"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, July 2, 2011

Hata Ukirukaruka!

Kuna njia nyingi sana za uzazi wa mpango ambazo huweza kuzuia mimba. Pia kuna imani potofu nyingi kama si kukosa uelewa halisi wa namna ya kujikinga ili mwanamke asipate mimba na pia zipo njia ambazo watu hutumia na haziwezi kufanya kazi kamwe ya kuzuia mimba.

Tuangalie baadhi ya imani potofu ambazo watu hutumia wakiamini wanaweza kuzui mimba kumbe ni kujidanganya mchana kweupe.

NANYONYESHA HIVYO SIWEZI KUPATA MIMBA:

Ingawa mwanamke anaponyonyesha anaahirisha (postpone) uwezekano wa kupata mimba, hii isikufanye ulemae. Unaweza kupata mimba hata kama unanyonyesha hivyo ni vizuri kutumia njia sahihi za kuzuia mimba.

MWANAMKE HAWEZI KUPATA MIMBA KAMA HAJAFIKA KILELENI:

Ufike kileleni au usifike, mwanaume akitoa sperms na zikafika kwenye yai mimba inaingia. Hata kama mwanaume atafika kileleni ili kutoa sperms kwa mwanamke haihitaji kufika kileleni ili kupata mimba.

SIWEZI KUPATA MIMBA KAMA NITAJIOSHA (DOUCHING)

Baada ya mwanaume kumwaga sperms ndani ya uke si rahisi kuziondoa kwa maji kwani huwa zimefika kwenye cervix na huko hakuna kinaweza kuzuia usipate mimba.

SIHITAJI KUJIKINGA KWA KUWA NIPO SIKU SALAMA.

Kuna wakati homoni zinazohusika na mzunguko wa siku huweza kubadilika kutokana na umri au dawa mwanamke anatumia au stress na hivyo ni vigumu kujua siku salama ni ipi.

SIWEZI KUPATA MIMBA KAMA TUNAFANYA MAPENZI HUKU TUMESIMAMA AU MWANAUME YUPO CHINI MIMI MWANAMKE JUU.

Unajidanganya, hata kama upo juu ya mwanaume sperms zinao uwezo wa kupanda mlima wowote kwa speed ya ajabu maana zinajua kile zinakitafuta yaani mimba.

Naturally, hata kama ni wima au juu sperms zina namna yake ya kwenda bila tatizo na kufanya kila kinastahili, mimba.

NAWEZA TUMIA BALLOON AU MFUKO WA PLACTIC KAMA SINA CONDOM.

Condom ni tofauti na plastic bag au balloon, kwanza haviwezi ku-fit vizuri na vinaweza kupasuka muda wowote.

Pia condom zimekuwa tested kwa ajili ya kufanya kazi tofauti na mchezo wa kijinga unaofanya.

SIWEZI KUPATA MIMBA KAMA MWANAUME ATATOA KABLA YA KUMWAGA MBEGU.

Si njia sahihi kwani hata kabla ya kuingiza kuna kiasi fulani cha sperms huwa tayari zimeingia na zaidi kuna wanaume ambao uwezo wa kutoa hana na hata akitoa (withdrawal) anakuwa tayari alishamaliza habari.

Kazi kwako!

SIWEZI KUPATA MIMBA KWA KUWA NI SIKU YANGU YA KWANZA KULALA NA MWANAUME:

Haijalishi ni siku ya kwanza au la kama ni siku ambayo unaweza kupata mimba basi mimba itapatikana tu.

SIWEZI KUPATA MIMBA KAMA NITAENDA HAJA NDOGO BAADA YA SEX

Kwenda kukojoa hakuwezi kuondoa sperms ambazo zimesha enda kwenye uterus.

BAADA YA SEX NIKIRUKARUKA SIWEZI KUPATA MIMBA

Ruka tu kadri ya unavyoweza kama ni mimba itakuwa imeingia tu kwani kuruka juu baada ya sex hakuzuii kupata mimba bali zoezi tu la kawaida la kupunguza uzito na kujiweka fiti.

5 comments:

Anonymous said...

SASA NI NJIA GANI YAFAA KUZUIA MIMBA? TUTASHUKURU KAMA UTANIELEZA NJIA AMBAZO NI SAHIHI NA SALAMA KWA KUZUIA MIMBA. MIMI NA MKE WANGU TUNATUMIA KALENDA NA SASA NI MWAKA MMOJA TANGU AJIFUNGUE NA TUMETUMIA NJIA HIYO BILA MIMBA. HUWA NAHESABU KUANZIA SIKU ALIYOONA DAMU MPAKA SIKU YA KUMI KAMA SIKU SALAMA. KUANZIA SIKU YA KUMI MPAKA 20 NI SIKU HATARI. SIKU YA 20 HADI HEDHI NYINGINE NI SALAMA. TUPO SAHIHI? paulakwilini@gmail.comKURU KAMA UTANIELEZA NJIA AMBAZO NI SAHIHI NA SALAMA KWA KUZUIA MIMBA. MIMI NA MKE WANGU TUNATUMIA KALENDA NA SASA NI MWAKA MMOJA TANGU AJIFUNGUE NA TUMETUMIA NJIA HIYO BILA MIMBA. HUWA NAHESABU KUANZIA SIKU ALIYOONA DAMU MPAKA SIKU YA KUMI KAMA SIKU SALAMA. KUANZIA SIKU YA KUMI MPAKA 20 NI SIKU HATARI. SIKU YA 20 HADI HEDHI NYINGINE NI SALAMA. TUPO SAHIHI? paulakwilini@gmail.com

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka,

Asante kwa maoni mazuri, basi nitajitahidi kuelezea njia mbalimbali ambazo zinaweza kuzuia mimba kwenye makala zinazofutata.

God bless u

Anonymous said...

teh teh teh,nimecheka sasa kaka una mashushu mbaya,eve hapa

Rik Kilasi said...

hahahha hapa umesema ukweli kuna watu wanafikiria hivyo eti akiosha,kuruka ruka basi nimecheka hio kuruka ruka unajiweka fit hahahhaha

Jack said...

Haya mawazo potofu tunakuwa nayo baada ya kushauriwa vibaya juu ya kuzuia mimba.Tunahitaji elimu sahihi.By Jb Haliye