"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, May 28, 2011

SIRI ZINGINE MMH!Kuwa mkweli na muwazi ni moja ya misingi ya kujenga mahusiano yanayodumu na hata kukabiliana na dhoruba mbalimbali za maisha ya mahusiano ya ndoa.

Swali kubwa ambao wengi hujiuliza, wanaume kwa wanawake hasa wale ambao wanaingia kwa mara ya kwanza katika mahusiano ya uchumba na hatimaye ndoa ni swali lifuatalo.

Je, nikieleza ukweli wote wa maisha yangu ya nyuma haiwezi kuathiri mahusiano na kupelekea mwenzangu kufikia hatua ya kuachana nami?

Inawezekana huko nyuma ulidhalilishwa (kubakwa nk) au uliwahi kutoa mimba nk. Je, kumueleza mpenzi wako jambo kama hilo haliwezi kupelekea yeye kukuacha hata kabla ya kuoana au unaweza kumueleza baada ya kuoana kwamba mwenzio nilibakwa au niliwahi kutoa mimba nk?
Je, kuna umuhimu wa kutunza au kusema ukweli mapema kabla ya mahusiano kufika mbali?

James alipooana na Jane, Jane hakumueleza kabisa terrible secret aliyokuwa nayo ingawa tangu siku ya kwanza walipogundua wanawaweza kuoana alikubaliana kwamba ni muhimu kila mmoja kueleza ukweli na kuwa wazi kusema ukweli na ukweli (trust/honest) kuwa ndiyo msingi wa mahusiano yao.

James na Jane walifahamiana tangu walipokuwa shule ya msingi ingawa baadae kila mmoja alienda shule tofauti tofauti ya sekondari na chuo hadi walipokutana na kuamua kuoana.

Baada ya kumaliza sekondari Jane alipoata mimba na akaamua kuitoa ili kwenda chuo na James hakuwa anajua hilo kwa kuwa aliyempa mimba alikuwa mwanaume mwingine.

Baada ya kuoana waliishi kwa furaha, amani na upendo wa hali ya juu hata hivyo furaha hiyo ya ndoa ilikuwa inazimika kila pale Jane anapofikiria namna alitoa mimba (abortion) na hata alipokuwa anawaza namna ya kuanza familia alikuwa anajisikia hatia na kujiona hastahili kwani alishajihusisha na kosa la mauaji ya motto asiye na hatia tumboni mwake.
Baada ya kukaa kwa muda mrefu na hiyo siri inayomuumiza ilifika siku akawaza na kuamini kwamba akimwambia James hiyo siri basi James atamsikiliza na kuendelea kumpenda kwani atakuwa amesema ukweli.

Siku moja James na Jane walitembelea wazazi wa Jane huko Korogwe Tanga, wakiwa chumbani wawili tu, Jane akaamua kutoboa hiyo siri inayoutesa moyo wake kwa kumwambia James kwamba
“KUNA KITU NILIKUWA SIJAWAHI KUKWAMBIA NACHO NI KWAMBA NILITOA MIMBA BAADA YA KUMALIZA SEKONDARI NA NILIFANYA HIVYO ILI NIWEZE KWENDA CHUO”

James hakuamini kile Jane ameongea amesema, kwani alimfahamu Jane tangu watoto na wakasoma shule moja ya msingi na zaidi Jane alikuwa ni mwanamke ambaye huwezi kuamini kwamba aliweza kupata mimba na zaidi kupata wazo la kuitoa hasa kutokana na malezi ya familia yao na maisha yake kwa ujumla.
Kilichomuumiza zaidi James ni kile kitendo cha Jane kwenda kutoboa siri yake siku ambayo wanakuwa kwa wazazi kwake, James alitafsiri kwamba Jane aliamua kutoa siri akiwa kwa wazazi wake ili hata kama baada ya kutoa hiyo siri James akaamua kuachana naye yeye Jane atakuwa huyo nyumbani kwa wazazi wake hivyo amepata sehemu ya kuishi baada ya kukurusha bomu lake.

Hata hivyo baada ya Jane kuiweka wazi hiyo siri mahusiano na mume wake yalibadilika na yakaingia kwenye wakati mbaya kuliko nyakati zote na kilichomuumiza James ni kwa nini Jane alificha hiyo siri hadi baada ya kuaoan kwanza na si kabla ya kuoana.
Kama Jane ameweza kutunza siri kubwa kama hiyo kwa huo muda je, anaweza kuaminiwa maeneo mengine ya maisha yake?

Pia tukumbuke kwamba binadamu si Mungu kwamba unapokiri dhambi zako basi anakusamehe na kusahau.
James hakusahau na alijiona ni mwanaume ambaye hafai duniani kwamba aliyemwambini duniani alificha siri kubwa.

“Huwezi kurusha kombora zito kama hilo na ukategemea mambo yataenda kama kawaida kuna kulipa gharama (price)

Sasa ndoa ilibadilika, kila ukitokea mgogoro au kutoelewa kokote sila ya James ilikuwa ni abortion ambayo Jane alifanya.

Ilifika mahali Jane alijiona ilikuwa afadhari kubaki na siri yake moyoni kuliko kukaa nayo kwa muda mrefu halafu unakuja kuitoa kwani ilikuwa ni kama amemkabidhi James silaha (magic bullet) ambayo James aliendelea kuitimia maisha yao yote ya ndoa yao.

Sasa kila alichokuwa anafanya Jane katika ndoa yao kilikuwa hakitoshi kwa kuwa ni msaliti, mficha siri na mnafiki……….

Je, ungekuwa wewe ni Jane ukifanya nini na hiyo siri?

Wednesday, May 11, 2011

USITANIE NI KUWA MBUNIFU!

Watu wawili wanaopendana na kuishi kila mmoja kivyake ni tofauti sana na watu wanaopendana na kuishi nyumba moja.
Wapo ambao hujiuliza inakuwaje wapenzi wawili waliokuwa wanapendana na kuwa na moto wa mapenzi wa kiwango cha juu sana wakianza kuishi pamoja mambo huanza kubadilika? Pia wapo ambao hukubaliana kwamba baada ya kuoana na kuishi pamoja watajitahidi sana kuhakikisha wanapendana kama mwanzo hata hivyo baada ya kuanza kuishi pamoja hujikuta wamekuwa dada na kaka na hakuna moto wa mapenzi tena.

Jambo la msingi unatakiwa uwe makini kwani kuishi kila mpenzi kwake ni tofauti na kuishi na mpenzi nyumba moja na kitanda kimoja.
Pia wapo wanaume au wanawake baada ya kuoa au kuolewa hufikiria na kuamini kwamba wale wameoana nao si wazuri kama wale walioko nje hata hivyo ukweli ni kwamba kwa kuwa huishi naye masaa 24 kwa siku Ndiyo maana unaona ni mzuri, ukiishi naye kwa saa 24 siku 365 kwa mwaka ndo utajua ni tofauti kabisa.

Inawezekana wakati mnaishi tofauti na mpenzi wako ilikuwa ni kulala saa sita au nane usiku kwani mlikuwa mnapigiana simu na kutumiana sms kiasi ambacho hamkulala hata hivyo baada ya kuoana sasa kila mmoja anakuwa sehemu ya maisha ya mwenzake kila siku inayipita duniani.

Sasa unalala naye, unaamka naye na kula chakula naye. Mnamiliki sebule moja, chumba cha kulala kimoja na kitanda kimoja, frji moja nk. Unajifunza tabia zake kwa undanim, unajifunza nini anapenda na nini anachukia, unajifunza udhaifu wake na uimara wake unajua nini anapenda kwenye TV na zidi rafiki zake watakuja kwenu upende usipende na kufanya au kuongea mambo yao.
Simu za rafiki zake zitapigwa kwenu, utakuwa domesticated man au domesticated woman.

Unapoishi na mtu mwingine taratibu hubadilika, masuala ya sex yatabadilika kwani utalazimika kufahamu hisia zake kimapenzi (feelings/emotions) mahitaji na kile anapenda siku zote na wewe kuwa mbunifu maana unaye kila siku.

Pia unatakiwa kuripoti kila siku kama utachelewa kurudi nyumbani utalazimika kumwambia mapema. Lazima utambue kwamba sasa utakuwa na mtu ambaye ana hofu na wewe kuchelewa au kutokupata habari zako ndani ya saa 6 mchana na huruhusiwi kwenda kimya hadi sita usiku bila yeye kujua upo wapi na kama ni salama.

Pia kuishi pamoja ni kujifunza kuwa kitu kimoja (coexist) na usiopokuwa makini unaweza kujikuta excitement zote za nyuma zinaisha na maisha yanakuwa tofauti na yale kabla ya kuishi pamoja.
Unahitaji kuwa mmbunifu wa namna ya kufanya kila siku inayokuja duniani inawapo mambo mazuri yanayofanya kila mmoja kuwa excited na mwenzake la sivyo badala ya kuishi kama wapenzi mtaishi kama dada na kaka wanaolala pamoja na ambao moto wa mapenzi umezima.

Friday, May 6, 2011

Usicheze!

Kawaida huwezi kumpa kila mwanaume treatment za mume wakati bado ni mchumba tu.
Vijana wengi leo wanapochumbiana au kutafuta urafiki wa kawaida katika ya kaka na dada (dating) wengi hawajajua kwamba hiyo ni hatua ya mwanzo kabisa na ni kama usaili tu wa kumpata mtu wa kuoana naye.
Ndoa na uchumba (girlfriend/boyfriend) ni vitu viwili tofauti kabisa uchumba huhusisha kumfahamu mwenzako kama anafaa kuwa mke au mume na ndoa ni agano na kumkubali mtu kuishi naye “No matter what” hadi kifo.

Hata siku moja uchumba si ndoa na ndoa si uchumba.

Ukimpa mchumba haki za mume au mke siku mkiachana na huo uchumba (kitu ambacho ni kawaida kama ukiona candidate uliyaye katika uchumba hawezi kwa excellent material ya ndoa) utaumizwa zaidi hasa mwanamke kwani mwanaume anaweza kumpata binti mwingine jioni yake au usiku huohuo na akaendelea na maisha.

Kinachoshangaza pia ni kwamba hata relationship inapovunjika mara nyingi mwanaume huumia kidogo kwa kuwa mwanaume siku zote anapoingia kwenye mapenzi huingia na “open mind”, wakati mwanamke akimpata mwanaume (uchumba) anajiona amampata “the Special one”.

Utasikia akina dada wengi wanasema “Nipo kwenye committed relationship” wakati ni ugirlfriend na uboyfriend tu, ni kweli uposahihi hata hivyo unatakiwa kuacha nafasi kwa ajli ya kuchunguza na si kumfanya huyo mwanaume ni mume wako na kumpa haki zote au services zote kiasi kwamba mahusiano yakivunjika unaanza kusaga meno.

Si busara kumpa mwanaume kila kitu katika mahusiano ya uchumba wakati hujaoana naye. Unamfulia nguo, unalala kwake, unampikia chakula wakati yeye ni boyfriend tu!

Swali ambalo mwanaume anajiuliza ni kwa nini aingie gharama za kukuoa kama umeshakuwa mke hata bila ring kwenye kidole?

Kwa nini akuoe wakati tayari ameshajua kila kitu kuhusu wewe?

Kwa nini anunue ng’ombe kama maziwa na nyama vyote anapata bure?

Kumbuka wazazi wetu walikuwa makini sana na hayo na mwanamke yeyeyote hakujifanya mke wakati ni mchumba tu. Uchumba ni daraja tu la kupita kufikia ndoa. Huwezi kugawa zawadi zote ambazo zipo kwenye begi kabla ya kufika kwa mwenyeji wako katika safari ya kuelekea kwenye ndoa.

