"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 29, 2011

Yeye Kwanza

Mitazamo ni suala muhimu sana inapokuja issue ya kumfanya mume wako ajisikie raha na wewe chumbani.

Kuna tofauti kubwa sana na pana sana kati ya mwanaume na mwanamke na tofauti kubwa hujiweka wazi katika suala la mapenzi.

Namna ya kuwasiliana kimapenzi (love/affection) kwa mwanaume na mwanamke kuna tofauti kubwa.

Kawaida mwanamke huweza kujisikia kusisimka kwa maongezi (kile anasikia), wakati mwanaume ni mwili (kile anaona).

Pia ili mwanamke ajisikie vizuri kimapenzi katika mwili wako hupenda kujiona au jisikia yupo connected kwanza na mume wako wakati huohuo ili mwanaume ajisikie ajisikia connected ni pale tu atakapojisikia raha kimwili kwanza.

Hii ina maana kwamba mwanamke anayehitaji kumfurahisha mume wako kimapenzi atatakiwa kufahamu mapema kwamba ili kujisikia connected na mume wako anatahitaji kujiweka wazi kimwili ili mume awe rahisi kuwa connected kwake hata kama kanuni inagoma.

Lengo si kwako mwanamke kumkwepa mumeo bali wewe kujitoa kwake na hii itafanya mume wako ajisikie raha zaidi na kwenda extra mile kwa kile kila eneo la maisha yenu na kwamba anakuhitaji kila wakati wewe tu.

Mwanamke hujisikia kusisimka pale mume wake akimnong’oneza maneno matamu sikioni mwake na wakati huohuo mwanaume hujisikia msisimko wa ajabu pale mke wake anapompapasa mwilini mwake kwa ngozi yake laini na kujikuta Mr. Happy wake anaanza kutoa maamuzi ambayo hajatumwa afanye.

Je ni kweli mwanaume ana sehemu kiungo kimoja tu cha kumsisimua kimapenzi?

Si kweli kwani kama mwanamke na mwanaume ana sehemu na ana utajiri mwingi wa sehemu ambazo mwanamke akimgusa basi anaweza kujisikia raha kwa mguso anaoupata.

Hata hivyo kila mwanaume ni tofauti na ana namna ya kumsisimua kimapenzi na anayejua ni yeye kwa wewe mwanamke kuwa mvumbuzi kwa kumuuliza na ujanja wako.

Tutaendelea……………….

Thursday, June 16, 2011

Wako ni wa aina gani?


Mara nyingi kuna usemi kwamba kwa mwanaume kawaida ana kitu kimoja tu ambacho kinaweza kumfanya apate hamu ya kufanya mapenzi nacho ni “kitu chochote”.
Najua hujanielewa ila Ukweli ni kwamba mwanaume ni tofauti sana na mwanamke linapokuja suala la kusisimka kimapenzi kwani mwanaume anaweza kusisimka (stimulated) hata pale tu mwanamke au mke wake akiwa nusu uchi, au uchi au hata kile kitendo cha kuvua nguo au akiwa amevaa kivazi chochote kinachoshawishi, wanawake hawapo hivyo.
Wanawake kila mmoja ni tofauti hata huyo mmoja (mke wako) yupo tofauti kila siku katika mwezi mmoja, mwaka na miaka.
Mwanaume unahitaji kuwa mbunifu kufahamu namna upepo wa hamu ya mapenzi unavyovuma kwa mke wako, kwani ukilemaa unaweza kuchanganya mambo na kupitwa na wakati.
Unahitaji kujifunza nini kinaweza au kwa sasa kunamsisimua mke wako kuwa tayari kukupa nafasi ya kufurahia tendo la ndoa.
Inawezekana mkeo ni aina ya wanawake ambao husisimka na kuwa tayari kimapenzi kwa kuguswa, kumbatiwa, shikwashikwa (caresses) yaani TOUCH GIRL!
Au Inawezekana mke wako ni aina ya wanawake ambao ukitaka apate hamu ya kuwa na wewe ni sharti uongee, umsifu, umtie moyo, uchonge sana maneno matamu yaani TELL ME GIRL.
Inawezekana yeye ni wale wa kuwashirikisha siri, au malengo au jambo lolote unafanya au waza ndipo afunguke kimapenzi yaani SHARE WITH ME GIRL.
Inawezekana mke wako ni walewale usipofanya kazi naye, usipomsaidia vikazi vidogo vidogo pale nyumbani, kupika chakula, kufunga net nk hawezi kujibu kimapenzi yaani DOING GIRL.
Inawezekana ni aina ya mwanamke ambaye ukitaka ufurahie mwili wake na moyo wake chumbani lazima mfanye maombi, au soma Neno (Biblia), au fanya ibada au ongea mambo ya kiroho yaaani SPIRITUAL GIRL.
nk
Je, wewe mwanaume unayesoma hapa unajua mke wako ni aina gani?

Moto unazima!

Mimi ni mwanaume nipo kwenye ndoa sasa mwaka wa 3 excitement ya mapenzi inazidi kufifia na naogopa tunakoelekea kunaonesha kagiza kimapenzi.

Je, unanishauri vipi niweze kurudisha moto wa mapenzi kama ule wa mwanzoni?

Asante kwa swali zuri, na hongera sana kwa kuchukua hatua na zaidi kuonesha nia ya kuhitaji kubadilika kwani kizuizi kikubwa cha mafanikio ya ndoa nyingi ni mitazamo wa kugoma kubadilika.

Jambo la msingi napenda kukukumbusha tu kwamba unatakiwa kufanya yale ulikuwa unafanya pale mwanzo kama vile:-

Je, unakumbuka namna mlikuwa mnapeana kisses na hugs pale mwanzo?

Tafuta muda na uwe na muda wa kumfurahia mwenzako kwa kumpa ladha za mabusu kwenye lips zake.

Maandalizi ya moto wa mapenzi huanzia nje ya chumbani hivyo ni busara kuhakikisha unakuwa connected na mke wako kwa kuwa na mawasiliano mazuri kimwili, kiroho na kimoyo.

Je, mnapomaliza sex huwa inakuwaje?

Kama huwa unazama kwenye usingizi na kumwacha mke wako bila kuendelea kuwa mwilini mwake na kumweleza namna unajisikia na raha unayopata na namna unavyompenda, Kumbuka wakati kama huu ni muhimu kuwa karibu zaidi kuliko mwanzo wa maandalizi ya kufanya mapenzi.

Je, unaendelea kuwa mwanafunzi wa kujifunza na kuwa mbunifu chumbani kwako?

Je, unajua mke wako anasisimka zaidi kwa kumfanyia vitu gani?

Vumbua maeneo yote anayoweza kusisimka kwani huwezi kufanya kile kile kila siku na akajisikia kusisimka na excited kwani si vibaya sana mke wako kufahamu kwamba mkiingia chumbani anajua utafanya 1, 2, 3, 4 kama kawaida yako.

Pia fahamu anaposema nimeridhika kwake ina maana gani.

Zaidi kumbuka unavyoendelea na ndoa mambo hubadilika, kuna masuala ya kazi, majukumu, maisha nk na kuna wakati mke huchoka, huwa na nguvu, hukasirika, huweza kutokea huzuni na misiba nk hii ina maana kuna aina mbali mbali za sex tofauti na siku ya honeymoon wakati ule wote lengo na mitazamo ulikuwa kupeana raha na kila mmoja alikuwa na matarajio makubwa sana.

Kuna wakati mke wako atajisikia hamu kubwa ya kufanya mapenzi na kutamani kila kinachotembea akirukie, hapa inabidi ujue upepo umevuma ili apewe perfect sex, fireworks na jitahidi kuwa connected na yeye then atafurahia hata kufika kileleni mara mbilimbili, hapo kazi kwako!

Kuna wakati mmoja atakuwa anahitaji kubwa la sex na mwingine hana hiyo hamu na Jifunze kwamba mnaweza kupeana sex ya chapuchapu (quickie) na mwingine kuridhika na mwingine kuendelea na ratiba zake.

Inawezekana pia wewe ukawa huna mood ya sex lakini mke wako anakuhitaji.

Hapa huhitaji kung’ang’ania iwe kama ile ya jana.

Pia kuna wakati mke wako au wewe mmoja atakutana na shida au huzuni na mmoja atahitaji kumfariji mwenzake na hakuna kitu muhimu na kizuri kama mmoja aliyehuzunishwa kujikukuta yupo kifuani na kuzungukwa na mikono ya mwenzi wake huku akipata maneno ya faraja na hata kushirikiana mwili hata katika huzuni (comfort sex).

Utakuwa hatua moja mbele kama utafahamu aina za sex katika ndoa na sababu zake na pia kufahamu kwamba lengo la sex wakati mwingine si kufika kileleni bali kuwa connected.

Pia uwe mwepesi kuweka wazi matarajio yako kwani mke huhitaji kuandaliwa kiakili kabla ya kuingiza chumbani hivyo kama kuna migongano, mvurugano au jambo ambalo lipo pending bila kupewa ufumbuzi basi linapewa ufumbuzi kabla ya kuingiza chumbani.

Kwa hapo Naamini unaweza kuwasha upya moto wa mahaba chumbani kwako na mwenzi wako kama mwanzo.

Wednesday, June 15, 2011

Nabubujikwa na machozi!

Mimi na mume wangu tuna maisha mazuri sana hasa linapokuja suala la sex. Hata hivyo siku nikiwa nimemtamani sana mume wangu (horny day) tukiwa kwenye sex hasa ninapofika kileleni huwa najisikia kulia machozi, sijui kwa nini? Je, ni kawaida kwa mwanamke kulia machozi wakati au baada ya sex?

Nahisi mume wangu huwa hajisikii vizuri (comfortable) kwa kuwa anahisi labda huwa naumizwa.

Je, hii huwatokea na wengine?

Ni mimi Jane J.

Asante kwa swali zuri hata hivyo ni kweli kwamba kama wakati wa sex na hasa unapofika kileleni huwa unajikuta unatiririsha machozi ya uhakika ni hakika unaweza kuchanganykiwa, kukatishwa tamaa na wakati mwingine. Hata hivyo nikuhakikishie tu kwamba hii huwatokea wanawake wengi na ni kitu cha kawaida. Ukweli wanawake wengi hujikuta wanabubujikwa na machozi bila sababu ya msingi wakati, na hata baada ya sex, na kuwaacha wapenzi wao wasijue cha kufanya.

Kuna wakati sababu ya kutoa machozi hujulikana na kuna wakati ni siri kubwa.

Ukweli ni mwitikio wa kawaida kihisia (emotions) kwani wapo watu hujikuta wakibubujikwa na kicheko, au kujikuta ana kiu au njaa ya chakula na wengine hulala fofofo na kuwa kama wamezimia na wengine hupiga kelele na hata kuimba au kutoa matusi ya nguoni na hii ni mwitikio wa kawaida kihisia kwa kufika kileleni.

Unapofika kileleni mwili hufanya majumuisho ya kuachia raha ya jumla na hii husukuma mwitikio wa tukuko (emotions/feelings) na kwako huo mwitikio ni kububujika machozi.

Pia ifahamike kwamba sex kati ya wawili wanaopendana ni suala la kumilikiana na kuingizana ndani ya kila mmoja kwenye nafsi ya mwenzake na wakati mwingine mwitikio unaotokea huwa nje ya ufahamu (unconscious level) wa hao wawili namna walivyounganishwa na matokeo yake mwanamke ambaye kwake suala la hisia huunganishwa na sex hujikuta akibubujikwa na machozi bila yeye mwenyewe kufahamu sababu halisi.

Jambo la msingi ni kwamba kama unajisikia raha na huku kuna kilio na machozi ni suala la mwenzako kuelewa kwamba ni mwitikio wa kazi yake nzuri ya kukufikisha pale unahitaji na si vinginevyo.

Haina haja kuwa na hofu kwani ni jambo la kawaida tu.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

Monday, June 13, 2011

Hujiona "Empty"

Darasa lipo "Empty"

Kaka pole na kazi, mimi ni mwanamke ambaye nimedumu kwenye ndoa kwa miaka 7 sasa na nahisi kitu kisicho cha kawaida kwani tunapokuwa kwenye tendo la ndoa najisikia safi tu ila tukisha maliza najiona empty ndani (sijisikii kuridhika na kuwa relaxed au kuwa karibu na mume wangu).

Je hii ni kawaida?

Elizabeth P.

Dada Elizabeth P.

Kwanza asante kwa kuuliza swali na hii ni kumaanisha kwamba unachukulia uzito na maana kubwa kwa mahusiano ya ndoa na mume wako na kwamba upo makini kuhakikisha ndoa yako inakuwa na afya.

Jambo la msingi ni kufahamu kwamba hisia zako (feelings) zina uhusiano mkubwa sana na kiwango cha ukaribu na imara wa mahusiano ya ndoa yako na mumeo.

Tendo la ndoa linatakiwa kuwaweka au kuwapa ukaribu wa kimapenzi wewe na mume wako na si wewe kujisikia mweupe (empty) baada ya kufanya mapenzi.

Kama unajisikia empty baada ya tendo la ndoa hii ina maana kwamba kuna kitu kinakosekana katika mahusiano yako na mumeo.

Jaribu kuchunguza mahusiano yako na mumeo nje ya chumbani.

Je, mume wako anakuchukulia (treat) vipi? Na wewe unamchukulia vipi mumeo?

Je, kuna tatizo lolote katika maeneo yoyote katika maisha yenu wewe na mumeo hamjamalizana au kuna jambo ambalo halijapatiwa ufumbuzi kati yako na mumeo na linasumbua sana kichwa chako?

Hayo yanaweza kuathiri namna unajisikia mkiwa wote katika tendo la ndoa.

Fikiria tendo la ndoa na namna unajisikia baada ya kumaliza ni kipima joto cha mahusiano yenu, na kama kuna conflicts nje ya chumbani haitakuwa rahisi kuwa na joto la kutosha la mapenzi chumbani mkiwa na faragha yenu.

Kuwa na migongano nje ya chumbani kupelekea mkiwa chumbani wote au mmoja kuwa jiwe lisilosikia lolote katika kuridhika na tendo la ndoa.

Unavyojisikia empty hiyo ni dalili (workup call) kwamba kuna kitu kinatakiwa kuwekwa sawa katika mahusiano yako na mumeo ndani na nje ya chumbani katika maisha yenu ya kila siku.

Pia inabidi utambue kwamba kuna mahitaji mengine ambayo sex haiwezi kutimiza isipokuwa ukaribu wako na mumeo nje ya chumbani.

Mara nyingi mtu kujisikia empty mara baada ya sex ni dalili ya namna wasivyokaribu (feelings distanced) na partner ambaye wamekuwa pamoja kimwili.

Pia Inawezekana ni namna ulijihusisha katika mapenzi kabla ya kuolewa na mumeo au mtu mwingine (sina uhakika kwani hujaniambia historia yako kimahusiano kabla ya kuolewa ilikuwaje).

Kama kabla ya kuoana mlishiriki mapenzi (sex) na mumeo hii ina maana kwamba ulimpa mumeo kipande cha moyo wako na mwili wako kitu ambacho huwezi kupata tena au kurudishiwa.

Pia kama huko nyuma uliwahi kudhalilishwa kimapenzi si rahisi kufuta kumbukumbu za hivyo vitendo hadi kufanyika kwa ushauri wa Kitaalamu namna ya kuondokana na hizo hisia hasa namna unajisikia kuhusu sex.

Bila kujali nini kimesababisha wewe kujisikia empty, jambo la msingi ni wewe kufanyia kazi kuanzia leo.

Bottom line ni kwamba kazi kubwa kwa mwanandoa (wewe unayesoma hapa) ni kujiuliza na kupata jibu kwa nini mmoja wenu (wewe au yeye) au wote kuwa kama jiwe wakati muhimu wa kuwa mwili mmoja?

Chukua hatua sasa.

Kiumbe huyu!


Wakati mwingine ni vigumu sana kwa wanawake kufahamu ni kiasi gani hamu ya kufanya mapenzi ilivyo kwa mwanaume.
Ingawa wanaume hutofautiana katika kiwango cha hamu ya mapenzi bado wanaume wanaonekana wapo juu katika hamu ya mapenzi kuliko wanawake.
Wataalamu wa masuala ya mapenzi (sex) wanasema kwamba mwanaume ni mtu wa mzunguko wa siku tano ( kwa maana kwamba huhitaji sex kila baada ya siku tano) na wakati huohuo mwanamke ni mtu wa mzunguko wa siku kumi ( kwa maana kwamba huhitaji sex kila baada ya siku kumi), kuna kaukweli fulani katika hili.
Hata hivyo kuna wanaume wengi sana hasa vijana wao hupenda kupata sex ikiwezekana kila siku na pengine wangependa iwe zaidi ya hapo kama miili yao ingeruhusu.
Je, hii ina maana gani kwako mwanamke?
Hii ina maana kwamba mume wako anapenda sana sex.
Pia anawaza sana kuhusu sex kila mara kuliko wewe unavyowaza kuhusu sex.
Haijalishi ni gentle and romantic kiasi gani lakini mwisho wa siku anachowaza ni kufanya sex na wewe.
Kwa kuwa ana drive kubwa ya sex kuliko wewe na anajisikia kufanya mapenzi na wewe, ukimzungusha anaweza kuchukua risk kubwa sana ya masuala ya sex bila kujali consequences zitakazompata (kutokuwa mwaminifu kwako, kulipa fedha apate sex nk).
Pia fahamu kwamba mwanaume humpenda mwanamke kwa mtindo wa vipande vipande kwa maana kwamba anaweza kuvutiwa na namna mwanamke anaonekana sura yake, miguu yake, matiti yake, meno yake akicheka, kiuno chake, makalio yake na wakati mwingine hata perfume ambayo mwanamke amejipiga.
Hivyo basi kama wewe ni mwanamke unasoma hapa hata siku moja usitanie kuhusu nguvu aliyonayo mume wako kuhusu sex.
Unatahadhalishwa!

Tuesday, June 7, 2011

Mara nyingi wanawake huwacheka sana wanaume ambao visamaki vyao ni vidogo sana kwa kuwatania kwamba hata ukikohoa tu wakati wapo sita kwa sita kanachomoka, wakati huohuo wanaume nao huwacheka wanawake ambao huko chini kwenye machimbo ya dhahabu kuna pwaya mno kiasi kwamba mwanaume akiingiza mpini hasikii kitu chochote yaani hakuna ule mgusano au msuguano unaoleta raha ya tendo la ndoa.

Pia kuna wanawake ambao uke umejaa maji kwelikweli hata uume ukiwa ndani ni kuteleza tu bila msuguano wowote wala kubana kokote matokeo yake hakuna ladha na utamu wa tendo lenyewe.

Je, kuna dawa yoyote ya kuweza kutibu hivyo visa?

Dawa ipo, tena bure na ipo ndani ya uwezo wako, kitu cha msingi ni kukubali mabadiliko na kuwa na hamu ya kutaka kubadilika.

Kukubali kubadilika na kutaka kuwa na uke tight unaokupa raha wewe na mume wako na zaidi afya yako ya uzazi kuwa imara.

Ni kawaida wanaume wengi kuogopa kwenda kwa daktari kuongea masuala ya afya ya uzazi, hapa huhitaji kwenda kwa daktari, daktari ni wewe mwenyewe kuwa serious, kwani ukifanya vizuri utakuwa na uwezo wa kusimamisha mti wako kwa muda mrefu na pia unaweza kuhimili kubana kutofika kileleni mapema kabla ya mwandani wako.

Wanawake wengi baada ya kuzaa zaidi ya mara moja na kama hawakuwa watu wa mazoezi, misuli ya uke hulegea na kupelekea kupoteza mnato na u-tight wa uke na pia kutojiamini wakati wa kufanya mapenzi kutokana na kupwaya kwa uke.

Dawa ya hili tatizo ni kufanya zoezi la kukaza misuli ya PC

Kitaalamu hili zoezi huweza kurudisha hiyo hali ya kuwa tight baada ya miezi miwili kwa kufanya kila siku mfululizo na kwa kujitoa na kuwa serious.

Je, hili zoezi ni gumu?

Si gumu,

Ni rahisi sana,

Ni salama.

Siyo zito na halichoshi.

Linaweza kukupa matokeo baada ya wiki nane

Je, unaanzaje au nitajuaje huu ndo msuli wenyewe?

Kwanza ili kufanya hili zoezi anza kwa kutambua misuli ya uke au uume inayohusika kwa kuzuia mkojo unapotoka, then kojoa kwa kukata huku ukikaza misuli kwa kutoa mkojo kwa kuhesabu sekunde 4 hadi 10 au namba 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10 ndipo unakojoa tena ujazo wa kijiko cha chai na hatimaye unaanza upya kwa kukata na kuhesabu 1 – 10 kila unapoenda kukojoa muda wowote.

Hii inasaidia kutambua msuli unaohusika na kukaza uke au uume.

Msuli uliotumia kuzuia mkojo ni rahisi kuuhisi na ndo huo unahusika.

Hii misuli husaidia kukaza matundu matatu huko chini kwa mwanamke ambayo ni uke, tundu la mkojo na tundu la kutolea haja kubwa.

