"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 7, 2011

Muda Maalumu!

Ndoa ni muunganiko (alliance) ambao binadamu hukutana nao na ni muungano muhimu na tofauti kuliko muungano wowote duniani.
Ni muungano muhimu kimwili, kiroho, kiakili na kifedha na hata kisaikolojia.
Mwanaume ambaye amechagua mke kwa busara atahakikisha huyo mke anakuwa mtu wa muhimu sana katika maisha yake na familia yake katika kuunda uwezo pamoja kufanya mambo (master mind) na kutekeleza mikakati ya maisha.

Kutokuelewana kwa mume na mke katika ndoa ni kitu kibaya sana bila kujali ni kwa sababu gani (No matter what); kwani huweza kuharibu kabisa nafasi ya mwanaume yeyote kufanikiwa katika maisha hata kama huyo mwanaume ana sifa zote za kuwa na mafanikio.

Mke anayo influence kubwa kwa mume wake kuliko mwanamke yeyote au mtu yeyote duniani ndiyo maana wanasema “Kila palipo na mwanaume mwenye mafanikio nyuma yake yupo mwanamke (mke wake)”.
Mume wako (kama wewe ni mwanamke) aliamua kukuchagua wewe na kukuoa kwa sababu alikupenda kuliko wanawake wote duniani bila kujali rangi, kabila au utamaduni hii ina maana wewe ndiye mwanamke anayekupenda kuliko wanawake wote duniani labda iwe mlioana kwa ndoa za kulazimishana au kupanga (arranged marriage).

Pia kumbuka kwamba upendo (love) ni moja ya vitu vinavyoweza kumsukuma (motivate) mwanaume kujitolea kufanya kitu chochote au kujitolea kufanya chochote, au kwenda mahali popote ili mradi tu mke ametoa penzi la kweli kwa mume wake.

Pia ikumbukwe kwamba tabia za kukefyakefya, wivu kupindukia, kuona makosa tu au kuendekeza tofauti hakuimarishi mahusiano au ndoa bali huua.
Mwanamke mwenye busara na hekima kutafuta muda au kupanga muda maalumu wa kuongea na mume wake ili kuwa na wakati wa kujadili mustakhabali wa familia (mutual interests) na inaweza kuwa ni wakati wa chakula cha asubuhi (breakfast au chakula cha jioni (supper).

Muda wa chakula hasa cha usiku (supper) ni muda maalumu kwa familia, kukaa pamoja na kuabudu, kufurahia, kuongea na kujadili mambo mazuri ya familia, kucheka na kudumisha umoja wa familia na si kuonyana au kusemana au kunyosheana vidole au kuweka matatizo mezani au kuonya watoto (discipline).

Inaeleweka kwamba “Man’s stomach is the way to his heart” hivyo basi muda wa chakula (ambacho kimeandaliwa vizuri) ni excellent opportunity kwa mke kuweza kufikia moyo wa mume wake kwa wazo lolote analohitaji kulipanda (kama mbegu) kwa moyo wa mumewe, hata hivyo lugha inayotumika iwe ya upendo, hekima na busara bila kujali huyo mume ni cha pombe au la.

Pia jambo la msingi na muhimu ni kwamba mke anahitaji kuwa na interest za kazi ya mume wake (occupation)kwa kumsaidia kimawazo na kivitendo. Ni muhimu kuepuka namna wanawake wengine husema na kutenda kwamba “ Leta fedha nyumbani nitumie na sijali namna umezipata na sina shida ya kujua umezipataje” huo ni ujinga na ipo siku mume hatajali kurudi nyumbani mikono mitupu hata kama amezalisha mamilioni.

Upendo katika ndoa hudumu tu pale mume na mke wanapoishi huku wakiwa na kusudi moja la kuiendesha familia yao.
Na mwanamke anayejua haya atakuwa na influence kubwa kwa mume wake katika maisha yao yote.
Kumbuka mke asiyefanya haya asishangae mume anaanza kutazama nje ili kupata model mpya ya gari la kuliendesha na wewe mwanamke kuwa spare tyre.
Mimi simo!

No comments: