"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, January 16, 2011

Ni Zaidi ya Urembo

Ni yule mwenye uwezo wa kujali mume na watoto na kuwatunza.
(Pichani ni Karen Lazarus)
Nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara na akina dada wengi ambao wamejikuta umri unaenda bila kuolewa pamoja na kwamba wao ni warembo na wana sura nzuri (great looks) za kuvutia kila mwanaume ambaye ana ndoto wa kumpata mwanamke wa kuoa.

Hawa wanawake warembo na beautiful one hujiuliza inakuwaje wanawake hawa wasio warembo (Wengine sura za chimpanzee) huolewa na wanaume handsome kama malaika.

Hawa wanawake hawa huamini kwamba ukiwa mwanamke mrembo na sura nzuri basi utaolewa na mwanaume mzuri au mwenye uwezo kitaaluma na kwa urembo wao hujawa na mawazo (fantasy) kujiona wapo Mbele ya madhabahu wakifunga ndoa na wanaume ma-handsome, madaktari, maprofesa, wabunge nk.

Hata hivyo wanasahau kwamba mahusiano ya ndoa ni zaidi ya urembo na sura nzuri au figure nzuri au great looks bali namna wawili wanaopendana wanavyoheshimiana na kufanana tabia na upendo wa kweli wenye kuwapa faida wote wawili na kila mmoja kumtanguliza mwenzake na si ubinafsi.

Ni kweli kwa urembo wako na sura yako nzuri unaweza kumvutia au kumvuta mwanaume hata hivyo kumvuta au kumvutia mwanaume ni suala lingine na mwanaume kubaki na wewe hadi akuone ni suala lingine.

Linapokuja suala la kuoana kimtazamo mwanaume na mwanamke hutofautiana kwani ndani ya mawazo ya mwanaume huwa kunakuwa na aina mbili za mwanamke. Aina ya kwanza ni mwanamke ambaye si wa kuoana bali kujifurahisha, rafiki, mtu wa kupeana company, kutembea naye sehemu tofauti, kuburudishana na mwanamke ambaye hata wanaume Wengine wakimuona ajisikie kweli ana mwanamke mrembo hata kama ana tabia ovyo na msumbufu.

Aina ya pili ni mwanamke ambaye mwanaume huona anafaa kuoana naye huyu ni mwanamke ambaye anamfaa (good marriage material).
Humjua tangu mapema wanapoanza urafiki kwani huanza kujenga mahusiano ambayo yanaonesha wana maisha ya pamoja baadae.
Humfahamu kama mzazi mwenzake na anafahamu fika huyu mwanamke atamtunza yeye mwanaume na watoto watakaobarikiwa kuwazaa.

Ni mwanamke mwenye mtazamo bora kuhusu maisha na familia siyo anayetaka starehe na maisha ya juu na ubinafsi.
Ni mwanamke mwenye tabia njema na si msumbufu.
Ni mwanamke mwenye mtazamo wa kimaendeleo kwa faida ya mume na watoto na si yeye binafsi.
Hivyo anaweza asiwe mrembo au akawa mrembo jambo la msingi kwa mwanaume ni kumppata mwanamke ambaye ni Good Marriage material na si urembo, sura nzuri na mwonekano mzuri tu.

Thursday, January 13, 2011

Je, akili ni Muhimu?

Genevieve Nnaji ni intelligent James ni kijana ambaye amemaliza chuo kikuu cha Tumaaini Iringa na anafanya kazi, katika pitapita zake alikutana na msichana Jane ambaye ni mrembo na kwa kumtazama tu James alijiona amepata chaguo lake, mwanamke anayetimiza ndoto zake. James kwa Jane alikuwa amefika na hakupoteza muda akamuomba kuwa mpenzi wake na mahusiano yakaanza.

Hata hivyo baada ya kudumu katika mahusiano kwa muda wa miezi miwili, James aligundua kwamba fahamu na akili ya kujua mambo na namna dunia inaenda kama vile siasa, uchumi, michezo nk. Ukiacha neno nakupenda na urembo Jane hana jipya la kuongea na James.
Jane ni mrembo na anajua kuvaa na zaidi ya hapo hajui nini kinaendelea katika ulimwengu wa sasa (modern world)

Bila kupoteza muda James aliona haina haja kuendelea na mahusiano kwani kwa namna Jane asivyokuwa na ufahamu au akili ya kujua mambo (intelligence) inaweza kuleta shida huko Mbele kwa yeye kushindwa kuwa mume bora na Jane kushindwa kuwa mke bora.

Swali ambalo ni la msingi kujiuliza je ufahamu au akili ya kujua mambo (intelligence) ni kitu muhimu sana katika mapenzi au ndoa au kwa Yule unaamua kuishi naye maisha yako yote?
Je, ili moto wa mapenzi uendelee kuwaka kati ya upendo na akili kipi muhimu?

Wapo wanaume ambao hukiri wazi kwamba si rahisi kwao kuoana na mwanamke ambaye hata hajui kile kinaendelea katika mazingira yanayomzunguka na dunia ya sasa bali uelewa na ufahamu na akili ya kujua mambo muhimu.

Wengine hujipangia kuhakikisha wale wanaoana nao ni lazima wawe na kiwango Fulani cha elimu hata hivyo wakati mwingine kiwango cha elimu ni tofauti na intelligence.

Wengine wanauliza kwamba je utajisikiaje kutumia muda wake wote wa maisha yako kuongea na mtu muhimu kwao hajui chochote hata jambo ambalo linaongelewa duniani kwa sasa, hajui facebook ni kitu gani, skyper au twitter, siasa, biashara nk.
Wengine wameenda mbali zaidi kwa kueleza kwamba sasa tunaishi katika ulimwengu ambao mapenzi ni zaidi ya hisia (feelings)

Hata hivyo dada Esha mtangazaji wa Radio moja jijini Dar es Salaam yeye anasema katika mahusiano au ndoa au mapenzi kukiwa na upendo wa kweli basi ufahamu au akili (intelligence) haina nafasi kubwa ya kuhatarisha mahusiano kwani upendo ni kila kitu na anatumia Biblia (1Wakorintho 13).

Je, wewe una mtazamo gani?