"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, July 1, 2011

Hata Sms!

Maisha yanaweza kuwa magumu na mahusiano (ndoa) yanaweza kuwa magumu pia.

Na pia kuishi na mtu mwingine siku hadi siku wakati mwingine huwa ni dhiki kuu (tribulation) hasa kama unafanya yafuatayo au unafanyiwa yafuatayo na kwa kuwa unasoma sasa hivi hapa basi ni vizuri kuepuka.

KUSHTUKIZA (surprise)

Kuna wakati kushtukiza huleta raha pale tu kama ni surprise ya manufaa kama vile kwenda outing siku za weekend au kuletewa zawadi ya chocolate nyumbani au kazini.

Hata hivyo kuna surprise zingine ni kutafuta maneno kwani mama yako amekwambia anakuja nyumbani na wewe hujamwambia mke wako au mume wako na hujamwambia kwamba atakaa wiki 3 hadi siku anaingia mlangoni. Au kwamba umemualika bosi wako nyumbani kwa ajili ya dinner bila kumwambia mke wako au mume wako.

KUTOA TAARIFA

Kama utachelewa kurudi nyumbani ni muhimu kutoa taarifa (piga simu au tuma sms). Katika zama za leo ambapo kila mtu ana simu ya mkononi na unaweza kupiga simu mahali popote kutoa taarifa, hakuna excuse tabia hii inaudhi.

Pia kutokana na kupanda kwa kiwango cha uhalifu mwenzio wako ukichelewa bila taarifa unampa homa.

Zaidi ni kukosa adabu kwa kutoheshima mwenzako ambaye anakubiri nyumbani bila wewe kutoa taarifa.

UBINAFSI:

Ni kweli si kila maamuzi lazima wote mshirikiane, hata hivyo kuna maamuzi mazito ambayo huweza kuathiri wote ni muhimu sana kushirikiana (shauriana kwanza) kabla ya kutoa uamuzi.

Huwezi ukaamua kuuza nyumba bila kumwambia mke au mume wako au huwezi kuruhusu mtu wa familia nyingine kuja kuishi na ninyi bila kumwambie mwenzi wako nk.

KUWA MKOROFI

Hii ni pamoja na kuwa mkali wa maneno kupindukia (matusi hata ya nguoni), kumdhalilisha mwenzi wako kimapenzi, kimwili au hata kuwa na wivu wa kupindukia, pia kuwa makini na namna unaongea na mke au mume wako mbele za watu. Pia kuwa mkali wa mwenzi wako inaonesha hajiamini na mwanandoa kuwa abusive si tabia za kindoa. Na hakuna mwanandoa anaweza kuvumilia pia ni hatari kwa watoto wanawaona mkikorofishana kila leo.

KUWA BUBU

Kuna wakati ni jambo zuri kubaki kimya baada ya kupandwa na hasara ili usije toa neno ambalo Linaweza kuwasha moto na kuua ndoa. Hata hivyo kumuadhibu mwenzi wako kwa kujibakia bubu kwa siku kadhaa ni hatari kwa mwenzi wako.

Kujifanya bubu kuzidisha matatizo ya kuchelewa kufikia majibu kwa migongano uliokuwepo.

MAMLAKA

Inategemea, kama mke wako au mume wako anapiga watoto bila sababu za msingi Utakuwa mjinga kama hutaingilia, hata hivyo kama mwenzi wako anawaambia watoto kwanza wale chakula cha usiku ndipo wanywe soda zao na si kabla ya chakula na wewe ukamzunguka na kwenda kuwapa hapo umechemsha kwani ninyi wawili lazima muwe kitu kimoja (united front) kwa watoto wenu.

Kumbuka Ndoa ni ushirikiano na si vita ya kufa mtu ili mmoja atawale. Kama unatumia pesa au sex kumthibiti mke wako au mume wako upo katika njia inayokupelea kwenye shimo.

5 comments:

Anonymous said...

kuhusu suala la kuwa bubu kaka kuna wanawake wengine co waelewa sijui? kwani unakuta kuna mambo madogomadogo inatakiwa myazungumze nyie wenyewe ndani myamalize. lakini utakuta ukianzisha mazungumzo ambayo lengo ni kuweka mambo sawa, inakuwa kama vile umemwagia petrol kwenye moto. mnaanza vizuri lakini katikati tofauti zinatokea tena hapohapo. WAKATI MWINGINE INAKATISHA TAMAA. P.A.M

Lazarus Mbilinyi said...

Hello P.A.M,

Ukweli ni kwamba kila ndoa ipo tofauti na kila mwanamke au mwanaume ni tofauti. Jambo kubwa zaidi ni kwamba wenzetu wanawake wapo tofauti zaidi kwa kuwa anaweza kubadilika namna ana respond mazungumzo kutokana na siku katika mwezi. Hivyo ni jukumu lako mwanaume kwanza kufahamu mke wako ni mtu wa aina gani na yupo wakati gani na wewe utumie njia gani ya kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri kwani ndoa ni kujifunza kila siku na kuwa mbunifu na zaidi upendo.

Kama unahisi mkeo hata kitu kidogo tu anawaka basi ni vizuri kufahamu namna ya kuishi naye kwa namna ambayo wewe unaona itafanya kazi vizuri na zaidi kuongeza upendo katika mahusiano yako.

Upendo daima

Anonymous said...

wanaume wamezidi kuwa madikteta katika mahusiano,huna raha,ukitaka muelewane basi wewe uwe upo chini ya miguu yake kila siku,hata raha ya mahisiano hakuna,jamani huu mi naona ni unyanyasaji sana

Anonymous said...

Asante bwana kaka. ni kweli mke wangu ni mtu wa hasira hata kwa kitu kidogo hata kama amechoka, huwa anakasirika. ndivyo alivyo kwani hata mama yake mzazi alishanieleza kwamba ndo tatizo lake. ila ikitokea amenikasirikia bila sababu, au hata kama kuna sababu, kwa baadae mambo hukaa sawa na wakati mwingine huwa hujuta. asante sana kaka kwa ushauri wako, kwani mara nyingi hunisaidia kwenye ndoa yangu kwa kiasi kikubwa. ubarikiwe na mungu akuongezee kipaji zaidi.by P.A.M.

Anonymous said...

Wanaume wengi ni wabinafsi.