"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, January 16, 2011

Ni Zaidi ya Urembo

Ni yule mwenye uwezo wa kujali mume na watoto na kuwatunza.
(Pichani ni Karen Lazarus)
Nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara na akina dada wengi ambao wamejikuta umri unaenda bila kuolewa pamoja na kwamba wao ni warembo na wana sura nzuri (great looks) za kuvutia kila mwanaume ambaye ana ndoto wa kumpata mwanamke wa kuoa.

Hawa wanawake warembo na beautiful one hujiuliza inakuwaje wanawake hawa wasio warembo (Wengine sura za chimpanzee) huolewa na wanaume handsome kama malaika.

Hawa wanawake hawa huamini kwamba ukiwa mwanamke mrembo na sura nzuri basi utaolewa na mwanaume mzuri au mwenye uwezo kitaaluma na kwa urembo wao hujawa na mawazo (fantasy) kujiona wapo Mbele ya madhabahu wakifunga ndoa na wanaume ma-handsome, madaktari, maprofesa, wabunge nk.

Hata hivyo wanasahau kwamba mahusiano ya ndoa ni zaidi ya urembo na sura nzuri au figure nzuri au great looks bali namna wawili wanaopendana wanavyoheshimiana na kufanana tabia na upendo wa kweli wenye kuwapa faida wote wawili na kila mmoja kumtanguliza mwenzake na si ubinafsi.

Ni kweli kwa urembo wako na sura yako nzuri unaweza kumvutia au kumvuta mwanaume hata hivyo kumvuta au kumvutia mwanaume ni suala lingine na mwanaume kubaki na wewe hadi akuone ni suala lingine.

Linapokuja suala la kuoana kimtazamo mwanaume na mwanamke hutofautiana kwani ndani ya mawazo ya mwanaume huwa kunakuwa na aina mbili za mwanamke. Aina ya kwanza ni mwanamke ambaye si wa kuoana bali kujifurahisha, rafiki, mtu wa kupeana company, kutembea naye sehemu tofauti, kuburudishana na mwanamke ambaye hata wanaume Wengine wakimuona ajisikie kweli ana mwanamke mrembo hata kama ana tabia ovyo na msumbufu.

Aina ya pili ni mwanamke ambaye mwanaume huona anafaa kuoana naye huyu ni mwanamke ambaye anamfaa (good marriage material).
Humjua tangu mapema wanapoanza urafiki kwani huanza kujenga mahusiano ambayo yanaonesha wana maisha ya pamoja baadae.
Humfahamu kama mzazi mwenzake na anafahamu fika huyu mwanamke atamtunza yeye mwanaume na watoto watakaobarikiwa kuwazaa.

Ni mwanamke mwenye mtazamo bora kuhusu maisha na familia siyo anayetaka starehe na maisha ya juu na ubinafsi.
Ni mwanamke mwenye tabia njema na si msumbufu.
Ni mwanamke mwenye mtazamo wa kimaendeleo kwa faida ya mume na watoto na si yeye binafsi.
Hivyo anaweza asiwe mrembo au akawa mrembo jambo la msingi kwa mwanaume ni kumppata mwanamke ambaye ni Good Marriage material na si urembo, sura nzuri na mwonekano mzuri tu.

No comments: