"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, May 11, 2011

USITANIE NI KUWA MBUNIFU!

Watu wawili wanaopendana na kuishi kila mmoja kivyake ni tofauti sana na watu wanaopendana na kuishi nyumba moja.
Wapo ambao hujiuliza inakuwaje wapenzi wawili waliokuwa wanapendana na kuwa na moto wa mapenzi wa kiwango cha juu sana wakianza kuishi pamoja mambo huanza kubadilika? Pia wapo ambao hukubaliana kwamba baada ya kuoana na kuishi pamoja watajitahidi sana kuhakikisha wanapendana kama mwanzo hata hivyo baada ya kuanza kuishi pamoja hujikuta wamekuwa dada na kaka na hakuna moto wa mapenzi tena.

Jambo la msingi unatakiwa uwe makini kwani kuishi kila mpenzi kwake ni tofauti na kuishi na mpenzi nyumba moja na kitanda kimoja.
Pia wapo wanaume au wanawake baada ya kuoa au kuolewa hufikiria na kuamini kwamba wale wameoana nao si wazuri kama wale walioko nje hata hivyo ukweli ni kwamba kwa kuwa huishi naye masaa 24 kwa siku Ndiyo maana unaona ni mzuri, ukiishi naye kwa saa 24 siku 365 kwa mwaka ndo utajua ni tofauti kabisa.

Inawezekana wakati mnaishi tofauti na mpenzi wako ilikuwa ni kulala saa sita au nane usiku kwani mlikuwa mnapigiana simu na kutumiana sms kiasi ambacho hamkulala hata hivyo baada ya kuoana sasa kila mmoja anakuwa sehemu ya maisha ya mwenzake kila siku inayipita duniani.

Sasa unalala naye, unaamka naye na kula chakula naye. Mnamiliki sebule moja, chumba cha kulala kimoja na kitanda kimoja, frji moja nk. Unajifunza tabia zake kwa undanim, unajifunza nini anapenda na nini anachukia, unajifunza udhaifu wake na uimara wake unajua nini anapenda kwenye TV na zidi rafiki zake watakuja kwenu upende usipende na kufanya au kuongea mambo yao.
Simu za rafiki zake zitapigwa kwenu, utakuwa domesticated man au domesticated woman.

Unapoishi na mtu mwingine taratibu hubadilika, masuala ya sex yatabadilika kwani utalazimika kufahamu hisia zake kimapenzi (feelings/emotions) mahitaji na kile anapenda siku zote na wewe kuwa mbunifu maana unaye kila siku.

Pia unatakiwa kuripoti kila siku kama utachelewa kurudi nyumbani utalazimika kumwambia mapema. Lazima utambue kwamba sasa utakuwa na mtu ambaye ana hofu na wewe kuchelewa au kutokupata habari zako ndani ya saa 6 mchana na huruhusiwi kwenda kimya hadi sita usiku bila yeye kujua upo wapi na kama ni salama.

Pia kuishi pamoja ni kujifunza kuwa kitu kimoja (coexist) na usiopokuwa makini unaweza kujikuta excitement zote za nyuma zinaisha na maisha yanakuwa tofauti na yale kabla ya kuishi pamoja.
Unahitaji kuwa mmbunifu wa namna ya kufanya kila siku inayokuja duniani inawapo mambo mazuri yanayofanya kila mmoja kuwa excited na mwenzake la sivyo badala ya kuishi kama wapenzi mtaishi kama dada na kaka wanaolala pamoja na ambao moto wa mapenzi umezima.

2 comments:

Anonymous said...

Tueleze basi kuhusu Schwarzenegger. Aliyekua Govenor wa Califonia, jimbo moja huko mrekani aliyekua amemuona kutoka the Kennedy family kwa miaka 25. Alikua naishi kwa kujifanya anampenda mkewe kumbe miaka kumi alikua anatembea na mfanyakazi wa nyumba na sasa leo amekubali kuwa huyo mtoto wa huyo mfanyakazi ni wake. Mtoto huyo ana miaka 10 sasa hivi na mfanyakazi huyo amefanya kazi hapo kwao kwa miaka 10. Kwa mda wote huo alikua anadanganya ulimwengu kuwa anampenda sana mkewe, mbele ya watu kumbe ikizimwa taa sio hivyo..Ni vigumu sana kuamini wanaume na sana sana wanachosema kwa vile kila siku tunaona tu mambo mengi.

Na mimi najiuliza shukuru Mungu yuko kwenye nchi ambayo maambukizo ya ukimwi ni kidogo. Je angekua kwenye nchi kama yetu, huyo mfanyakazi tutajua analala na nani baada ya huyo kiboss chake? Na huyo boss si angempeleka magonjwa mama wa watu?

Inaumiza sana na ndio maana kila siku watu tunaokwenda shule na kusoma na kutafuta masiha. Mwishowe tunasema tutafute mtu wa kuenjoy naye lakini kutkana na haya mambo kila siku mtu unajiuliza ninachotafuta kutoka kwa mwanaume ni mapenzi tu. Kama ni kujitunza mimi na kusaidia ndugu zangu ninao na wala sitategemea mtu yeyote sasa je is it worth kuolewa kweli? Men are like chameleons na wanafurahishw ana fantasy. Ikiisha honeymoon basi wao wanaona waanze kusakanya mtu mwingine. Wanaenjoy zile feelings za kuwa na secret lover au feelings za kuogopa kushikwa. Kile ambacho ni love na cha kwako hawaenjoy...

Lazarus Mbilinyi said...

Dadangu,

Asante kwa comments zako na umeeleza mambo ya msingi sana na kwa uchungu sana kiasi kwamba ni kweli wanaume ni viumbe wa ajabu ingawa si wanaume wote na ni kweli wanaume wazuri na waaminifu bado wapo. Pia kuna wanawake hatari sana leo na hii haina maana wanawake waaminifu hawapo.

Jambo la msingi kufahamu kwamba tunaishi nyakati tofauti na kwamba maisha ya mahusiano yanahitaji sacrifice kubwa na tofauti na ikiwezekana kujikana mwenyewe kwamba naoana na mtu ambaye ni Mungu tu ndiye atanisaidia.

Pia mwenyewe bado najiuliza kulikoni na huyu gavana kwani kwa style ya ndoa za kizungu kuweza kuficha siri kubwa kama hiyo kwa miaka 10 bila mke kujua na kwa mtu maarufu kama yeye hapo kweli gavana katengeneze movie nyingine ambayo dunia nzima tunajuliza.

Upendo daima