"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, July 30, 2011

Kukumbatiana

Binadamu ana muhitaji sita muhimu katika maisha nayo ni Hewa, Chakula, Maji, Mavazi, Malazi, Kukumbatiwa (hug)

Hugging ni asili, ni kitendo kinachotupa afya, hakina pesticide, wala preservatives zozote.

Kukumbatiana (hugging) ni sayansi, njia rahisi ya Kusaidiana, kuponya, kukua na ina kipimo cha ajabu katika matokeo yake.

Pia kukumbatiana ni sanaa, kukumbatiwa si tu ni vizuri bali pia ni hitaji, sayansi inathibitisha kwamba kukumbatiwa ni muhimu kwa maisha yetu kihisia, kimwili, kiroho na maisha yote kwa ujumla

Pia imehibitika kwamba hugging husaidia maendelea ya mtoto katika lugha na IQ yake.

Hugs ni tamu, huondoa upweke, huondoa hofu, hufungua milango kwa ajili ya feelings, hujenga mtu kuwa jasiri, hupunguza kuzeeka, kuongeza hamu ya chakula, husaidia kuweka mikono na mabega katika ubora zaidi pamoja na misuli yake, kama wewe mfupi basi hugs zinakufanya kazi nzuri kukunyosha vizuri na kama wewe ni mrefu basi hugs hukuwezesha kukupa zoezi la kujikunja na kujinyosha.

Kidemokrasia hugs zinamfaa mtu yeyote bila kufuata chama kama ni tawala au upinzani, zinamfaa maskini, tajiri, mweupe, mweusi, wanene, watoto, vijana, wazee, vikongwe, wafupi au warefu wote hugs zinawafaa.

Hug halina caffeine, nicotine wala calories na artificial ingredients asilimia mia moja ni kamilifu safi kabisa.

Hug ni halisi, kitu timamu ambacho hakina kitu chochote hatari haihitaji battery wala checkup ya kila siku, hata wakati wa hugging huhitaji nguvu bali ukipokea au kutoa hug unapata nguvu maradufu.

Hugs kiuchumi ni sound, hazina impact katika mazingira yetu ni environmentally friendly, hakuna global warming kwa kukumbatiana, hugs hazihitaji vifaa maalumu ni rahisi, huwezesha siku za furaha kuwa za furaha zaidi, hufanyi siku zisizowezekana kuwa siku zinazowezekana.

Huwezi kulipishwa kodi kwa hugging, huwezi kupata unene kwa hugging, huwezi kupata pollution kwa hugging, hakuna bills za hugging, wala hakuna inflation kwa hugging.

Hugging ni afya kwa mwili na roho, huponya msongo wa mawazo, kupunguza mawazo, huongeza uwezo wa kupata usingizi.

Huwezesha mwili kuwa na immunity ya kutosha kwa magonjwa, huhuisha maisha ya mtu bila side effect kama medications zingine

Hugging ni dawa yenye miujiza

Hugs ni free ndiyo maana wengi wanachukulia ni for granted, kama hugs zingekuwa zinauzwa kwenye maduka au stores au supermarkets, genge au grocery basi kwanza bei yake ingekuwa haishikiki na pia kila mtu angekimbilia kununua angalau japo apate moja kwa siku.

Hata kama hugs ni bure zisipotumika hazina thamani yoyote. Hugs zisizotumika hupotea milele

Katika dunia ambayo watu wana njaa ya kupendwa je, Ni vizuri kupoteza angalau hata hug moja?

Wanasayansi wamethibitisha kwamba:

Hugs 4 kwa siku ni hitaji la kila Binadamu kwa siku ili aishi.

Hugs 8 kwa siku huhitajika kwa ajili ya kuimarisha kiwango cha emotions.

Hugs 12 kwa siku ni muhimu kwa ajili ya kukua na kuwa mtu mwema na bora.

Hakuna kitu kinaitwa hugs mbaya, hugs zote ni nzuri.

Lazima ukumbatiane na mtu angalau kwa siku mara moja na kama kuna mvua angalau mara mbili kwa siku

Pia kumbatia huku unatabasamu, kufumba macho si lazima

Kukumbatiana wakati mnaenda kulala hufukuza ndoto mbaya

Usikumbatie kesho kama leo unaweza kukumbatiaThursday, July 28, 2011

Kwepa Kabisa

Wewe ambaye umeoa au kuolewa na upo unafikiria kuachana na mwenzi wako.

Fikiri upya uamuzi wako.
Fikiria hao watoto mlionao, Fikiria nyakati zote nzuri mlizokuwa nazo pamoja kama mke na mume, Fikiria sehemu tofauti ambazo mlitembelea pamoja, marafiki wazuri mliokuwa nao wote wawili kama mke na mume.
Iepuke talaka kwa gharama zote, sababu zinazokufanya uamue kuachana na huyo mume wako au mke wako zinaweza kuwa ndizo zitakazokuwa sababu mara nyingine tena mbele ya safari kama utaamua kuoa au kuolewa tena.
Sasa unaachana na James kwa kuwa umechoka na tabia zake za kulewa sana pombe, au kukutaka sex mara nne kwa siku na next time unaweza kujikuta unaachana na John kwa kuwa anakupiga mingumi usiku kucha na yeye sex kwa mwaka mara moja.
Inawezekana unataka kuachana na Jane kwa sababu ni msumbufu na anakusema hata kwa vitu vidogo, hata hivyo unaweza kujikuta unaacha na Joyce baadae kwa sababu si mwaminifu katika fedha.
Sasa utaishia wapi na hiyo project ya kuachana na kila unayeoana naye?
Ukiangalia kwa makini kinachobadilika ni tabia na mhusika tu ila wote ni binadamu na binadamu asiye na kasoro bado hajazaliwa hadi leo.


Maisha ni matamu sana kiasi cha kuyapoteza kwa kupeana talaka.
Wanaume wote duniani wanafanana pia wanawake wote duniani wanafanana , na sote ni binadamu.
Waingereza wanamsemo usemao "better the devil you know than the angle you don’t" tumia ubongo.
Wapo wanandoa ni wazembe kiasi ambacho huacha kutumia kila alichonacho kuhakikisha ndoa inarudi kwenye mstari, kukimbilia talaka si jibu bali ni kumsukuma tatizo mbele na matokeo yake utakuja kukutana nalo tena mbele ya safari.
Hata kama kuna mtu amekuahidi kwamba ukiachana na huyo uliyenaye basi yeye atakufanya uwe mtu mwenye furaha, hatakuumiza wala kukuacha, ni mwongo na anakudanganya kwani katoka sayari gani na binadamu gani.
Anaonekana anakufaa kwa kuwa huishi naye ukianza kuishi naye utajikuta umeruka mikojo na kukanyaga…………………………..


Jiulize mwenyewe upya.
Hivi kweli nimetumia uwezo kiasi gani kuhakikisha mwenzi wangu anajua namna tunahitaji kuirudisha ndoa yetu kwenye mapenzi upya kama tulivyoahidiana siku tunaoana?
Je, ni kweli nimefanya kila linalowezekana kusamehe na kusahau?
Je, ni kweli tunataka kuachana na kupeana talaka kwa sababu za msingi?
Kabla ya kuwasiliana na ndugu zako, rafiki zako, washauri wako, wanasheria au wachungaji wako Jaribu kukaa mwenyewe, na mwenzako kujadili upya na kwa upendo namna ya kutatua tatizo lenu na hakuna anayejua shida ya ndoa yako isipokuwa wewe na mwenzi wako.
Usifanye kwa haraka ukiamini unaingia kwenye uhuru.
Dawa ya kuachana au talaka ni kusamehe bila masharti.


Kwa maelezo zaidi soma click hapa chini
http://mbilinyi.blogspot.com/2010/05/si-rahisi-hivyo.html

Wednesday, July 27, 2011

Si kweli

ETI MNGEKUWA NA FEDHA ZA KUTOSHA BASI NDOA YENU ISINGEKUWA NA MATATIZO.

Fedha haziwezi kununua upendo wala furaha ya kweli.

Kama ni hivyo basi Prince Charles na Diana wasingetengana pamoja na kuwa na fedha za kutosha.

Lipo tatizo lingine la msingi ndiyo maana ndoa yenu hairidhishi.

ETI KWA SABABU ULIOANA NA MTU AMBAYE HAFANANI NA WEWE NDIYO MAANA MNA MATATIZO YA NDOA.

Ni kweli wanandoa kuoana huku wakifanana tabia ni moja ya suala la msingi katika kuifanya ndoa iwe imara, hata hivyo hii haina maana kwamba hamtakutana na matatizo katika ndoa yenu.

Matatizo ni kipimo kizuri cha Uimara wa ndoa yenu.

Matatizo, vikwazo, kupingana na hata kutoelewana kutakuwepo tu katika ndoa ila namna mnatatatua hayo mambo ndiyo ufunguo na msingi wa kuishi kwa raha au shida na mwenzi wako.

ETI NIMEINGIA KWENYE MATATIZO KATIKA NDOA HII KWA SABABU NIMEOANA NA HUYU MTU.

Ni uwongo uliotukuka!

Ni kweli Inawezekana huyo mtu wako anatatizo fulani pekee linalokupa shida hata hivyo hata mwingine unayedhani asingekuwa na tatizo naye ana matatizo yake mpya makubwa kuliko ya huyo uliyenaye, huoni matatizo yake kwa kuwa huishi naye.

Hakuna mtu ambaye hana matatizo duniani.

ETI TATIZO NI YEYE SIYO MIMI NDIYO MAANA NDOA INA MATATIZO

Umeamua kuwa jaji, hakimu na mwendesha mashitaka?

Nikupe homework?

Kama ni ndiyo, basi tafuta wanandoa 2 walioachana, muulize wa kwanza akupe sababu za kuachana. Jibu ni kwamba kila mmoja atamlaumu mwenzake.

Why?

Kwa sababu ndoa ni wawili na kila mmoja huchangia kuleta furaha au huzuni, kujenga au kubomoa period!

ETI NDOA YENYE FURAHA HAINA MIGONGANO KAMWE.

Huo ni uwongo mweupe!

Hata zile ndoa zenye furaha kuliko zote duniani hukumbana na matatizo na migogoro mara kwa mara.

Namna wanashughulikia matatizo na migogoro kwa upendo na pamoja ndicho hufanya ndoa zao kuwa imara na zinazoridhisha.

ETI KAMA NITAJIWEA BUBU BILA KUZUNGUMZA CHOCHOTE LINAPOTOKEA TATIZO BASI LITAYEYUKA LENYEWE

Unajidanganya!

Kula jiwe si suluhisho bali husababisha tatizo kubwa mlima ambao huwezi kupanda au shimo refu ambalo ukiingia kutoka huwezi.

ETI ILI KUEPUKA KUBISHANA NITAKUWA NAMJIBU NDIYO KWA KILA KITU

Ukweli hukipendi ndoa yako!

Kujibu ndiyo kwa kila kitu ili kuepuka kubishana unafanya mwenzako akuone mtu usiyewajibika na huna jipya na akili yako inapungua na badala ya kukua inadumaa na huna mchango katika ndoa.

ETI KWA KUWA TUMEOANA WOTE DINI MOJA, KABILA MOJA, MKOA MMOJA, RANGI MOJA NA ELIMU SAWA BASI HATUTAKUWA NA MATATIZO KATIKA NDOA

Kama umeoana na dini yake, kabila lake, mkoa wake, rangi yake na elimu yake basi matatizo hayatakuwepo ila kama umeoana na kiumbe kinaitwa mtu basi jiandae la sivyo utakuwa disappointed kama si kuwa frustrated.

Tuesday, July 12, 2011

Je, Nimuonjeshe?

Wakatazama movie hadi...........

Kaka Mbilinyi nashukuru kwa kutuelimisha kupitia blog yako ambayo kila mara napenda kuipitia ili kupata maarifa kimahusiano.

Nimepata mchumba na sasa tuna kama miezi 4 hivi, nimepanga kwamba suala la sex hadi baada ya kuoana yaani siku ya honeymoon, hata hivyo naona namna anaongea na anavyonitega kuna harufu ya kunitaka sex.

Nampenda na Sipendi nimuudhi je, sex kabla ya ndoa ina athari zozote?

Nisaidie!

Dada Jane (siyo jina halisi)

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Dada Jane asante kwa swali zuri ambalo huulizwa mara nyingi sana na akina dada.

Pia nashukuru sana kwa kupita hapa na kujifunza kwani mwenyewe najifunza kuliko ninyi wasomaji.

Pia hongera kwa kupata mchumba na zaidi ahadi yako ya kuhakikisha unamkabidhi kila kitu siku ya ndoa yenu na sivinginevyo.

Jibu sahihi ni kwamba sex kabla ya ndoa si sahihi na msimamo wa blog hii ni kwamba kabla ya ndoa sex ni dhambi na kuna athari kubwa sana zinazopelekea kutokuaminiana na zaidi kusababisha ndoa kuanza kufa mapema.

Sipendi kuhukumu na kuwa mzungumzaji sana kwenye issue muhimu na personal kama hiyo, hata hivyo naweza kukushauri uende kwa kiongozi wako wa dini na muulize kama atakukubalia sex kabla ya ndoa na akikubali urudi uniambie ili nami niongee naye.

Pia suala si sex tu bali soma hapa

+++++++++++++++++++++++++++++++++

Nikupe mfano wa kweli

Nancy (siyo jina halisi) ni dada ninayemfahamu anaishi Kimara Dar es salaam na alimpata mchumba James (siyo jina halisi) mwanaume wa miaka 40 naye anaishi Tegeta jijini Dar es salaam, wamekuwa wanaenda wote sehemu tofauti na kujiona ni kweli kuna kila dalili ya kuwa mke na mume.

Kwa kuwa Nancy ana miaka 36 kumpata James kwake ni kitu adimu na alijipanga tayari kuolewa kwani muda unaenda na nguvu ya uvutano ilishaanza kuvuta kwenda chini.

James alikuwa akimshawishi Nancy walale wote kitanda kimoja mara kwa mara na Nancy alikuwa anagoma na kumuahidi wasubiri hadi siku ya harusi.

Hata hivyo miezi miwili baadae, James alimualika Nancy kwenye sherehe ya rafiki zake huko Tegeta (jumapili) na sherehe zilichelewa kumalizika kitendo kilichopelekea James kuondoka na mchumba wake (Nancy) na kwenda naye kwake.

Walipofika kwake (James) walikaa kwenye sofa wakaweka movie wakaanza kuitazama na hatimaye Nancy akajikuta yupo kifuani kwa James.

Movie ikanoga, mara wakaanza kuwekeana miguu kila mmoja juu ya mwenzake, mara kushikana mikono, mara kukumbatiana, hatimaye kisses zikaanza, miguno ya raha ya mahaba ikaendelea kujikoleza, joto la mahaba likapanda na romance ikanoga na hatimaye wakajikuta wameingia ulimwengu mwingine wa kurusha kila nguo waliyovaa kusikujulikana, kilichoendelea Naamini unajua……

Asubuhi Nancy akajikuta kile amefanya si kile alipanga na akarudi kwao Kimara huku amejawa machozi na mawazo maana hata kupima walikuwa hawajaenda.

Siku iliyofuata ilikuwa Jumatatu Nancy akaamua kumpigia simu James na hakupokea na akaanza visababu.

James aliacha kumpigia simu Nancy na hata baada ya Nancy kulalamika na kuuliza kwa nini hapigi simu tofauti na nyuma kabla ya kupewa zabibu, James aliendelea kujibu utumbo kama si pumba.

Baada ya hapo James alipotea kabisa kwenye uso wa dunia na mbele ya macho ya Nancy kwa namna yoyote.

Kuona hivyo Nancy akaamua kupiga kiguu na njia hadi kwa James (Tegeta) na kwa kuwa hakutoa taarifa alichokikuta ni James yupo kifuani kwa mrembo mwingine.

Hadi hapo umenielewa dada Jane?

++++++++++++++++++++++++

Kwa asili wanaume huwa na respect ndogo sana kwa wanawake ambao wameshalala nao, so kama unataka ndoa kaa mbali na sex kabla ya ndoa.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

Kwa moyo wote!

Sababu za kuwa na migogoro kati ya mume na mke mara nyingi ni kwa sababu wanaume hawawaelewi kabisa wanawake (don’t understand) na wanawake wanawaelewa vibaya wanaume (misunderstand).

Kibaya zaidi wanaume mara zote huendelea kufanya kinyume na vile wanawake wanategemea wawafanyiwe na waume zao.

Na wanaume nao wanawashangaa wanawake namna wanavyobadilika kila mara kwani unaweza kumkuta mke dakika moja yupo na furaha na kicheko na baadae kidogo anajikunyata na kuhuzunika na wanaume huwaona wanawake ni viumbe wa ajabu sana chini ya jua.

Linapokuja suala la kutafuta mpenzi (mume mtarajiwa) wanawake wanatabia ya kumkubali na kumshika mwanaume mzima mzima. Na hutumia akili kuhakikisha anamnasa hata kwa kujipitisha sehemu au njia ambazo anaamini anaweza kukutana naye.

Kama anajua mwanaume yule hupatikana maeneo fulani na anampenda basi hujipeleka hilo eneo ili wakutane ili iwe coincidence fulani.

Atasubiri hako kanafasi ili wakutane ghafla.

Mwanamke hutumia njia ya hisia anapoingia kwenye suala la mapenzi na kuwa karibu na kifua chake (moyo) si mwonekano kama wanavyofanya wanaume.

Kawaida mwanaume huchelewa sana kufungua moyo kwa mwanaume na akishaufungua huufungua kwa asilimia 100 na akimpenda huyo mwanaume (fall in love) basi huwekeza kila kitu maishani mwake kwa ajili ya huyo mwanaume.

Soma hapa kujifunza zaidi

Wanawake huhitaji mwanaume ambaye atamhakikishia upendo na kwamba anapendwa kila siku, wanapenda kupokea sifa kwa mavazi, namna anaonekana na kila kitu, wanawake wapo sensitive sana katika issue za mapenzi na huumizwa kirahisi.

Wanawake wanapompata mwanaume wa kupendana naye huwekeza kwa muda mrefu na kwao mahusiano huwa na maana sana kama pumzi anayovuta.

Huwekeza katika kufahamu sifa za ndani za mwanaume kuliko uzuri wa sura ndiyo maana wanawake wengi wazuri kwa sura huishia kuona na wanaume wenye sura zinazofanana na chimpanzee (kidding)

Pia wanawake huwa wazi kimahusiano, kama kuna kitu kinamsumbua huongeza waziwazi tofauti na wanaume. Pia wanawake ni wazuri kusoma mwanaume akiwa na tatizo au kumshtukia kama kuna kitu kinaenda ndivyo sivyo.

Maelezo zaidi soma hapa

Mwanamke anapoongea na mpenzi wake hutegemea mume wake huyo kuacha kila kitu na kumsikiliza kwa makini.

Pia mwanamke hupenda kufanya kazi kama timu na ushirika ndiyo maana hata kama mume amempa rafiki yake pesa na akagundua bila kuambiwa kwake ni issue ingawa tatizo si zile fedha bali kwa nini hakuambiwa.

Pia wanawake hupenda surprise leo na kesho au mara kwa mara, hufurahia kufanyiwa vitu vidogovidogo kama vile mkienda restaurant mwanaume anachukua jukumu la kumuagizia chakula na kumletea ale (kuhudumiwa kama queen au princes)

Pia wanawake hupenda vitu tofauti tofauti kila eneo la kimwili (kama hujaelewa niulize).

Pia wanawake huwa hawapendi mwanaume kuongelea habari za mwanamke mwingine labda huyo mwanamke awe na sifa pungufu kuliko yeye kila idara.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

A woman in love, loves only one man!

Monday, July 11, 2011

Wanaposaka Huchemka

Wanaume, kama walivyotofauti na wanawake hufanya kitu kimoja kimoja (one track minded), kila wanachofanya huwa kimoja kwanza na huweza kuweka focus kwenye kitu kimoja anachofanya.

Kwa maelezo zaidi soma link ya hapa chini

http://mbilinyi.blogspot.com/2009/08/mwanaume-ni-box.html

Mwanaume anaweza kumualika mwanamke nyumbani kwake anachokiwaza ni sex, anaweza kumualika mwanamke kwa ajili ya lunch au supper anaweza kuwa na lengo moja tu kichwani mwake nacho ni sex, kama mwanamke atamtania huyu mwanaume, atakachofikiria na kuchukulia ni sex.

Kazi ni kwako!

Wanaume huwekeza kiasi kidogo sana kwenye bank ya mapenzi na cha ajabu huwekeza kidogo sana wakitegemea kuvuna vingi tena kwa muda mfupi. Mwanaume akimpenda mwanamke hata kwa muda mfupi huamini alichowekeza anaweza kuvuna mara mbili yake hata kwa wiki moja. Katika mapenzi wanaume huwekeza kwa malengo ya muda mfupi kuliko muda mrefu.

Ndivyo asili yao inavyowatuma ndiyo maana kwenye mahusiano mengi wanawake ndiyo huumizwa.

Linapokuja suala la mahusiano wanaume huangalia tu suala la mwonekano (physical attributes) za mwanamke kuliko kitu chochote kingine.

Mwanaume anaweza kumpenda mwanamke kwa sababu ya urembo wake na anaamini Mungu atamsaidia kujua mengine yaliyobaki kama vile tabia nk.

Wanaume hupenda kuongeza (control) kila eneo, hupenda kuiendesha gari bila kuelekezwa hata kama amepotea, hupenda kulipa bill hotelini hata kama ana fedha kidogo, hupenda kujieleza alivyo na mafanikio hata kama yupo kwenye wakati mgumu kimaisha.

Pia wanaume huchukua muda mrefu kujua makosa yako na hata wakijua mara nyingi huwa “too late to catch the bus”.

Pia wanaume huwa hawapendi kuomba msamaha na wapo tayari kuomba msamaha kiana kwa kuwanunulia wapenzi wao zawadi badala ya kukiri tu “nimekosa nimsamehe mpenzi wangu”

NAMNA WANAUME HUCHEMKA WAKATI WA KUSAKA MPENZI

Kwa kuwa wanapenda urembo, sura na mwonekano wa nje kwa mwanamke na huamini kwamba kwa kuwa huyu mwanamke (dada) ni beautiful lazima atakuwa na tabia njema, mwelewa, mvumilivu, amelelewa vizuri na mwema na wanajisahau kufahamu sifa za mwanamke ambaye anafaa kwa mahusiano (sifa na mitazamo ya mwanamke), matokeo yake wanaume huchanganya upendo na tamaa (love/lust). Matokeo yake hutumia muda wao na nguvu zao kusherehekea urembo wa mwanamke badala ya kuchunguza sifa za ndani ambazo pia kazi yake ili kufahamu ni ngumu au huchosha. Akili yake inamtuma kumpa kwanza huyo mrembo na baadae atafahamu tabia yake.

In dating game, men are usually disaster!

Unaweza kusoma hapa chini kwa maelezo zaidi

http://mbilinyi.blogspot.com/2010/04/ndivyo-walivyo.html

http://mbilinyi.blogspot.com/2010/05/mume-akupende.html

Tuesday, July 5, 2011

Tabasamu

Tabasamu ni njia rahisi isiyo na gharama ya kubadilisha mwonekano wako.
Tabasamu ni kitu gani?
Tabasamu ni dirisha linaloonesha nini kilichopo ndani ya moyo wa mtu, ni kitu kinachonyoosha kila kitu kuwa katika mstari ulioonyoka.
Ukiwa mtu wa kutabasamu unakuwa na marafiki wengi na ukiwa mtu wa ndita watu huanza kukukwepa.

Kila unapotabasamu kwa mtu yeyote ni ishara ya upendo, ni zawadi kwa yule mtu ni kitu kizuri.
Tabasamu ni kusema karibu, tabasamu ni uwezo ambao unaweza kuifanya siku ya giza kuwa siku ya nuru, huweza kufanya pasipo na upendo kuwa na upendo.
Inagharimu misuli 17 tu kutabasamu na inakugharimu misuli 43 kuwa na ndita kwa nini ujizeeshe mapema?
Amani huanza kwa tabasamu!

Huwezi kuvaa ukapendeza bila kuvaa tabasamu, huwezi kuwa mrembo bila kuvaa tabasamu huwezi kuitwa beautiful one kama hujavaa tabasamu huwezi kuitwa handsome kama hujavaa tabasamu period!
Tafiti zinaonesha mtu anayetabasamu huwezi kuongeza miaka mingi katika maisha yake.
Hata hivyo watoto hujifunza kutabasamu kutoka kwa wazazi wao.

Umemaliza kusoma hapa, sasa zamu yako kutabasamu then kicheko!

Ananivutia sana why?

Je, mwili hufaidi kitu gani unapojihusisha na mapenzi?
Mwili kawaida hutoa kiasi fulani cha kemikali ambazo hufanya ujisikie vizuri ukiwa kwenye mapenzi.
Hii husaidia wewe kuwa mbunifu unayeweza kuunda vitu vipya na ndiyo maana wasanii wengi au waandishi wa vitabu pia ni watu smart kwenye suala la mapenzi (siyo wote)
Mapenzi huweza kuzaa sex na sex huweza kubadilisha hali ya mwili kabisa kuanzia kwenye nywele kichwani hadi kwenye kucha za miguuni.
Wataalamu wanaeleza kwamba sex husaidia sana mwili.
Faida za sex katika mwili soma hapa

Kama mapenzi ni kemikali kati ya mwanaume na mwanamke inakuwaje tunavutiwa na mwanaume fulani au mwanamke fulani na si kila mmoja?
Kwa nini huwa hatuvutiwi na kila mtu ambaye tunakutana naye na kuna mwingine ukikutana naye anakuvutia kiasi cha kukuingiza majaribuni?

Watafiti wanasema kwamba kila mmoja mwili wake hutoa (release) aina fulani ya kemikali ambayo hata pua zetu haziwezi kunusa ila Ubongo huweza na Ubongo huweza kuchambua harufu ya kemikali tofauti na ya kwako kwa mwanamke au mwanaume mwingine hasa ile yenye kiwango kikubwa cha Immune na huvutiwa nayo ndiyo maana tunavutiwa na watu wachache sana na si wote.

Monday, July 4, 2011

Steve called a Doctor and said,  
Hello doctor, I want to be castrated."
 
"What on earth for?" asks the doctor in amazement 
"It's something I've been
thinking about for a long time and I want to have it done" replies Steve.
 
"But have you thought it through properly?" asks the doctor, "It's a very
serious operation and once it's done, there's no going back. It will change
your life forever!"
 
"I'm aware of that and you're not going to change my mind -- either you book
me in to be castrated or I'll simply go to another doctor."
 
"Well, OK.” says the doctor, "But it's against my better judgment!"
 
So Steve has his operation, and the next day he is up and walking very
slowly, legs apart, down the hospital corridor with his drip stand. Heading
towards him is another patient, who is walking exactly the same way.
 
"Hi there," says Steve, "It looks as if you've just had the same operation
as me."
 
"Well," said the patient, "I finally decided after 37 years of life that I
would like to be circumcised."
 
Steve stared at him in horror and screamed, "Shit! THAT'S the word!"
 
Enjoy Your Day!!!!

Wanawake nao...

Wanaume hukatishwa tamaa na wanawake kwa kuwa wanawake hawapendi sex na wanawake hukatishwa tamaa sana na wanaume kwa kuwa wanaume kila mara wanachotaka ni sex.

Wanawake hulaumu sana wanaume kwa kuwa hawajui kupenda (love) ni kitu gani.

Na wanaume huwalaumu sana wanawake kwa kuwa hupenda kuongelea sana upendo (love) lakini hawataki kufanyia kazi (vitendo).

Kwa maelezo zaidi soma hapa

Urefu wake....

Wanawake si rahisi kufahamu vipimo sahihi vya uke kwa kuwa si rahisi kupima, Inawezekana wewe ni mwanamke na unajua kwa kukisia vipimo vya uke wake kutokana na hekaheka za matumizi hata hivyo jambo la msingi ni kwamba kuta za uke ni elastic na si rahisi kujua vipimo halisi.

Je, vipimo sahihi vya uke wa mwanamke akiwa relaxed ni kiasi gani?

Mwanamke akiwa relaxed urefu wa uke ni wastani wa sentimita 8 na nusu hadi 10

Wakati kipenyo ni chini ya sentimita 3

Akiwa amesisimka uke hupanuka na kuwa kati ya sentimita 13 hadi 15.

Wakati kipenyo huwa sentimita 3 hadi 6.

Na wakati anapojifungua mtoto uke hufika urefu wa sentimita 20 hadi 23 na kipenyo huwa kati ya sentimita 3 hadi 5.

Wanawake wengi wanaamini kwamba wakiwa na uke unaobana husaidia kuleta raha kwa mume na mke wakati wa sex, kuna Ukweli ndani yake kwani namna uke unavyozidi kubana maana yake ni raha zaidi na msuguano zaidi.

Na kwa kweli uke ambao unapwaya husababisha dhiki kuu katika sex.

Hata hivyo swali la msingi kujiuliza ni je, ni kiasi gani tutasema uke unapwaya?

Uke hutofautiana katika vipimo kila wakati, mwanamke anapokuwa relaxed kuta za uke huweza kukutana hata hivyo vipimo huanza kubadilika wakati mwanamke anakuwa amesisimka na kuwa tayari kwa sex.

Kipenyo huwa kidogo mwanzo wa uke (opening) na huendelea kupanuka unavyoingia ndani.

Mara nyingi uke hubadilisha vipimo hasa baada ya mwanamke kujifungua kutokana na kutanuka kwa uke wakati wa kuzaa mtoto na wanawake wengi hulalamika kwamba wanajisikia wanapwaya na hata kushindwa kuthibiti kibofu cha mkojo baada ya kuzaa.

Njia sahihi ni kufanya zoezi la kukaza misuli Kegel au surgery ya kukaza uke.

Je kuna sababu ya mwanamke kuhofia mwanaume alinayebarikiwa kuwa na uume mrefu au mpana?

Haina haja kwa sababu kwa sababu namna uke unaweza kupanuka basi huweza kufanya accommodation ya size yoyote ya uume.

Ndiyo maana mtoto huweza kupita wakati wa kuzaliwa.

Kimahesabu asimilia 60 ya wanawake duniani wana size ya wastani, asilimia 10 size ndogo na asilimia 30 ni size kubwa, sijajua wewe upo kundi gani.


Pia hii ni kukutahadharisha kwamba kama una size kubwa ya uke unaweza kukumbana na matatizo yafuatayo.

Kwanza ni huwezi kupata raha na kuridhishwa vizuri na partner wako wakati wa sex kwa kuwa unapwaya yaani hakuna msuguano.

Pili hewa huweza kuingiza wakati wa sex na kuanza kutoa mlio unaoweza kupunguza kujiamini na raha ya mapenzi pia unaweza kuwa na matatizo ya kubana mkojo.

Njia sahihi ya kuimarisha size ya uke ni mazoezi ya kegel.

Je, Nirudi yule wa Zamani?

SWALI:

Mimi ni mwanamke ambaye nipo kwenye ndoa sasa ni mwaka wa pili na nusu na tayari mahusiano yangu na mume wangu naona hayana mapenzi na linapokuja suala la sex ni kama tumechokana hakuna jipya.

Kabla ya huyu mume wangu kunioa Nilikuwa na rafiki wa kiume ambaye niliamini tungeoana ila aliniacha kwa sababu ya mwanamke mwingine na sasa wameachana yupo mwenyewe na wiki mbili zilizopita nilikutana naye na tukapata lunch pamoja na akanieleza kwamba anasikitika sana kwa yale yalitokea na kwamba hajaona mwanamke kama mimi ambaye anaweza kujaza nafasi ndani ya moyo wake na kwamba anaomba nimsamehe kwa yale alifanya.

Aliniambia sasa ninapendeza sana na nikajiona kweli ninampenda kiasi cha kutaka nirudiane naye na kuachana na huyu niliyenaye.

Je, nibaki na huyu wa sasa au nirudi kwa yule wa zamani?

MAJIBU

Kwanza karibu sana kwenye maisha ya ndoa, ukifika kwenye ndoa lazima ufahamu kwamba sasa vipepeo hakuna na hicho kimoja umekishika hutakiwi kuuliza kama ni chenyewe au la, hiyo ndiyo habari njema.

Ndoa ni kazi kwa maana kwamba lazima kila siku ufanye kitu kuchangia, ndoa ni kujitoa na lazima ujiulize nimechangia kiasi gani kuhakikisha tunakuwa na moto wa mapenzi ninaohitaji.

Suala si mume wako tu bali na wewe umefanya kitu gani kuhakikisha kunakuwa na mapenzi motomoto.

Hapa ni 50 kwa 50, wewe 50% na mume wako 50% na kunapotokea tatizo lolote wewe unatakiwa kuchangia 100 kwa 100 kutafuta suluhisho.

Kwa namna yoyote hutakiwa kumlaumu mume wako peke yake kwa kuwa ndoa yenu haina mapenzi tena na kujiona mmechokana,

Hata kama unaona mmechokana kimapenzi bado ndani yako kuna upendo ambao ukiamua kuelekeza nguvu zako penzi litafufuka.

Upendo si feelings za muda bali ni kuwa na mtu ambaye anabaki ndani ya moyo wako maisha yote hata baada ya kujua tabia zake na namna alivyo kwani upendo huvumilia, hauoni mabaya (1Wakorintho 13)

Feelings ulizonazo kwa rafiki yako wa zamani si kitu halisi, jiulize kama aliweza kukuacha kwa ajili ya mwanamke mwingine je alikuwa anakujali kweli, je alikuwa anakupenda kweli, hakujua anakuumiza? Mume wako hastahili kuumizwa kama unavyotaka kufanya.

Jitahidi kuhakikisha ndoa ina work, weka efforts, ongea na mume wako namna unajisikia na vile unapenda mambo yawe.

Jitoe usiku na mchana kuhakikisha kila kitu kinarudi kwenye mstari.

Huyo mwanaume wako wa zamani anaonekana kama anakupenda na wewe unajiona kweli unampenda kwa sababu nyumbani kwako hujisikii vizuri na huo ni ugonjwa.

Kwa nini usitafute siku wewe na mume wako mkapata muda wa kwenda mbali kabisa na mazingira ya kila siku mkakaa na kuongea na wewe mwenyewe jiweke mrembo na weka akilini kile ulikiona kwa mume wako siku za mwanzo wakati mnapendana, mpe upendo mume wako hadi uishe wote uone kama mambo hayatabadilika.

Mwanaume wako wa zamani anaonekana ni jibu la matatizo yako kwa sasa kwa sababu upo bored na huishi naye.

Kurudi kwa mwanaume wako huyo ni wazo potofu na zaidi ni kutaka kupata disappointment zingine na frustration kubwa katika maisha na unataka kuharibu maisha zaidi.

Unatakiwa kuwa mkweli na mume wako.

Jenga ndoa yenu kwa upendo na ushirikiano.