"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, May 5, 2011

Uwe Boss kazini, Mke mwema Nyumbani

Wakati dunia nzima inaungana kuhakikisha mwanamke anapata haki zote na kupewa kipau mbele katika masuala ya msingi ya maendeleo wapo wanawake wachache ambao huchanganya mambo kwenye ndoa zao.

Ni dhahiri na ni ukweli kwamba wanawake leo katika dunia ya tatu sasa wana elimu, wana kazi zao, na fedha zao na taaluma kitu ambacho ni kizuri na jambo la msingi sana kwa familia yoyote kuwa na mke na mume ambao wote wanachangia pato la familia.

Hata hivyo kwa upande mwingine suala la mahusiano baada ya mke na mume wote kufanya kazi na kuwa na taaluma yake data zinaonesha suala la mahusiano katika ndoa linazidi kuwa gumu na linapelekea ndoa nyingi kwenye ICU au kufa kabisa.

Ni kama vile kutatua tatizo la wanawake kupewa uwezo na haki zao kumetengeneza tatizo jipya kabisa la mahusiano kwa maana kwamba baadhi ya wanawake (siyo wote) anataka akiwa boss kazini basi akirudi nyumbani anataka awe boss pia.

Ndiyo maana baadhi ya wanaume ambao hawajiamini bado hupendelea kuoa mwanamke ambaye elimu yake au kipato chake ni kidogo kuliko wao na huwa wanaamini kwamba wanawake wenye fedha na elimu hupendelea kukalia wanaume zao.

Ukichunguza kwa undani sababu za baadhi ya wanawake ambao wana uwezo kitaaluma na kifedha kuliko waume zao, mwanaume kukaliwa ni suala la mtazamo (attitude). Kwa kuwa kazini ni boss na ana mshahara mkubwa na elimu kubwa kumzidi mume basi huyo mwanamke huamini na nyumbani anatakiwa kuwa juu ya mumewe.

Wanaume hukiri kwamba zamani wanawake walidumu katika ndoa kwa sababu walimtegemea mume kwa kila kitu na baada ya sasa kupewa uwezo wanawake wanabadilika.

Nina elimu, taaluma na fedha, kwa nini mwanaume anibabaishe”, wapo wanawake wanaoamini hivyo. Ndiyo maana kuachana na idadi ya single moms inaongezeka kila kukicha na inaonekana ni kitu cha kawaida.

Hata hivyo kutokana na tamaduni zetu za kiafrika haijalishi mwanamke una kazi nzuri kiasi gain au fedha nyingi kiasi gain unaotakiwa kumtii na kumpa mume respect anayostahili ili mahusiano yadumu.
Mumeo ni mumeo na nyumba haiwezi kuwa na wanaume wawili.

Uwe boss kazini na uwe mke mwema nyumbani!

2 comments:

Anonymous said...

Shaloom,

Mimi nafikiri, huwa si wanawake wote wako hivyo na pia mwanamme huwa by nature anaanza kufikiria hivyo. mimi nina mfano halisi kwa wangu nashuka sana hata kuongea waweza kuwa makini sana isije ikaonekana ni we uko juu lakini mume mwenyewe anajisikia tayari inferior, kiasi ambacho siwezi kufanya maamuzi yeyote yale nakaa kimya tu nikiongea anasema kwa sabau umetoa hela ndio unaongea. wakati mwingine najitahidi hata kama kwenda kununua vitu nampa atm card namwambia chukua pesa twende tukanunue vitu, na akifanya hivyo bado naona hajisikii vizuri, mi naamua kutokufanya chochote ila namshauri tu. na ukimshauri kitu kizuri anasema kwa sababu una pesa unataka nipitishe ushauri wako basi nimesema hakuna. hapo huwa sishindani naye kabisa. akipiga simu mtu akinipa ujumbe wake nikimpa nakuja juu kwa nini akupe wewe ujumbe basi tabu tupu na mimi utanisaidiaje?

Lazarus Mbilinyi said...

Dadangu,
Kwanza hongera sana kwa hekima na busara ambazo umejaliwa kwamba unafahamu namna unatakiwa kuwa makini na kuishi na mwanaume ambaye hajiamini (high insecurity) na ni kweli ni kazi sana kwani lolote unalofanya kwake ni kwa sababu una uwezo au fedha.

Jambo la msingi ni wewe kuendelea kumpa heshima yake kwa kila jambo unafanya na jambo ambalo naweza kukusaidia ilikuwa ni kuongea na mumeo kumsaidia namna anaweza kujiamini na kufurahia kuwa na mwanamke ambaye anaweza na anamawazo mazuri ya kimaendeleo na maisha kwa ujumla.

Pia ni vizuri kuhudhuria semina na mikutano au masomo yoyote ambao anaweza kujifunza namna ya kujiamini na zaidi kukuamini mke wewe mke wake ambaye naamini kwa upande wangu wewe ni mwanamke wa tofauti sana na naamini kujifunza kukua katika ndoa au maeneo yoyote ya maisha ni muhimu sana na kwamba baada ya kuoana ndo mwanzo wa kila mmoja kuangalia eneo ambalo ni dhaifu na kuendelea kujifunza na kukua na kuwa mtu bora na excellent marriage material.

Ubarikiwe dadangu.

Upendo daima