"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, June 13, 2011

Hujiona "Empty"

Darasa lipo "Empty"

Kaka pole na kazi, mimi ni mwanamke ambaye nimedumu kwenye ndoa kwa miaka 7 sasa na nahisi kitu kisicho cha kawaida kwani tunapokuwa kwenye tendo la ndoa najisikia safi tu ila tukisha maliza najiona empty ndani (sijisikii kuridhika na kuwa relaxed au kuwa karibu na mume wangu).

Je hii ni kawaida?

Elizabeth P.

Dada Elizabeth P.

Kwanza asante kwa kuuliza swali na hii ni kumaanisha kwamba unachukulia uzito na maana kubwa kwa mahusiano ya ndoa na mume wako na kwamba upo makini kuhakikisha ndoa yako inakuwa na afya.

Jambo la msingi ni kufahamu kwamba hisia zako (feelings) zina uhusiano mkubwa sana na kiwango cha ukaribu na imara wa mahusiano ya ndoa yako na mumeo.

Tendo la ndoa linatakiwa kuwaweka au kuwapa ukaribu wa kimapenzi wewe na mume wako na si wewe kujisikia mweupe (empty) baada ya kufanya mapenzi.

Kama unajisikia empty baada ya tendo la ndoa hii ina maana kwamba kuna kitu kinakosekana katika mahusiano yako na mumeo.

Jaribu kuchunguza mahusiano yako na mumeo nje ya chumbani.

Je, mume wako anakuchukulia (treat) vipi? Na wewe unamchukulia vipi mumeo?

Je, kuna tatizo lolote katika maeneo yoyote katika maisha yenu wewe na mumeo hamjamalizana au kuna jambo ambalo halijapatiwa ufumbuzi kati yako na mumeo na linasumbua sana kichwa chako?

Hayo yanaweza kuathiri namna unajisikia mkiwa wote katika tendo la ndoa.

Fikiria tendo la ndoa na namna unajisikia baada ya kumaliza ni kipima joto cha mahusiano yenu, na kama kuna conflicts nje ya chumbani haitakuwa rahisi kuwa na joto la kutosha la mapenzi chumbani mkiwa na faragha yenu.

Kuwa na migongano nje ya chumbani kupelekea mkiwa chumbani wote au mmoja kuwa jiwe lisilosikia lolote katika kuridhika na tendo la ndoa.

Unavyojisikia empty hiyo ni dalili (workup call) kwamba kuna kitu kinatakiwa kuwekwa sawa katika mahusiano yako na mumeo ndani na nje ya chumbani katika maisha yenu ya kila siku.

Pia inabidi utambue kwamba kuna mahitaji mengine ambayo sex haiwezi kutimiza isipokuwa ukaribu wako na mumeo nje ya chumbani.

Mara nyingi mtu kujisikia empty mara baada ya sex ni dalili ya namna wasivyokaribu (feelings distanced) na partner ambaye wamekuwa pamoja kimwili.

Pia Inawezekana ni namna ulijihusisha katika mapenzi kabla ya kuolewa na mumeo au mtu mwingine (sina uhakika kwani hujaniambia historia yako kimahusiano kabla ya kuolewa ilikuwaje).

Kama kabla ya kuoana mlishiriki mapenzi (sex) na mumeo hii ina maana kwamba ulimpa mumeo kipande cha moyo wako na mwili wako kitu ambacho huwezi kupata tena au kurudishiwa.

Pia kama huko nyuma uliwahi kudhalilishwa kimapenzi si rahisi kufuta kumbukumbu za hivyo vitendo hadi kufanyika kwa ushauri wa Kitaalamu namna ya kuondokana na hizo hisia hasa namna unajisikia kuhusu sex.

Bila kujali nini kimesababisha wewe kujisikia empty, jambo la msingi ni wewe kufanyia kazi kuanzia leo.

Bottom line ni kwamba kazi kubwa kwa mwanandoa (wewe unayesoma hapa) ni kujiuliza na kupata jibu kwa nini mmoja wenu (wewe au yeye) au wote kuwa kama jiwe wakati muhimu wa kuwa mwili mmoja?

Chukua hatua sasa.

No comments: