"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, July 27, 2011

Si kweli

ETI MNGEKUWA NA FEDHA ZA KUTOSHA BASI NDOA YENU ISINGEKUWA NA MATATIZO.

Fedha haziwezi kununua upendo wala furaha ya kweli.

Kama ni hivyo basi Prince Charles na Diana wasingetengana pamoja na kuwa na fedha za kutosha.

Lipo tatizo lingine la msingi ndiyo maana ndoa yenu hairidhishi.

ETI KWA SABABU ULIOANA NA MTU AMBAYE HAFANANI NA WEWE NDIYO MAANA MNA MATATIZO YA NDOA.

Ni kweli wanandoa kuoana huku wakifanana tabia ni moja ya suala la msingi katika kuifanya ndoa iwe imara, hata hivyo hii haina maana kwamba hamtakutana na matatizo katika ndoa yenu.

Matatizo ni kipimo kizuri cha Uimara wa ndoa yenu.

Matatizo, vikwazo, kupingana na hata kutoelewana kutakuwepo tu katika ndoa ila namna mnatatatua hayo mambo ndiyo ufunguo na msingi wa kuishi kwa raha au shida na mwenzi wako.

ETI NIMEINGIA KWENYE MATATIZO KATIKA NDOA HII KWA SABABU NIMEOANA NA HUYU MTU.

Ni uwongo uliotukuka!

Ni kweli Inawezekana huyo mtu wako anatatizo fulani pekee linalokupa shida hata hivyo hata mwingine unayedhani asingekuwa na tatizo naye ana matatizo yake mpya makubwa kuliko ya huyo uliyenaye, huoni matatizo yake kwa kuwa huishi naye.

Hakuna mtu ambaye hana matatizo duniani.

ETI TATIZO NI YEYE SIYO MIMI NDIYO MAANA NDOA INA MATATIZO

Umeamua kuwa jaji, hakimu na mwendesha mashitaka?

Nikupe homework?

Kama ni ndiyo, basi tafuta wanandoa 2 walioachana, muulize wa kwanza akupe sababu za kuachana. Jibu ni kwamba kila mmoja atamlaumu mwenzake.

Why?

Kwa sababu ndoa ni wawili na kila mmoja huchangia kuleta furaha au huzuni, kujenga au kubomoa period!

ETI NDOA YENYE FURAHA HAINA MIGONGANO KAMWE.

Huo ni uwongo mweupe!

Hata zile ndoa zenye furaha kuliko zote duniani hukumbana na matatizo na migogoro mara kwa mara.

Namna wanashughulikia matatizo na migogoro kwa upendo na pamoja ndicho hufanya ndoa zao kuwa imara na zinazoridhisha.

ETI KAMA NITAJIWEA BUBU BILA KUZUNGUMZA CHOCHOTE LINAPOTOKEA TATIZO BASI LITAYEYUKA LENYEWE

Unajidanganya!

Kula jiwe si suluhisho bali husababisha tatizo kubwa mlima ambao huwezi kupanda au shimo refu ambalo ukiingia kutoka huwezi.

ETI ILI KUEPUKA KUBISHANA NITAKUWA NAMJIBU NDIYO KWA KILA KITU

Ukweli hukipendi ndoa yako!

Kujibu ndiyo kwa kila kitu ili kuepuka kubishana unafanya mwenzako akuone mtu usiyewajibika na huna jipya na akili yako inapungua na badala ya kukua inadumaa na huna mchango katika ndoa.

ETI KWA KUWA TUMEOANA WOTE DINI MOJA, KABILA MOJA, MKOA MMOJA, RANGI MOJA NA ELIMU SAWA BASI HATUTAKUWA NA MATATIZO KATIKA NDOA

Kama umeoana na dini yake, kabila lake, mkoa wake, rangi yake na elimu yake basi matatizo hayatakuwepo ila kama umeoana na kiumbe kinaitwa mtu basi jiandae la sivyo utakuwa disappointed kama si kuwa frustrated.

No comments: