"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, July 4, 2011

Je, Nirudi yule wa Zamani?

SWALI:

Mimi ni mwanamke ambaye nipo kwenye ndoa sasa ni mwaka wa pili na nusu na tayari mahusiano yangu na mume wangu naona hayana mapenzi na linapokuja suala la sex ni kama tumechokana hakuna jipya.

Kabla ya huyu mume wangu kunioa Nilikuwa na rafiki wa kiume ambaye niliamini tungeoana ila aliniacha kwa sababu ya mwanamke mwingine na sasa wameachana yupo mwenyewe na wiki mbili zilizopita nilikutana naye na tukapata lunch pamoja na akanieleza kwamba anasikitika sana kwa yale yalitokea na kwamba hajaona mwanamke kama mimi ambaye anaweza kujaza nafasi ndani ya moyo wake na kwamba anaomba nimsamehe kwa yale alifanya.

Aliniambia sasa ninapendeza sana na nikajiona kweli ninampenda kiasi cha kutaka nirudiane naye na kuachana na huyu niliyenaye.

Je, nibaki na huyu wa sasa au nirudi kwa yule wa zamani?

MAJIBU

Kwanza karibu sana kwenye maisha ya ndoa, ukifika kwenye ndoa lazima ufahamu kwamba sasa vipepeo hakuna na hicho kimoja umekishika hutakiwi kuuliza kama ni chenyewe au la, hiyo ndiyo habari njema.

Ndoa ni kazi kwa maana kwamba lazima kila siku ufanye kitu kuchangia, ndoa ni kujitoa na lazima ujiulize nimechangia kiasi gani kuhakikisha tunakuwa na moto wa mapenzi ninaohitaji.

Suala si mume wako tu bali na wewe umefanya kitu gani kuhakikisha kunakuwa na mapenzi motomoto.

Hapa ni 50 kwa 50, wewe 50% na mume wako 50% na kunapotokea tatizo lolote wewe unatakiwa kuchangia 100 kwa 100 kutafuta suluhisho.

Kwa namna yoyote hutakiwa kumlaumu mume wako peke yake kwa kuwa ndoa yenu haina mapenzi tena na kujiona mmechokana,

Hata kama unaona mmechokana kimapenzi bado ndani yako kuna upendo ambao ukiamua kuelekeza nguvu zako penzi litafufuka.

Upendo si feelings za muda bali ni kuwa na mtu ambaye anabaki ndani ya moyo wako maisha yote hata baada ya kujua tabia zake na namna alivyo kwani upendo huvumilia, hauoni mabaya (1Wakorintho 13)

Feelings ulizonazo kwa rafiki yako wa zamani si kitu halisi, jiulize kama aliweza kukuacha kwa ajili ya mwanamke mwingine je alikuwa anakujali kweli, je alikuwa anakupenda kweli, hakujua anakuumiza? Mume wako hastahili kuumizwa kama unavyotaka kufanya.

Jitahidi kuhakikisha ndoa ina work, weka efforts, ongea na mume wako namna unajisikia na vile unapenda mambo yawe.

Jitoe usiku na mchana kuhakikisha kila kitu kinarudi kwenye mstari.

Huyo mwanaume wako wa zamani anaonekana kama anakupenda na wewe unajiona kweli unampenda kwa sababu nyumbani kwako hujisikii vizuri na huo ni ugonjwa.

Kwa nini usitafute siku wewe na mume wako mkapata muda wa kwenda mbali kabisa na mazingira ya kila siku mkakaa na kuongea na wewe mwenyewe jiweke mrembo na weka akilini kile ulikiona kwa mume wako siku za mwanzo wakati mnapendana, mpe upendo mume wako hadi uishe wote uone kama mambo hayatabadilika.

Mwanaume wako wa zamani anaonekana ni jibu la matatizo yako kwa sasa kwa sababu upo bored na huishi naye.

Kurudi kwa mwanaume wako huyo ni wazo potofu na zaidi ni kutaka kupata disappointment zingine na frustration kubwa katika maisha na unataka kuharibu maisha zaidi.

Unatakiwa kuwa mkweli na mume wako.

Jenga ndoa yenu kwa upendo na ushirikiano.

1 comment:

Rik Kilasi said...

kazi nzuri kaka hongera ujumbe safi sana.