"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, July 30, 2011

Kukumbatiana

Binadamu ana muhitaji sita muhimu katika maisha nayo ni Hewa, Chakula, Maji, Mavazi, Malazi, Kukumbatiwa (hug)

Hugging ni asili, ni kitendo kinachotupa afya, hakina pesticide, wala preservatives zozote.

Kukumbatiana (hugging) ni sayansi, njia rahisi ya Kusaidiana, kuponya, kukua na ina kipimo cha ajabu katika matokeo yake.

Pia kukumbatiana ni sanaa, kukumbatiwa si tu ni vizuri bali pia ni hitaji, sayansi inathibitisha kwamba kukumbatiwa ni muhimu kwa maisha yetu kihisia, kimwili, kiroho na maisha yote kwa ujumla

Pia imehibitika kwamba hugging husaidia maendelea ya mtoto katika lugha na IQ yake.

Hugs ni tamu, huondoa upweke, huondoa hofu, hufungua milango kwa ajili ya feelings, hujenga mtu kuwa jasiri, hupunguza kuzeeka, kuongeza hamu ya chakula, husaidia kuweka mikono na mabega katika ubora zaidi pamoja na misuli yake, kama wewe mfupi basi hugs zinakufanya kazi nzuri kukunyosha vizuri na kama wewe ni mrefu basi hugs hukuwezesha kukupa zoezi la kujikunja na kujinyosha.

Kidemokrasia hugs zinamfaa mtu yeyote bila kufuata chama kama ni tawala au upinzani, zinamfaa maskini, tajiri, mweupe, mweusi, wanene, watoto, vijana, wazee, vikongwe, wafupi au warefu wote hugs zinawafaa.

Hug halina caffeine, nicotine wala calories na artificial ingredients asilimia mia moja ni kamilifu safi kabisa.

Hug ni halisi, kitu timamu ambacho hakina kitu chochote hatari haihitaji battery wala checkup ya kila siku, hata wakati wa hugging huhitaji nguvu bali ukipokea au kutoa hug unapata nguvu maradufu.

Hugs kiuchumi ni sound, hazina impact katika mazingira yetu ni environmentally friendly, hakuna global warming kwa kukumbatiana, hugs hazihitaji vifaa maalumu ni rahisi, huwezesha siku za furaha kuwa za furaha zaidi, hufanyi siku zisizowezekana kuwa siku zinazowezekana.

Huwezi kulipishwa kodi kwa hugging, huwezi kupata unene kwa hugging, huwezi kupata pollution kwa hugging, hakuna bills za hugging, wala hakuna inflation kwa hugging.

Hugging ni afya kwa mwili na roho, huponya msongo wa mawazo, kupunguza mawazo, huongeza uwezo wa kupata usingizi.

Huwezesha mwili kuwa na immunity ya kutosha kwa magonjwa, huhuisha maisha ya mtu bila side effect kama medications zingine

Hugging ni dawa yenye miujiza

Hugs ni free ndiyo maana wengi wanachukulia ni for granted, kama hugs zingekuwa zinauzwa kwenye maduka au stores au supermarkets, genge au grocery basi kwanza bei yake ingekuwa haishikiki na pia kila mtu angekimbilia kununua angalau japo apate moja kwa siku.

Hata kama hugs ni bure zisipotumika hazina thamani yoyote. Hugs zisizotumika hupotea milele

Katika dunia ambayo watu wana njaa ya kupendwa je, Ni vizuri kupoteza angalau hata hug moja?

Wanasayansi wamethibitisha kwamba:

Hugs 4 kwa siku ni hitaji la kila Binadamu kwa siku ili aishi.

Hugs 8 kwa siku huhitajika kwa ajili ya kuimarisha kiwango cha emotions.

Hugs 12 kwa siku ni muhimu kwa ajili ya kukua na kuwa mtu mwema na bora.

Hakuna kitu kinaitwa hugs mbaya, hugs zote ni nzuri.

Lazima ukumbatiane na mtu angalau kwa siku mara moja na kama kuna mvua angalau mara mbili kwa siku

Pia kumbatia huku unatabasamu, kufumba macho si lazima

Kukumbatiana wakati mnaenda kulala hufukuza ndoto mbaya

Usikumbatie kesho kama leo unaweza kukumbatiaNo comments: