"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, June 16, 2011

Moto unazima!

Mimi ni mwanaume nipo kwenye ndoa sasa mwaka wa 3 excitement ya mapenzi inazidi kufifia na naogopa tunakoelekea kunaonesha kagiza kimapenzi.

Je, unanishauri vipi niweze kurudisha moto wa mapenzi kama ule wa mwanzoni?

Asante kwa swali zuri, na hongera sana kwa kuchukua hatua na zaidi kuonesha nia ya kuhitaji kubadilika kwani kizuizi kikubwa cha mafanikio ya ndoa nyingi ni mitazamo wa kugoma kubadilika.

Jambo la msingi napenda kukukumbusha tu kwamba unatakiwa kufanya yale ulikuwa unafanya pale mwanzo kama vile:-

Je, unakumbuka namna mlikuwa mnapeana kisses na hugs pale mwanzo?

Tafuta muda na uwe na muda wa kumfurahia mwenzako kwa kumpa ladha za mabusu kwenye lips zake.

Maandalizi ya moto wa mapenzi huanzia nje ya chumbani hivyo ni busara kuhakikisha unakuwa connected na mke wako kwa kuwa na mawasiliano mazuri kimwili, kiroho na kimoyo.

Je, mnapomaliza sex huwa inakuwaje?

Kama huwa unazama kwenye usingizi na kumwacha mke wako bila kuendelea kuwa mwilini mwake na kumweleza namna unajisikia na raha unayopata na namna unavyompenda, Kumbuka wakati kama huu ni muhimu kuwa karibu zaidi kuliko mwanzo wa maandalizi ya kufanya mapenzi.

Je, unaendelea kuwa mwanafunzi wa kujifunza na kuwa mbunifu chumbani kwako?

Je, unajua mke wako anasisimka zaidi kwa kumfanyia vitu gani?

Vumbua maeneo yote anayoweza kusisimka kwani huwezi kufanya kile kile kila siku na akajisikia kusisimka na excited kwani si vibaya sana mke wako kufahamu kwamba mkiingia chumbani anajua utafanya 1, 2, 3, 4 kama kawaida yako.

Pia fahamu anaposema nimeridhika kwake ina maana gani.

Zaidi kumbuka unavyoendelea na ndoa mambo hubadilika, kuna masuala ya kazi, majukumu, maisha nk na kuna wakati mke huchoka, huwa na nguvu, hukasirika, huweza kutokea huzuni na misiba nk hii ina maana kuna aina mbali mbali za sex tofauti na siku ya honeymoon wakati ule wote lengo na mitazamo ulikuwa kupeana raha na kila mmoja alikuwa na matarajio makubwa sana.

Kuna wakati mke wako atajisikia hamu kubwa ya kufanya mapenzi na kutamani kila kinachotembea akirukie, hapa inabidi ujue upepo umevuma ili apewe perfect sex, fireworks na jitahidi kuwa connected na yeye then atafurahia hata kufika kileleni mara mbilimbili, hapo kazi kwako!

Kuna wakati mmoja atakuwa anahitaji kubwa la sex na mwingine hana hiyo hamu na Jifunze kwamba mnaweza kupeana sex ya chapuchapu (quickie) na mwingine kuridhika na mwingine kuendelea na ratiba zake.

Inawezekana pia wewe ukawa huna mood ya sex lakini mke wako anakuhitaji.

Hapa huhitaji kung’ang’ania iwe kama ile ya jana.

Pia kuna wakati mke wako au wewe mmoja atakutana na shida au huzuni na mmoja atahitaji kumfariji mwenzake na hakuna kitu muhimu na kizuri kama mmoja aliyehuzunishwa kujikukuta yupo kifuani na kuzungukwa na mikono ya mwenzi wake huku akipata maneno ya faraja na hata kushirikiana mwili hata katika huzuni (comfort sex).

Utakuwa hatua moja mbele kama utafahamu aina za sex katika ndoa na sababu zake na pia kufahamu kwamba lengo la sex wakati mwingine si kufika kileleni bali kuwa connected.

Pia uwe mwepesi kuweka wazi matarajio yako kwani mke huhitaji kuandaliwa kiakili kabla ya kuingiza chumbani hivyo kama kuna migongano, mvurugano au jambo ambalo lipo pending bila kupewa ufumbuzi basi linapewa ufumbuzi kabla ya kuingiza chumbani.

Kwa hapo Naamini unaweza kuwasha upya moto wa mahaba chumbani kwako na mwenzi wako kama mwanzo.

No comments: