"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 15, 2011

Nabubujikwa na machozi!

Mimi na mume wangu tuna maisha mazuri sana hasa linapokuja suala la sex. Hata hivyo siku nikiwa nimemtamani sana mume wangu (horny day) tukiwa kwenye sex hasa ninapofika kileleni huwa najisikia kulia machozi, sijui kwa nini? Je, ni kawaida kwa mwanamke kulia machozi wakati au baada ya sex?

Nahisi mume wangu huwa hajisikii vizuri (comfortable) kwa kuwa anahisi labda huwa naumizwa.

Je, hii huwatokea na wengine?

Ni mimi Jane J.

Asante kwa swali zuri hata hivyo ni kweli kwamba kama wakati wa sex na hasa unapofika kileleni huwa unajikuta unatiririsha machozi ya uhakika ni hakika unaweza kuchanganykiwa, kukatishwa tamaa na wakati mwingine. Hata hivyo nikuhakikishie tu kwamba hii huwatokea wanawake wengi na ni kitu cha kawaida. Ukweli wanawake wengi hujikuta wanabubujikwa na machozi bila sababu ya msingi wakati, na hata baada ya sex, na kuwaacha wapenzi wao wasijue cha kufanya.

Kuna wakati sababu ya kutoa machozi hujulikana na kuna wakati ni siri kubwa.

Ukweli ni mwitikio wa kawaida kihisia (emotions) kwani wapo watu hujikuta wakibubujikwa na kicheko, au kujikuta ana kiu au njaa ya chakula na wengine hulala fofofo na kuwa kama wamezimia na wengine hupiga kelele na hata kuimba au kutoa matusi ya nguoni na hii ni mwitikio wa kawaida kihisia kwa kufika kileleni.

Unapofika kileleni mwili hufanya majumuisho ya kuachia raha ya jumla na hii husukuma mwitikio wa tukuko (emotions/feelings) na kwako huo mwitikio ni kububujika machozi.

Pia ifahamike kwamba sex kati ya wawili wanaopendana ni suala la kumilikiana na kuingizana ndani ya kila mmoja kwenye nafsi ya mwenzake na wakati mwingine mwitikio unaotokea huwa nje ya ufahamu (unconscious level) wa hao wawili namna walivyounganishwa na matokeo yake mwanamke ambaye kwake suala la hisia huunganishwa na sex hujikuta akibubujikwa na machozi bila yeye mwenyewe kufahamu sababu halisi.

Jambo la msingi ni kwamba kama unajisikia raha na huku kuna kilio na machozi ni suala la mwenzako kuelewa kwamba ni mwitikio wa kazi yake nzuri ya kukufikisha pale unahitaji na si vinginevyo.

Haina haja kuwa na hofu kwani ni jambo la kawaida tu.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

3 comments:

Anonymous said...

hiyo nahisi ni kawaida...je kaka mbilinyi..inakuwaje pale watu wapo kwenye mahusihano ya miaka 2 bila sex lakini mwanaume ana mstimulate mchumba wake mpaka afike kileleni..lakin yeye mwanaume hajali ku-pees bora mchumba wake aridhike..je msichana ni selfish?na msichana atafanyaje kumridhisha mchumba wake mbali na sex maana bado hawajaoana na msichana anamsimamo.

Lazarus Mbilinyi said...

Asante kwa swali:

Duh, huyo mwanaume kiboko! anawezaje kumsisimua mchumba wake bila yeye kuingia majaribuni? Je, unaweza kuweka makaa ya moto kifuani na usiungue?

Huyo mwanaume rijali anawezaje kuvuka mipaka kiasi hicho na kila kitu kwake kikawa shwari? kazi kwelikweli!

Hako kamchezo kenu ka kusisimuana wakati hamjaona na kuwa commited kanaonekana kazuri ila mnaweza kujikuta ndoto ya ndoa imeota mabawa.
Unaomba ushauri namna ya kumridhisha mwanaume ambaye hajakuoa na utumie mbinu ipi?

Sina ushauri ila ukiolewa tu nitakwambia.

Ukipuuzia shauri yako maana siku ukijiona mjanja na ukaamua kumridhisha na mkawasha moto usiozimika unaweza kujikuta ndoto za kuolewa zimeyeyuka.
Kwa nini anunue ng'ombe kama maziwa atapana bure?

Kwa maelezo zaidi soma hapa http://mbilinyi.blogspot.com/2011/05/usicheze.html

Upendo daima

Anonymous said...

asante sana kaka mbilinyi kwa jibu zuri lililonyooka na lauwazi..kweli si vyema kujuana mwili kabla ya ndoa hata kwa hizo stimulation...shida inakuwa pale mkishaanza romance ni ngumu kuacha..kwa ushauri wako nitaufanyia kazi ndoa isijeota mabawa..asante na ubarikiwe sana.