"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 7, 2011

Basi tu awe na wewe!

Black is beautiful! Fikiria wewe ni binti mwenye sifa zote za kuolewa (excellent marriage material) na umri wako ni sahihi kuolewa, umempata kijana wa kiume mwenye sifa zote za kuoana na wewe.
Anakujali kwa kila kitu na unaona mambo yanaenda vizuri, baada ya muda mrefu unaamua kumuuliza akupe majibu lini mnaweza kuoana, yeye anakuruka na kusema muda bado na unapoendelea kumuuliza akupe majibu sahihi anagoma na kukuacha huku hujui kama kweli yupo committed.

Unajiuliza na kujihoji kama kweli anakupenda na ana upendo wa kweli kwako na je upendo wake kwako una maana yoyote kama hataki kujitoa na kuamua kuoana?

Unajiuliza kwa ukaribu (intimate) uliopo je kuna tatizo gani kwake kushindwa kukubali lini tuoane na kuamua kuishi kama mke na mume?
Kila siku inayoenda unajikuta una maswali mengi kuliko majibu.

Swali kuu ni kwa nini huyu mwanaume anakugeuka tu pale unapotaja suala la kwenda madhabahuni kufunga ndoa ili kuthibitisha kwamba anakujali, anakupenda na kwamba wewe ndiyo chaguo lake duniani kama anavyotamka mkiwa pamoja.

Je, ungekuwa wewe ni huyu mwanamke ungefanyeje?

Ukweli ni kwamba kuna wanaume ambao ni ovyo, hujiingiza katika mahusiano bila lengo la kuoana bali “just for fun

Pia ieleweke kwamba hakuna mwanamke anaweza kulazimisha mwanaume kumuoa kama mwanaume mwenyewe hayupo tayari au hataki.
Ukweli ni kwamba unavyozidi kumlazimisha ndivyo anatakavyokuwa mgumu zaidi kukubali.

Jambo la msingi ni kumuuliza huyo mwanaume mapema kabisa kabla uhusiano haujafika mbali akueleze wazi maana ya uhusiano mnaoanza ili asikupotezee muda wako wa thamani na kuchezea hisia zao na kukupa matumaini makubwa wakati hana mpango wowote bali kujifurahisha.

Pia wapo wanaume ambao kwao kuoa ni kupoteza uhuru, kuongezewa majukumu, wanaamini ukishaoa unapoteza uhuru na zaidi “kwa nini ununue ng’ombe kama unaweza kupata maziwa bure”

Haina haja kuwa katika mahusiano ambayo mmoja hakubaliani na aina ya mahusiano unahitaji.

2 comments:

Anonymous said...

ni kweli unachochosema kaka,nadhani ungefundisha somola uvumilivu,kwa sababu ukisema tuachane na watu wetuambao kweli suala la madhabahuni wabishi sana,lakini wanatusaidia,sasa tukisema tuachane nao tutaishije mjini hapa na sie wengine maisha yetu ni ya kuunga tu,tutaachana na wangapi?au unataka tuwe na list ya wanaume?

Lazarus Mbilinyi said...

So ni afadhari kuwa nawe mradi tu uwe naye hata kama unaelewa future haipo?

Hata hivyo wanaume wa aina hii uwe naye na usiwe naye haina maana kwani ipo siku anakupiga chini.

Tanguliza Mungu na weka malengo pia hata kama umeungaunga maisha jambo la msingi jiamini unaweza hata kama hujawezeshwa period