasa Kwenye mtego wa mwanaume yuleyule kama John.

Swali la Jane lilikuwa kwa nini kila mara nikipenda mwanaume naangukia kwa mwanaume mwenye tatizo linalofanana, anasema anaogopa kupenda sasa.

Mwalimu Juma ameshaachana na wasichana wawili ambao wote alipoanza urafiki nao walimtegemea kwa kila kitu kifedha na alipotamka kuoana kila mmoja kwa wakati wake walimruka na kumkimbia.

Jane na mwalimu Juma si wao tu katika kujikuta wanaangukia kwa wapenzi wanaowaumiza mara zote inawezekana hata wewe unayesoma hapa yamekukuta, umejikuta upon Kwenye replay ya kosa lilelile kwa mpenzi wa zamani na sasa lipo kwa mpenzi mpya.

Watafiti wa masuala ya mahusiano wanakiri kwamba namna tumelelewa na familia ambazo zinatulea tangu watoto zina effect kubwa sana katika maisha yetu na namna tunaweza kumtafuta mwenzi wa maisha.

Kuna namna ya asili (natural Instinct) ambayo hutueleza namna ya kutafuta usalama wa kudumu kimaisha na hizi natural instinct hufanya tofauti na ufahamu wetu wa ndani hasa katika suala la mahusiano kwa kutofahamu tunatafuta kutimiza hisia zetu (emotions & feelings) kwa yale tuliona wakati tunalelewa.

Matokeo yake kama ulizaliwa familia ambayo baba na mama walikuwa wanagombana unaweza kuishia kumpata mpenzi mgomvi ambaye atakuwa anakudunda kila siku.

Je, unatakiwa kufanya nini kama unajikuta ni mtu wa kurudia kosa lilelile?

Jambo la msingi ni kufananisha sifa za mpenzi wako wa kwanza aliyekuumiza na huyu unataka kuwa naye na tafuta tofauti zake pia na orodhesha vitu ambavyo hupendi vijirudie.

Kama wewe ni Jane (Kwenye mfano) kwa nini kutafuta mwanaume kwa sababu ni smart au ana mafanikio badala ya mwanaume mwenye sifa tofauti na hizo?

Kwa nini kama wewe ni kama mwalimu Juma (Kwenye mfano hapo juu) utumie fedha kama njia ya kumvuta mwanamke akupende badala ya upendo tu bila kuonesha fedha zako au uwezo ulionao?

Kufanya jambo lilelile kwa njia ile ile si rahisi kupata matokeo tofauti.

Tumia ubongo2 comments:

Anonymous said...

Habari kaka Mbilinyi

Mimi ni yule dada Ishita kama unanikumbuka.

Ndoa yango imefika kikomo nimeamua niachie manyanga kwani mbali na mume wangu kuwa amezaa nje ya ndoa tukawa tumeyasuluisha, bado mume wangu hakutaka kubadilika na kwa vile mara nyingi huwa nasafiri huwa analeta wanawake ndani nimevumilia naona nitakuja kufa kwa ukimmwi na bado nina mtoto mchanga.

Na mpaka nimefikia hatua yakusema nabwaga manyanga imefikia hatua alitaka kunichinja na alinishikia bastola kutaka kuniua ila Mungu ni mwema siku yangu ya kufa ilikuwa haijafika, na bahati nyumbani alikuwa mdogo wake ndio aliyetuokoa na hapo nikapata mwanya mimi na mwanangu tukatoroka nikarudi kijijini ili nipumzishe mawazo. Lakini kwa sasa mwenzangu hata hashituki na isitoshe halali nyumbani.

Je! ni haki nikaomba tuachane najua kidini hairuhusu au niamue tu kukaa nae mbali maana kwa sasa namuogopa anaweza kuniua. Naomba ushauri wako. Namwacha mume wangu while bado nampenda na ndio maana niliweza kuvumilia yote ilipofika ya kutaka kuniua ndio nimeamua kuondoka. Nifanyeje kwa sasa niko kwa rafiki yangu naanza maisha upya.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Ishita,

Pole sana kwa yale unapitia na nafahamu namna inavyokuumiza na zaidi uchungu na mateso unayopitia jambo la msingi ni wewe kuwa strong na kwamba Dark days are not permanent! after dark days there are good days, jambo la msingi una afya njema na be strong, usikubali kukata tamaa hata siku moja.

Ni kweli issue za ndoa huwa ngumu sana hasa linapokuja suala la dini, ninachojua mimi ni kwamba ndoa kidini (christian) huwa haivunjwi ila unaweza kuondoka na kukaa mbali (separation) huku mkiendelea na taratibu za kuangalia ni namna gani kila mmoja anaweza kujirekebisha au yule anayemuumiza yule ambaye ni innocent anaweza namna gani kujirekebisha na wakati huohuo ukitumia washauri wa ndoa kama wachungaji, ndugu na wazazi na washauri kitaalamu kuangalia ni namna gani mume mume wako anaweza kujirekebisha pamoja na kupima afya yake kujua kama ni salama au la.
Kwa sasa uamuzi wako upo sahihi kwani ni kweli anaweza kukuua kama anaweza kuleta wanawake hadi kitandani kwako.
Pia jipe muda hata kama unampenda sana, maisha yapo jikite katika kuyaweza maisha yako vizuri na mtoto na baadae ndipo uangalie namna ambavyo mume wako amebadilika.

Pole sana na ni maombi yangu kwamba Mungu atakusaidia kukupa nguvu na ushindi kwani suala lililo mbele yako ni kubwa na linamaliza sana namna unawaza na kufanya kazi zako kila siku.

Ukipata muda unaweza kuwasiliana nami kwa 0767 0344 41 au lazarusmbilinyi@gmail.com

Mungu akusaidie