Ndiyo maana watu wanaofanya upuuzi ule wa sodoma na gomora kuna wakati huhitaji kuvalishwa nepi maana misuli imelegea hauwezi kuzuia tena haja kubwa.

Ukishapatia kujua msuli upi unatumia kuzuia mkojo, basi unaweza kuendelea na zoezi hata kama hukojoi kwa kuendelea kukaza kama vile unakojoa ingawa siyo.

Unaweza kurudia zoezi muda wowote hata kama hukojoi mahali popote, kwenye kiti ofisini, kwenye daladala nk.

Wakati unafanya Hakikisha kuna tofauti ya sekunde tatu hadi kumi.

Pia unaweza kuongeza kukaza hiyo misuli kila ukikojoa, fanya zaidi ya 20 kwa siku

Fanya kwa wiki nane mfululizo.

Kama wewe ni mwanamke ambaye chini kunapwaya au mume wako amekuwa analalamika kwamba hapati ladha na utamu halisi basi hili zoezi la kubana misuli litakuwezesha kubana uume au kuuvuta kwa ndani (milking), au kwa kuukamua hatimaye anapata raha kwa msuguano unaokuwepo na wewe kufika kileleni haraka.

Ukitaka kujua uke wako unakubali zoezi jaribu kuingiza kidole wakati unafanya hili zoezi then utahisi kidole kubana zaidi kuliko kawaida.

Basi tu awe na wewe!

Black is beautiful! Fikiria wewe ni binti mwenye sifa zote za kuolewa (excellent marriage material) na umri wako ni sahihi kuolewa, umempata kijana wa kiume mwenye sifa zote za kuoana na wewe.
Anakujali kwa kila kitu na unaona mambo yanaenda vizuri, baada ya muda mrefu unaamua kumuuliza akupe majibu lini mnaweza kuoana, yeye anakuruka na kusema muda bado na unapoendelea kumuuliza akupe majibu sahihi anagoma na kukuacha huku hujui kama kweli yupo committed.

Unajiuliza na kujihoji kama kweli anakupenda na ana upendo wa kweli kwako na je upendo wake kwako una maana yoyote kama hataki kujitoa na kuamua kuoana?

Unajiuliza kwa ukaribu (intimate) uliopo je kuna tatizo gani kwake kushindwa kukubali lini tuoane na kuamua kuishi kama mke na mume?
Kila siku inayoenda unajikuta una maswali mengi kuliko majibu.

Swali kuu ni kwa nini huyu mwanaume anakugeuka tu pale unapotaja suala la kwenda madhabahuni kufunga ndoa ili kuthibitisha kwamba anakujali, anakupenda na kwamba wewe ndiyo chaguo lake duniani kama anavyotamka mkiwa pamoja.

Je, ungekuwa wewe ni huyu mwanamke ungefanyeje?

Ukweli ni kwamba kuna wanaume ambao ni ovyo, hujiingiza katika mahusiano bila lengo la kuoana bali “just for fun

Pia ieleweke kwamba hakuna mwanamke anaweza kulazimisha mwanaume kumuoa kama mwanaume mwenyewe hayupo tayari au hataki.
Ukweli ni kwamba unavyozidi kumlazimisha ndivyo anatakavyokuwa mgumu zaidi kukubali.

Jambo la msingi ni kumuuliza huyo mwanaume mapema kabisa kabla uhusiano haujafika mbali akueleze wazi maana ya uhusiano mnaoanza ili asikupotezee muda wako wa thamani na kuchezea hisia zao na kukupa matumaini makubwa wakati hana mpango wowote bali kujifurahisha.

Pia wapo wanaume ambao kwao kuoa ni kupoteza uhuru, kuongezewa majukumu, wanaamini ukishaoa unapoteza uhuru na zaidi “kwa nini ununue ng’ombe kama unaweza kupata maziwa bure”

Haina haja kuwa katika mahusiano ambayo mmoja hakubaliani na aina ya mahusiano unahitaji.

Nani zaidi?

Hapo zamani hasa katika desturi na mitazamo ya mila za kiafrika, mwanamke aliyeolewa akiwa mnene alipongezwa kwa kupata mume tajiri na pia kama hajaolewa wanaume walimpapatikia kwa kuwa ana dalili ya afya njema.
Katika kizazi cha leo meza zimegeuzwa na kumezuka mabishano ya nani zaidi katika ya mwanamke mnene au mwembamba (skinny VS Fatty).
Pia kumekuwa na juhudi za wanawake kupunguza unene tofauti na zamani.

Sipendi kufahamu kile unawaza au kufikiri bali napenda kujua uhalisi wa uzoefu wako je, mwanamke mnene na mwembamba nani zaidi?

Huwezi kutoa Amri!Kwa kuwa asilimia kubwa ya sex organ kwa mwanaume ni nje ya mwili na huonekana kirahisi kuna imani potofu kwamba size ya uume ndiyo jambo la msingi katika kazi.
Na wapo wanawake huamini kwamba kazi ya mwanaume ni kutoa amri kwa uume wake na automatically unasimama na kuwa tayari kwa kazi.

Kukosa uelewa na ufahamu wa namna hiki kiungo kinavyofanya kazihupelekea kwa baadhi ya wanandoa kutoridhishana na hata kuwa frustrated wakati wa faragha zao.
Kufahamu namna hiki kiungo cha thamani kinavyofanya kazi huweza kukufanya uwe na maisha salama ya kimapenzi kwa Yule unayempenda.

Je, nini hutokea mwanaume anaposisimka kimapenzi?
Ubongo husafirisha taarifa za kusisimka (iwe baada ya kuona au kuguswa) hadi kwenye uume na damu inayoingia huko huzuiliwa isitoke na hii hufanya uume kudinda na huweza kubadilisha direction kutoka kulala na kuangalia chini hadi kusimama na kunyooka kwa kwenda juu mithili ya mti au fimbo.

Hakuna mwanaume duniani anaweza kuamrisha uume wake kusimama kwani sehemu inayosimamia uume kusimama katika Ubongo ni ile inajitegemea bila ufahamu (unconscious level), ingawa mawazo ya ufahamu (conscious) husababisha au kuzuia uume kusimama.
Wapo wanawake ambao hawajui kwamba mwanaume hana uwezo au ujanja wa kuamua erection itokee na huwa very disappointed pale mwanaume anapomaliza na uume kulala kabla ya yeye mwanamke kuridhika.
Hata hivyo silaha muhimu kwa mwanamke anapoona uume wa mume wake umegoma kazi ni kutoa neno tamu au kumtia moyo au kumsifia na hiyo inaweza kuwa switch ya kufungua na baada ya sekunde Mr. happy anaweza kusimama wima na kuwa tayari kwa kazi.

Hii ina maana kwamba mwanaume ambaye fimbo yake imegoma kuendelea na kazi hataweza kushiriki sex wakati mwanamke hata kama hajisikii bado anaweza kushiriki sex pale tu penetration ikiwezekana.
Pia hii ina maana mwanamke anaweza kudanganya (fake) sex na mambo yakawa shwari hata kama hana hamu, wakati mwanaume haiwezekani kudanganya kwani uume lazima usimame na hawezi kulazimisha au kutoa amri uume usimame.
Baada ya mwanaume kufika kileleni uume hurudi katika hali yake ya kawaiada na mwanaume hujisikia kulala usingizi. Na hapo mwanaume huhitaji muda zaidi ili aweze kufanya tena labda awe bado kijana sana kwani kwa mwanaume wa miaka mingi huhitaji masaa kadhaa ili aweze kurudia tena.
Uimara na ugumu wa uume wake ukiwa umesimama ni kipimo cha uwezo wake wa kusisimka hata hivyo mwanaume anaweza kuonesha dalili zote za kusisimka na bado akawa na poor erection kwa sababu ya labda uchovu, au kutokuwa tayari kwa sex kutokana na mawazo au kukosa nguvu za kiume (impotent).

Mwanamke anaweza kutumia trick ya kuingiza uume ambao haujasimama vizuri (half erection) huku akiendelea kumpa kisses, maneno matamu na kumshikashika sehemu tofauti kimahaba hii husababisha uume kusimama na wakaendelea kufurahia mapenzi.
Hii ina maana soft erection kwa mwanaume haina maana kwamba ni mwisho wa sex.
Pia hakuna ushahidi unaoonesha kisayansi kwamba baada ya mwanaume kukua kama anaweza kuongeza ukubwa au urefu wa uume wake.
Hakuna mwanaume anaweza kufanya hakuna vidonge wala cream au kitu kinaweza kuongeza size ya uume.
Pia vijana wa umri mdogo mara nyingi humaliza haraka kutokana na kukosa uzoefu wa kuweza kuthibiti mwili ingawa pia kama mwanaume hajashiri sex kwa muda mrefu anaweza kumaliza mapema na ili aweze kutumia muda mrefu kumaliza ni muhimu kushiriki sex na mke wake mara kwa mara.

Muda Maalumu!

Ndoa ni muunganiko (alliance) ambao binadamu hukutana nao na ni muungano muhimu na tofauti kuliko muungano wowote duniani.
Ni muungano muhimu kimwili, kiroho, kiakili na kifedha na hata kisaikolojia.
Mwanaume ambaye amechagua mke kwa busara atahakikisha huyo mke anakuwa mtu wa muhimu sana katika maisha yake na familia yake katika kuunda uwezo pamoja kufanya mambo (master mind) na kutekeleza mikakati ya maisha.

Kutokuelewana kwa mume na mke katika ndoa ni kitu kibaya sana bila kujali ni kwa sababu gani (No matter what); kwani huweza kuharibu kabisa nafasi ya mwanaume yeyote kufanikiwa katika maisha hata kama huyo mwanaume ana sifa zote za kuwa na mafanikio.

Mke anayo influence kubwa kwa mume wake kuliko mwanamke yeyote au mtu yeyote duniani ndiyo maana wanasema “Kila palipo na mwanaume mwenye mafanikio nyuma yake yupo mwanamke (mke wake)”.
Mume wako (kama wewe ni mwanamke) aliamua kukuchagua wewe na kukuoa kwa sababu alikupenda kuliko wanawake wote duniani bila kujali rangi, kabila au utamaduni hii ina maana wewe ndiye mwanamke anayekupenda kuliko wanawake wote duniani labda iwe mlioana kwa ndoa za kulazimishana au kupanga (arranged marriage).

Pia kumbuka kwamba upendo (love) ni moja ya vitu vinavyoweza kumsukuma (motivate) mwanaume kujitolea kufanya kitu chochote au kujitolea kufanya chochote, au kwenda mahali popote ili mradi tu mke ametoa penzi la kweli kwa mume wake.

Pia ikumbukwe kwamba tabia za kukefyakefya, wivu kupindukia, kuona makosa tu au kuendekeza tofauti hakuimarishi mahusiano au ndoa bali huua.
Mwanamke mwenye busara na hekima kutafuta muda au kupanga muda maalumu wa kuongea na mume wake ili kuwa na wakati wa kujadili mustakhabali wa familia (mutual interests) na inaweza kuwa ni wakati wa chakula cha asubuhi (breakfast au chakula cha jioni (supper).

Muda wa chakula hasa cha usiku (supper) ni muda maalumu kwa familia, kukaa pamoja na kuabudu, kufurahia, kuongea na kujadili mambo mazuri ya familia, kucheka na kudumisha umoja wa familia na si kuonyana au kusemana au kunyosheana vidole au kuweka matatizo mezani au kuonya watoto (discipline).

Inaeleweka kwamba “Man’s stomach is the way to his heart” hivyo basi muda wa chakula (ambacho kimeandaliwa vizuri) ni excellent opportunity kwa mke kuweza kufikia moyo wa mume wake kwa wazo lolote analohitaji kulipanda (kama mbegu) kwa moyo wa mumewe, hata hivyo lugha inayotumika iwe ya upendo, hekima na busara bila kujali huyo mume ni cha pombe au la.

Pia jambo la msingi na muhimu ni kwamba mke anahitaji kuwa na interest za kazi ya mume wake (occupation)kwa kumsaidia kimawazo na kivitendo. Ni muhimu kuepuka namna wanawake wengine husema na kutenda kwamba “ Leta fedha nyumbani nitumie na sijali namna umezipata na sina shida ya kujua umezipataje” huo ni ujinga na ipo siku mume hatajali kurudi nyumbani mikono mitupu hata kama amezalisha mamilioni.

Upendo katika ndoa hudumu tu pale mume na mke wanapoishi huku wakiwa na kusudi moja la kuiendesha familia yao.
Na mwanamke anayejua haya atakuwa na influence kubwa kwa mume wake katika maisha yao yote.
Kumbuka mke asiyefanya haya asishangae mume anaanza kutazama nje ili kupata model mpya ya gari la kuliendesha na wewe mwanamke kuwa spare tyre.
Mimi simo!