Wanaume ni binadamu si Mungu na kila binadamu ana sifa ya kugeuka nyuma pale anapoona njia anayoenda si yenyewe.

Uwe na lengo lakuhakikisha unaweza kuweka mipaka na usimfanye huyo mwanaume ndo kila kitu hata duniani kwani kuna siku anaweza kubadili uamuzi ndipo kujuta kutakuja.
Ni busara kwa wewe mwanamke hata kama una mchumba uendelee kujihusisha na kazi yako, taaluma yako kiasi kwamba hata ikitokea amekuacha huwezi kuchanganyikiwa.

Kama umewekeza kwa mchumba upendo na mapenzi ya asilimia 100 Je, baada ya kuoana utawekeza kiaasi gain?

Usijifanye mke wakati ni mchumba.

“Don’t play wife if you are nothing, but mere girlfriend”

Thursday, May 5, 2011

Uwe Boss kazini, Mke mwema Nyumbani

Wakati dunia nzima inaungana kuhakikisha mwanamke anapata haki zote na kupewa kipau mbele katika masuala ya msingi ya maendeleo wapo wanawake wachache ambao huchanganya mambo kwenye ndoa zao.

Ni dhahiri na ni ukweli kwamba wanawake leo katika dunia ya tatu sasa wana elimu, wana kazi zao, na fedha zao na taaluma kitu ambacho ni kizuri na jambo la msingi sana kwa familia yoyote kuwa na mke na mume ambao wote wanachangia pato la familia.

Hata hivyo kwa upande mwingine suala la mahusiano baada ya mke na mume wote kufanya kazi na kuwa na taaluma yake data zinaonesha suala la mahusiano katika ndoa linazidi kuwa gumu na linapelekea ndoa nyingi kwenye ICU au kufa kabisa.

Ni kama vile kutatua tatizo la wanawake kupewa uwezo na haki zao kumetengeneza tatizo jipya kabisa la mahusiano kwa maana kwamba baadhi ya wanawake (siyo wote) anataka akiwa boss kazini basi akirudi nyumbani anataka awe boss pia.

Ndiyo maana baadhi ya wanaume ambao hawajiamini bado hupendelea kuoa mwanamke ambaye elimu yake au kipato chake ni kidogo kuliko wao na huwa wanaamini kwamba wanawake wenye fedha na elimu hupendelea kukalia wanaume zao.

Ukichunguza kwa undani sababu za baadhi ya wanawake ambao wana uwezo kitaaluma na kifedha kuliko waume zao, mwanaume kukaliwa ni suala la mtazamo (attitude). Kwa kuwa kazini ni boss na ana mshahara mkubwa na elimu kubwa kumzidi mume basi huyo mwanamke huamini na nyumbani anatakiwa kuwa juu ya mumewe.

Wanaume hukiri kwamba zamani wanawake walidumu katika ndoa kwa sababu walimtegemea mume kwa kila kitu na baada ya sasa kupewa uwezo wanawake wanabadilika.

Nina elimu, taaluma na fedha, kwa nini mwanaume anibabaishe”, wapo wanawake wanaoamini hivyo. Ndiyo maana kuachana na idadi ya single moms inaongezeka kila kukicha na inaonekana ni kitu cha kawaida.

Hata hivyo kutokana na tamaduni zetu za kiafrika haijalishi mwanamke una kazi nzuri kiasi gain au fedha nyingi kiasi gain unaotakiwa kumtii na kumpa mume respect anayostahili ili mahusiano yadumu.
Mumeo ni mumeo na nyumba haiwezi kuwa na wanaume wawili.

Uwe boss kazini na uwe mke mwema nyumbani!

Wednesday, May 4, 2011

Love is a flower which turns into fruit of Marriage
Finnish Proverb