"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, July 11, 2011

Wanaposaka Huchemka

Wanaume, kama walivyotofauti na wanawake hufanya kitu kimoja kimoja (one track minded), kila wanachofanya huwa kimoja kwanza na huweza kuweka focus kwenye kitu kimoja anachofanya.

Kwa maelezo zaidi soma link ya hapa chini

http://mbilinyi.blogspot.com/2009/08/mwanaume-ni-box.html

Mwanaume anaweza kumualika mwanamke nyumbani kwake anachokiwaza ni sex, anaweza kumualika mwanamke kwa ajili ya lunch au supper anaweza kuwa na lengo moja tu kichwani mwake nacho ni sex, kama mwanamke atamtania huyu mwanaume, atakachofikiria na kuchukulia ni sex.

Kazi ni kwako!

Wanaume huwekeza kiasi kidogo sana kwenye bank ya mapenzi na cha ajabu huwekeza kidogo sana wakitegemea kuvuna vingi tena kwa muda mfupi. Mwanaume akimpenda mwanamke hata kwa muda mfupi huamini alichowekeza anaweza kuvuna mara mbili yake hata kwa wiki moja. Katika mapenzi wanaume huwekeza kwa malengo ya muda mfupi kuliko muda mrefu.

Ndivyo asili yao inavyowatuma ndiyo maana kwenye mahusiano mengi wanawake ndiyo huumizwa.

Linapokuja suala la mahusiano wanaume huangalia tu suala la mwonekano (physical attributes) za mwanamke kuliko kitu chochote kingine.

Mwanaume anaweza kumpenda mwanamke kwa sababu ya urembo wake na anaamini Mungu atamsaidia kujua mengine yaliyobaki kama vile tabia nk.

Wanaume hupenda kuongeza (control) kila eneo, hupenda kuiendesha gari bila kuelekezwa hata kama amepotea, hupenda kulipa bill hotelini hata kama ana fedha kidogo, hupenda kujieleza alivyo na mafanikio hata kama yupo kwenye wakati mgumu kimaisha.

Pia wanaume huchukua muda mrefu kujua makosa yako na hata wakijua mara nyingi huwa “too late to catch the bus”.

Pia wanaume huwa hawapendi kuomba msamaha na wapo tayari kuomba msamaha kiana kwa kuwanunulia wapenzi wao zawadi badala ya kukiri tu “nimekosa nimsamehe mpenzi wangu”

NAMNA WANAUME HUCHEMKA WAKATI WA KUSAKA MPENZI

Kwa kuwa wanapenda urembo, sura na mwonekano wa nje kwa mwanamke na huamini kwamba kwa kuwa huyu mwanamke (dada) ni beautiful lazima atakuwa na tabia njema, mwelewa, mvumilivu, amelelewa vizuri na mwema na wanajisahau kufahamu sifa za mwanamke ambaye anafaa kwa mahusiano (sifa na mitazamo ya mwanamke), matokeo yake wanaume huchanganya upendo na tamaa (love/lust). Matokeo yake hutumia muda wao na nguvu zao kusherehekea urembo wa mwanamke badala ya kuchunguza sifa za ndani ambazo pia kazi yake ili kufahamu ni ngumu au huchosha. Akili yake inamtuma kumpa kwanza huyo mrembo na baadae atafahamu tabia yake.

In dating game, men are usually disaster!

Unaweza kusoma hapa chini kwa maelezo zaidi

http://mbilinyi.blogspot.com/2010/04/ndivyo-walivyo.html

http://mbilinyi.blogspot.com/2010/05/mume-akupende.html

No comments: