"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, January 13, 2011

Je, akili ni Muhimu?

Genevieve Nnaji ni intelligent James ni kijana ambaye amemaliza chuo kikuu cha Tumaaini Iringa na anafanya kazi, katika pitapita zake alikutana na msichana Jane ambaye ni mrembo na kwa kumtazama tu James alijiona amepata chaguo lake, mwanamke anayetimiza ndoto zake. James kwa Jane alikuwa amefika na hakupoteza muda akamuomba kuwa mpenzi wake na mahusiano yakaanza.

Hata hivyo baada ya kudumu katika mahusiano kwa muda wa miezi miwili, James aligundua kwamba fahamu na akili ya kujua mambo na namna dunia inaenda kama vile siasa, uchumi, michezo nk. Ukiacha neno nakupenda na urembo Jane hana jipya la kuongea na James.
Jane ni mrembo na anajua kuvaa na zaidi ya hapo hajui nini kinaendelea katika ulimwengu wa sasa (modern world)

Bila kupoteza muda James aliona haina haja kuendelea na mahusiano kwani kwa namna Jane asivyokuwa na ufahamu au akili ya kujua mambo (intelligence) inaweza kuleta shida huko Mbele kwa yeye kushindwa kuwa mume bora na Jane kushindwa kuwa mke bora.

Swali ambalo ni la msingi kujiuliza je ufahamu au akili ya kujua mambo (intelligence) ni kitu muhimu sana katika mapenzi au ndoa au kwa Yule unaamua kuishi naye maisha yako yote?
Je, ili moto wa mapenzi uendelee kuwaka kati ya upendo na akili kipi muhimu?

Wapo wanaume ambao hukiri wazi kwamba si rahisi kwao kuoana na mwanamke ambaye hata hajui kile kinaendelea katika mazingira yanayomzunguka na dunia ya sasa bali uelewa na ufahamu na akili ya kujua mambo muhimu.

Wengine hujipangia kuhakikisha wale wanaoana nao ni lazima wawe na kiwango Fulani cha elimu hata hivyo wakati mwingine kiwango cha elimu ni tofauti na intelligence.

Wengine wanauliza kwamba je utajisikiaje kutumia muda wake wote wa maisha yako kuongea na mtu muhimu kwao hajui chochote hata jambo ambalo linaongelewa duniani kwa sasa, hajui facebook ni kitu gani, skyper au twitter, siasa, biashara nk.
Wengine wameenda mbali zaidi kwa kueleza kwamba sasa tunaishi katika ulimwengu ambao mapenzi ni zaidi ya hisia (feelings)

Hata hivyo dada Esha mtangazaji wa Radio moja jijini Dar es Salaam yeye anasema katika mahusiano au ndoa au mapenzi kukiwa na upendo wa kweli basi ufahamu au akili (intelligence) haina nafasi kubwa ya kuhatarisha mahusiano kwani upendo ni kila kitu na anatumia Biblia (1Wakorintho 13).

Je, wewe una mtazamo gani?

4 comments:

Anonymous said...

Hello!

Habari ya siku nyingi kaka na heri ya mwaka mpya jamani!

Yaani mada nzuri sana,
Mimi niko tofauti kdg naona hata uelewa pia unahitajika ktk swala la ndoa kwa ujumla coz kuna muda kama mke lazma amshauri mume na awe na mifano mbalimbali ili mume ashawishike kwa namna moja au nyingine unajua kaka unaweza ukawa na wazo zuri lakini mwenzio kumbe kwake ni upuuzi tu sasa bila kuwa na mfano hatokuelewa hata uwe na PhD ni bure ndio inahitaji ubunifu na akili pia ya ushawishi kwani hata mwanaume anapotongoza anatumia akili hakurupuki na hasa kama anajua kuwa huyu anafaa kuwa mke lazma akili inahitajika hapo.

NOTE:

WATU WANAENDA SHULE KUONDOA UJINGA LAKINI UPUMBAVU UNAKUWA PALEPALE TU. NI WEWE MWENYEWE JINSI YA KUUONDOA.


Mama P!

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P.
Mimi ni mzima wa afya njema. U busy tu dadangu.
Asante kwa comments zako.

Upendo daima

Anonymous said...

Habari kaka
Kweli umenigusa na sina cha kusema coz yalishanitokea

Elibaric

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Elibaric,

Ni kweli haya mambo yako na yanatokea na jambo la msingi ni upendo na kuchukuliana kwani hakuna binadamu aliyesahihi kila eneo la maisha yake.

Pia wakati unafunga ndoa ulikubali kumchukua kama alivyo ingawa inawezekana alionesha yupo smart na anaweza kwenda na wewe popote na zaidi akatimiza ndoto zako pamoja na mbele ya safari unakuta mambo sivyo.

Upendo daima