"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, December 18, 2010

Anataka Tuangalie Mkanda!

Kaka Mbilinyi habari za siku!

Nina swali ambalo naomba msaada kwani najikuta nipo njia panda na swali lenyewe ni kama ifuatavyo.

Mume wangu anataka tununue mkanda wa pornography kwa ajili ya kutusaidia kuwa na “mood” kwa ajili ya tendo la ndoa. Hata hivyo sipo comfortable na hilo pendekezo ingawa anadai kwamba kukataa kwangu ni kwa sababu nimeotoka familia ya dini sana. Sina cha kufanya kwani nampenda sana mume wangu na sipendi ajisikie vibaya na napenda kumpa heshima yake ili kudumisha ndoa yangu. Kitendo cha kuangalia picha za mwanamke mwingine na mwanaume mwingine wakifanya mapenzi wkangu naamini kitanifanya kuzimia kabisa na kukosa hamu kabisa kwani dhamira yangu inakataa.

Je, nifanyeje?

Dada Pole sana kwa kuuliza swali lako na kuwa wazi kuomba msaada kwa ajili ya swali lako ni kweli swali ulilouliza ni swali muhimu sana hasa kwa nyakati tulizonazo ambapo mambo yamekuwa tofauti kiasi kwamba kuna mambo mengi sana yapo sokoni kwania ajili ya wanandoa na mengine hujenga ndoa na mengine hubomoa ndoa na kuwa vipande vipande na hatimaye kuziua.

Kutokana na namna mwanaume na mwanamke walivyoumbwa tofauti hata linapokuja suala la pornography (picha za ngono) wanaume hujisikia tofauti na wanawake kwani wanaume wapo wired tofauti kwa kile wanachoona. Wanaume wengi huwa addicted na picha za porniography wakati wanawake wengi huwa addicted na movies za romance.

Bottom line ni kwamba mikanda ya pornography si picha tu bali wale ni watu walihisi ambao wana hisia, matumaini, matatizo, mahitaji na pia wameumbwa na Mungu tatizo ni kwamba wamejiingiza kwenye hiyo business kwa sababu ya uhitaji wa pesa na ni kitu kibaya.

Kwa mwanaume halisi, mwanaume wa ukweli, mwanaume anayejali, mwanaume rijali anayempenda mke wake lazima atamlinda na njia kamili ya kumlinda ni kuachana na kuleta mwanamke au mwanamke wa tatu badala ya mke wake.

Yule mwanamke kwenye mkanda yupo pale kwa ajili ya biashara, kila anachofanya ni kuigiza ni kitu cha kweli na zaidi hizo picha zinapitia katika editing ya hali ya juu kutokana na soko na kwamba mwanamke wa kawaida ambaye amelelewa vizuri hawezi kufanya vile Yule mwanamke anafanya kwani ni aibu na si kweli.

Kitu ambacho kitatokea ni kwamba wewe mwanamke huwezi kushinda na maigizo ya Yule mwanamke na pia hizo picha zimesafishwa kiasi ambacho wewe huwezi kuwa vile ma matokeo yake mume wako atakushangaa kwa nini pamoja na kuangalia umeshindwa kufanya kama alivyofanya Yule mwanamke kwenye mkanda na matokeo yake yeye ni kuona wewe huwezi kumpa kile anahitaji kwa kuwa tayari kichwa chake kimejaa picha za Yule mwanamke kwenye mkanda.

Dadangu kama unampenda mume wako ni pamoja na kukataa kutumia hizo picha chafu kama njia ya kuwapa mood kwa ajili ya tendo la ndoa badala yake kama hakuna mood basi pigeni magoti na kumuomba Mungu aliyewaumba awape mood natural na kulirudisha lile penzi la kweli (original) lililowavuta hadi mkaona na si kutumia picha cha ngono za watu wingine.

Dada onesha kwamba na wewe una backbone kwa ajili ya kuilinda ndoa yako, mwambie mume wako kwa upendo na wazi kabisa kwamba hutaweza kuangalia vitu kama hivyo na badala yake wewe mwenyewe uwe huru chumbani kiasi cha yeye kukuona kama ulivyo na kukufurahia badala ya hizo picha.

Pornography katika uhalisia ni Kitendo cha aibu na kitu kibaya kinachoshusha hadhi ya biandamu aliyeumbwa na Mungu kuwa tofauti na wanyama wengine na hufanya na binadamu waliopotoka kimalezi. Athari zake ni mbaya sana na huwezi kupelekea binadamu kuwa na tabia zaidi ya wanyama kama vile mapenzi kinyume na maumbile.

Ubarikiwe!

No comments: