"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, July 12, 2011

Je, Nimuonjeshe?

Wakatazama movie hadi...........

Kaka Mbilinyi nashukuru kwa kutuelimisha kupitia blog yako ambayo kila mara napenda kuipitia ili kupata maarifa kimahusiano.

Nimepata mchumba na sasa tuna kama miezi 4 hivi, nimepanga kwamba suala la sex hadi baada ya kuoana yaani siku ya honeymoon, hata hivyo naona namna anaongea na anavyonitega kuna harufu ya kunitaka sex.

Nampenda na Sipendi nimuudhi je, sex kabla ya ndoa ina athari zozote?

Nisaidie!

Dada Jane (siyo jina halisi)

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Dada Jane asante kwa swali zuri ambalo huulizwa mara nyingi sana na akina dada.

Pia nashukuru sana kwa kupita hapa na kujifunza kwani mwenyewe najifunza kuliko ninyi wasomaji.

Pia hongera kwa kupata mchumba na zaidi ahadi yako ya kuhakikisha unamkabidhi kila kitu siku ya ndoa yenu na sivinginevyo.

Jibu sahihi ni kwamba sex kabla ya ndoa si sahihi na msimamo wa blog hii ni kwamba kabla ya ndoa sex ni dhambi na kuna athari kubwa sana zinazopelekea kutokuaminiana na zaidi kusababisha ndoa kuanza kufa mapema.

Sipendi kuhukumu na kuwa mzungumzaji sana kwenye issue muhimu na personal kama hiyo, hata hivyo naweza kukushauri uende kwa kiongozi wako wa dini na muulize kama atakukubalia sex kabla ya ndoa na akikubali urudi uniambie ili nami niongee naye.

Pia suala si sex tu bali soma hapa

+++++++++++++++++++++++++++++++++

Nikupe mfano wa kweli

Nancy (siyo jina halisi) ni dada ninayemfahamu anaishi Kimara Dar es salaam na alimpata mchumba James (siyo jina halisi) mwanaume wa miaka 40 naye anaishi Tegeta jijini Dar es salaam, wamekuwa wanaenda wote sehemu tofauti na kujiona ni kweli kuna kila dalili ya kuwa mke na mume.

Kwa kuwa Nancy ana miaka 36 kumpata James kwake ni kitu adimu na alijipanga tayari kuolewa kwani muda unaenda na nguvu ya uvutano ilishaanza kuvuta kwenda chini.

James alikuwa akimshawishi Nancy walale wote kitanda kimoja mara kwa mara na Nancy alikuwa anagoma na kumuahidi wasubiri hadi siku ya harusi.

Hata hivyo miezi miwili baadae, James alimualika Nancy kwenye sherehe ya rafiki zake huko Tegeta (jumapili) na sherehe zilichelewa kumalizika kitendo kilichopelekea James kuondoka na mchumba wake (Nancy) na kwenda naye kwake.

Walipofika kwake (James) walikaa kwenye sofa wakaweka movie wakaanza kuitazama na hatimaye Nancy akajikuta yupo kifuani kwa James.

Movie ikanoga, mara wakaanza kuwekeana miguu kila mmoja juu ya mwenzake, mara kushikana mikono, mara kukumbatiana, hatimaye kisses zikaanza, miguno ya raha ya mahaba ikaendelea kujikoleza, joto la mahaba likapanda na romance ikanoga na hatimaye wakajikuta wameingia ulimwengu mwingine wa kurusha kila nguo waliyovaa kusikujulikana, kilichoendelea Naamini unajua……

Asubuhi Nancy akajikuta kile amefanya si kile alipanga na akarudi kwao Kimara huku amejawa machozi na mawazo maana hata kupima walikuwa hawajaenda.

Siku iliyofuata ilikuwa Jumatatu Nancy akaamua kumpigia simu James na hakupokea na akaanza visababu.

James aliacha kumpigia simu Nancy na hata baada ya Nancy kulalamika na kuuliza kwa nini hapigi simu tofauti na nyuma kabla ya kupewa zabibu, James aliendelea kujibu utumbo kama si pumba.

Baada ya hapo James alipotea kabisa kwenye uso wa dunia na mbele ya macho ya Nancy kwa namna yoyote.

Kuona hivyo Nancy akaamua kupiga kiguu na njia hadi kwa James (Tegeta) na kwa kuwa hakutoa taarifa alichokikuta ni James yupo kifuani kwa mrembo mwingine.

Hadi hapo umenielewa dada Jane?

++++++++++++++++++++++++

Kwa asili wanaume huwa na respect ndogo sana kwa wanawake ambao wameshalala nao, so kama unataka ndoa kaa mbali na sex kabla ya ndoa.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

5 comments:

Anonymous said...

Miezi minne mbona haraka hivyo? Ungesema miaka ningekuelewa. Minne mmeshakua wachuma au ni rafiki tu huyo?
Unajua lugha yetu kutokua na neno la girl friend kwa vile miaka ile ilikua hamna hilo la watu kufahamiana kabla ya kwenda kwenye level ya uchumba. Enzi zile ilikua unachaguliwa mke/mume that was it..Sasa hivi itabidi watafutte neno la watu wakiwa kwenye relationship kabla ya kwenda kwa uchumba...
Mchumba ni yule aliyekuvalisha pete kama huna pete yake huyo sio mchumba, na pia kama hmvai pete basi mchumba ni yule aliyekuwaambia wazazi wako kuwa nataka kukuoa. Miezi minne kuanza kufikiria mambo ya sex kwa mwanaume sio big deal lakini kwa mwanamke use your brain. Kama anakupenda kweli atakuelewa kama hakupendi hata ukimpa haitakua njia ya kutomkasirisha. Atakuja na lingine.

Kabla ya yote nendeni mkapime. Utajuaje miezi mitano iliyopita alikua na nani? Love yourself gal and show a little dignity...

emu-three said...

Ujumbe mzurii sana mkuu, kuonjana kabla ya ndoa sio kuzuri, kwani hadhi ya mwanadamuu na `whatever' ipo pale pale, ni kama nyama madukani, ni ile ile, kinachotakiwa nai mapishi tu
Jambo jema fungeni ndoa halafu muanze mambo, na huko mtafundishana , mtaelewana tu...!

Lazarus Mbilinyi said...

Emu-Three,

Una Busara sana na ujumbe umefika.

Upendo daima

Anonymous said...

I just added your website on my blogroll. Really enjoyed reading through. Excellent information!

Anonymous said...

Really great article with very interesting information. You might want to follow up to this topic!?! 2011