"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, June 16, 2011

Wako ni wa aina gani?


Mara nyingi kuna usemi kwamba kwa mwanaume kawaida ana kitu kimoja tu ambacho kinaweza kumfanya apate hamu ya kufanya mapenzi nacho ni “kitu chochote”.
Najua hujanielewa ila Ukweli ni kwamba mwanaume ni tofauti sana na mwanamke linapokuja suala la kusisimka kimapenzi kwani mwanaume anaweza kusisimka (stimulated) hata pale tu mwanamke au mke wake akiwa nusu uchi, au uchi au hata kile kitendo cha kuvua nguo au akiwa amevaa kivazi chochote kinachoshawishi, wanawake hawapo hivyo.
Wanawake kila mmoja ni tofauti hata huyo mmoja (mke wako) yupo tofauti kila siku katika mwezi mmoja, mwaka na miaka.
Mwanaume unahitaji kuwa mbunifu kufahamu namna upepo wa hamu ya mapenzi unavyovuma kwa mke wako, kwani ukilemaa unaweza kuchanganya mambo na kupitwa na wakati.
Unahitaji kujifunza nini kinaweza au kwa sasa kunamsisimua mke wako kuwa tayari kukupa nafasi ya kufurahia tendo la ndoa.
Inawezekana mkeo ni aina ya wanawake ambao husisimka na kuwa tayari kimapenzi kwa kuguswa, kumbatiwa, shikwashikwa (caresses) yaani TOUCH GIRL!
Au Inawezekana mke wako ni aina ya wanawake ambao ukitaka apate hamu ya kuwa na wewe ni sharti uongee, umsifu, umtie moyo, uchonge sana maneno matamu yaani TELL ME GIRL.
Inawezekana yeye ni wale wa kuwashirikisha siri, au malengo au jambo lolote unafanya au waza ndipo afunguke kimapenzi yaani SHARE WITH ME GIRL.
Inawezekana mke wako ni walewale usipofanya kazi naye, usipomsaidia vikazi vidogo vidogo pale nyumbani, kupika chakula, kufunga net nk hawezi kujibu kimapenzi yaani DOING GIRL.
Inawezekana ni aina ya mwanamke ambaye ukitaka ufurahie mwili wake na moyo wake chumbani lazima mfanye maombi, au soma Neno (Biblia), au fanya ibada au ongea mambo ya kiroho yaaani SPIRITUAL GIRL.
nk
Je, wewe mwanaume unayesoma hapa unajua mke wako ni aina gani?

11 comments:

Abraham said...

Aisee unazidi kunifungua,ubarikiwe ndugu,kazi yako si bure.

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Abraham,

Nashukuru kwa wewe kupita hapa na kujifunza kitu kwani mahusiano au ndoa ni suala la kuendelea kujifunza kila siku maisha yote ya ndoa au mahusiano.

Ubarikiwe

Upendo daima

Anonymous said...

shalom kaka, nimerudi mdau mda mrefu nilikuwa bize, ila tupo pamoja, barikiwa kwa kazi yako njema

ms gbennett

Lazarus Mbilinyi said...

Ms Gbennett,

Nimefurahi kwamba upo mzima na nimefurahi kwamba tupo pamoja.

Upendo daima

Anonymous said...

kaka ndio hii topic iliyonigharimu
Eva

Anonymous said...

kaka ndio hii topic iliyonigharimu
Eva

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Eva,
Imekugharimu? umejifunza kiu gani kutokana na hilo?

Upendo daima

Anonymous said...

topic kama topic ni nzuri na haina tatizo,tatizo lipo kwenye uelewa,walokole sisi tukipita kusoma vitu kama hivi unaonekana wewe huna mungu,au hujaokoka,maana mi imefikia wakati naambiwa tangu lini changudoa akaokoka,means mimi changudoa, na hao hao wanasema hakuna lilalo mshinda mungu,sasa hapo ndio mkanganyiko unapokuja,mahusiaono kazi jamani

Anonymous said...

topic kama topic ni nzuri na haina tatizo,tatizo lipo kwenye uelewa,walokole sisi tukipita kusoma vitu kama hivi unaonekana wewe huna mungu,au hujaokoka,maana mi imefikia wakati naambiwa tangu lini changudoa akaokoka,means mimi changudoa, na hao hao wanasema hakuna lilalo mshinda mungu,sasa hapo ndio mkanganyiko unapokuja,mahusiaono kazi jamani

Lazarus Mbilinyi said...

Umenena kweli,
Tuliookoka hatujifunzi masuala ya ndoa zaidi ya masuala ya kiroho, matokeo yake hatukui na kutokukua kunafanya ndoa kukosa ladha.

Ubarikiwe

Anonymous said...

Duuuuuuuh kaka umepagusa hasa m mke wangu namshukuru mungu aisee before any thing we must thanx to God then ndio mambo mengine ila nakushukuru sana ndugu yangu na mungu azid kukupa uzima shule yako hahaha umenitoa tongotongo hakika asante