"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, August 25, 2011

Kileleni!

Katika ndoa sex ni kitu kizuri kinachowafanya wanandoa kuwa mwili mmoja kwa maana ya kuwaleta karibu.

Jambo kubwa ambalo huleta raha ya kiwango cha juu kwa wanandoa wakati wa tendo la ndoa ni suala la kufika kileleni (orgasm)

Kila mwanandoa anaweza kufika kileleni Ingawa si kila mmoja, kufika kileleni kwa wengine si issue rahisi hasa kwa wanawake Ingawa kwa wanaume ni kitu rahisi hata kitendo cha mwanaume kuwa na penetration na kuingia kwa mke wake basi anaweza kujikuta anafika kileleni, Ingawa hilo haliwezi kumfanya mwanamke kufika kileleni.

Kufika kileleni ni nini?

Ni kitendo cha kufikishwa juu kabisa katika raha ya sex, msukumo wa kiwango cha juu wa raha ya tendo la ndoa ambalo huishia kumwacha muhusika ajisikie yupo relaxed na mwepesi. Kwa mwanamke kufika kileleni huwa kwa sekunde kadhaa ambazo huendana na kujisikia relaxed na msukumo wa kutamani kama kunyanyuka ili kupokea kitu au kutoa hata hivyo kama mwanamke ataendelea kusisimuliwa huweza kujikuta anafika kileleni tena Ingawa hii ni kwa wanawake wa umri fulani.

Je kuna aina ngapi za kufika kileleni kwa mwanamke?

Kimsingi kuna aina mbili za mwanamke kufika kileleni na hizi aina zinajikita kutokana na aina ya msisimko anaoupata (stimulation).

Kwanza ni kifika kileleni kwa njia ya kusisimuliwa kisimi chake (clitoral) kwa mwanaume kukisisimua kwa kuchezea kwa njia Tofauti anazozijua au wanazoelekezana wakati wa tendo la ndoa.

Pili ni kufika kileleni kwa njia ya uke (vaginal) na hii mara nyingi hutokea kutokana na mwanaume kuingia na kutoka kwa mawimbi huku akigusa eneo la G-Spot

Uzuri ni kila aina ya kufika kileleni ina ladha yake na wanawake wenye uzoefu wa hizi aina wanafahamu Tofauti yake.

Ni wanawake wachache sana hufika kileleni kwa kitendo cha Mr. Happy kuwa ndani ya uke hata hivyo ni rahisi mwanamke kufika kileleni kwa kuchezewa kisimi/kinembe chake kwa namna zote (touching/rubbing or kissing)

Je, ni milalo ipi husaidia mwanamke kufika haraka kileleni?

Kwanza ni ule wa mwanamke kuwa juu ya mwanaume na pile ule wa mwanamke kulala kwa tumbo lake na mwanaume kumuingia kwa nyuma.

Je ni mambo gani yanaweza kuathiri mwanamke kufika kileleni?

KWANZA

Mara ngapi mwanamke anapata sex, ili mwanamke kufika kileleni anahitaji kuwa na sex ya mara kwa mara (use it or loss it). Mwanamke anapokaa kwa muda mrefu bila sex ndivyo anakuwa mgumu kusisimka na mgumu kufika kileleni period.

PILI

Lazima mwanamke awe relaxed na hana stress au tension. Ili mwanamke apate raha ya mapenzi ni lazima awe comfortable na mazingira yaliyopo na pia mahusiano au ndoa yake bila trust na mwenzi wake mwili unajifunga na ngumu kufungua.

TATU:

Hii inamuhusu mwanaume ambaye anahusika na huyu mwanamke anayetakiwa afike kileleni Kwani anatakiwa kuwa caring na anayefahamu kumsisimua mwanamke asisimke kiasi cha kutosha na kumsaidia kufika kileleni kwa kusoma upepo unavyovuma.

Pia ni vizuri kwa mwanamke mwenyewe kujitambua na kufahamu mwili wake vizuri na zaidi kushirikiana na mume wake kuwa wazi kumweleza kile anaona kinampa raha na kitapelekea kufika kileleni.

Je, unahitaji sex inayosisimua katika ndoa soma hapa

Tuesday, August 23, 2011

Nimpe?

Je, ni muhimu wanandoa kusalimiana mnapoamka asubuhi?

Kwanza fahamu kwamba wanandoa wanapokaa muda mrefu baadhi ya vitu huanza kuchakaa kimapenzi. Hata hivyo upendo na wema husaidia kurudisha moto wa mapenzi na wanandoa kujiona wapya kila umri unavyozidi kuongezeka.

Matendo yanayoonesha wema kwa wanandoa ni gundi inayoshikisha wawili kujiona wapo karibu na moja ya tendo la wema ni kumsalimia mwenzako wakati mnaamka hata kama mmelala kitandani kimoja na hata mlikumbatiana usiku mzima au ulimuweka mwenzi wako kifuani usiku mzima.

Anayesalimiwa hujiona anapendwa, ana thamani na pia appreciated.

++++++++++++++++++++++++++

Tupo kwenye new millennium kiasi ambacho watu tupo busy hata kuamka tunahitaji kuweka alarm ituamshe hata hivyo badala ya kukimbia bathroom kuoga ni muhimu kumpa kwanza salamu mwenzi wako ndipo uendelee na kazi zingine au na ratiba yako.

Tafiti zinaonesha wanandoa ambao husalimiana asubuhi wanajiona ndoa yao ni nzuri sana na wana mahusiano yanayoridhisha.

++++++++++++++++++++++++++++++++

Je, nini kinafanya maneno ya salaamu ya asubuhi kuwa muujiza katika ndoa na mahusiano?

Unapomsalimia mwenzi wako maana yake unamwambia na kumpa ujumbe kwamba ni asubuhi njema tumeamka pamoja katika upendo na furaha na kwamba unajisikia vizuri kuanza siku mpya na mtu wako na pia unaweza msingi mzuri wa mawasiliana kwa hiyo siku mpya.

Wanaume Nao......

Kwa nini wanaume hununua sex?

Mwanaume anaondoka na kwenda kumtafuta mwanamke wa kumlipa fedha ili ampe sex bila kuhusisha upendo au mahusiano wala kuhusisha hisia kati ya wawili.

Suala la wanawake Malaya (prostitutes) kuua mwili kwa wanaume ni suala la dulia zima haijalishi ni mzungu au mweusi au muasia, wasomi na wasio wasomi, maskini na matajiri, waliooa na ambao hawajaoa wote wamekuwa wakijihusisha na hii tabia.

Wanaume walioulizwa kwa nini wanaenda kununua sex wengi walitoa Sababu zifuatazo Ingawa walikiri kwamba wakati wa sex na hao Malaya huwa wanajisikia aibu, hatia, na hisia hasi kulipa ili upate sex.

Sababu kubwa ya wanaume kununua mapenzi wengi walikiri ni kumridhisha hitaji ya sex na raha yake kwa wakati ule (32%)

Waliofuatia walisema Sababu kubwa ni kutaka kupata ladha Tofauti ya mwanamke (21%)

Wengine walikiri kwamba wanaenda kununua sex kwa Sababu hawapati kile wanahitaji kutoka kwa wake zao nyumbani (20%)

Wengine walikiri kwamba ni kwa Sababu wao wana fedha na Malaya wanapatikana bila Tatizo (15%)

Asilimia 8 walikiri kwamba wananunua sex kwa Malaya kwa Sababu ya kufurahia tu sex (thrill/surprise) wanayopata

Na asilimia 3 walikiri kwamba kununua sex kwa Malaya ni addiction ambayo imo ndani yao kama walivyo walevi au wavuta sigara.

Je, hawa wanaume hufanyia wapi hivi vitendo vyao ya kununua sex na Malaya?

Wengi walikiri kwamba sehemu ambazo unaweza kununua sex kwa Malaya ni kwenye danguro (60%), sehemu za kufanya massage (47%), wanaotoa huduma za kusindikiza (33%) na Saunas (27%).

Sehemu zingine ni makaburini, kwenye magari na wakati mwingine huchukuliwa majumbani kwa hao wanaume.

Hata hivyo cha ajabu ni kwamba hawa wanaume wanakiri kwamba kama Hakuna Malaya wa wao kununua sex wangeweza kubaka kama Hakuna kukamatwa na wanaamini kwamba hawa Malaya hawana haki au kuongea chochote wakati wa sex kwa kuwa wamewanunua.

Je, hawa wanaume hupata kitu gani kwa hawa Malaya wanaowauzia sex?

Wengi wanakiri kwamba Hakuna kipya wanakipata kwa hawa Malaya na baada ya sex hujikuta wapo empty moyoni, aibu na kujutia matumizi ovyo ya fedha hata hivyo cha ajabu pamoja na kujisikia vibaya bado wanaendelea kwenda kununua hiyo huduma.

Hata hivyo wapo wanaume ambao wamekiri wazi kwamba hawajui namna ya kujihusisha na mwanamke na kufanya bonding ya mapenzi hivyo njia rahisi kwao ni kulipa na kumpata huyo Malaya.

Je, Malaya nao hufurahia sex Wakiwa na wateja wao

Mmoja ya mteja amesema si sahihi kwa Malaya kupata raha ya sex kwa kuwa hana haki Kwani ameuza na kazi yake ni kumpa raha aliyenunua vinginevyo utakuwa ni uchakachuaji.

Je, wanawake Malaya wana sifa Tofauti na wanawake wengine?

Wazoefu ya hiyo huduma wanakiri kwamba ni kweli wanao uwezo wa kufanya vitu ambavyo mwanamke wa kawaida hawezi kuvifanya kwa mwanaume vitendo ambavyo wengine huviona kama vinachefua.

Monday, August 22, 2011

Ukweli wao!

Mshauri maarufu wa masuala ya ndoa M. Gary Neuman alifanya Utafiti kwa kuwauliza wanaume 200 ambao kati yao walishachepuka nje ya ndoa zao na wengine walikuwa hawajawahi kuchepuka (cheat) na lengo lake lilikuwa ni kufahamu kwa nini hawa wanaume huchepuka nje ya ndoa zao.

Mara nyingi watu wanaotaka kujua kwa nini wanaume wana cheat huwauliza wanawake hata hivyo Gary Neuman aliamua kuwauliza wanaume wenyewe ili wajieleze kwa nini wanachepuka (cheat) na pia alitaka kuwauliza je nini kingefanyika basi wasinge thubutu kuchepuka.

++++++++++++++++++

Asilimia 48 ya hao wanaume walikiri kwamba kutoridhishwa kihisia (emotions) ilikuwa Sababu ya msingi kuchepuka.

Wengi huamiini kwamba mwanaume ili kutoka nje ya ndoa yake hufuata sex tu, wanaamini kinachomfanya mwanaume kuwa na furaha ni sex.

Ukweli ni kwamba hata wanaume ni viumbe wa hisia (feelings/emotions), wanapenda wake zao wawashukuru, wawape sifa wanazostahili kutokana na juhudi zao za kifamilia na masuala ya ndani ya ndoa (appreciation).

Tatizo kubwa ni kwamba wanaume hushindwa namna ya kuelezea hisia zao kwa wake zao na matokeo yake mahitaji yao ya kihisia hupitwa bila kupewa kila wanahitaji.

Nini mwanamke anatakiwa kufanya kwa mume wake:

Ni kumpa appreciation idara zote na hiyo ni silaha

++++++++++++++++++++++

Asilimia 66 walikiri kwamba hujisikia hatia (guilt) wanapochepuka (cheat)

Si kwamba wanaume wanaochepuka ni wanaume ovyo tu bali kuna asilimia 68 ya wanaume hawakuwahi kuota kama kuna siku watachepuka na pia husikitika kwamba afadhari wasingethubutu kufanya.

Hii ni kudhihirisha kwamba kujisikia hatia wakati wa kuchepuka hakuwezi kuzuia asichepuke.

Tabia kubwa ya mwanaume ni kiumbe ya kitu kimoja kwa wakati (compartmentalization, single task) kwa maana kwamba hata kama anajisikia hatia bado huwa na uwezo wa kufurahia sex na anajua atashughulikia hiyo hatia baadae Kwani kujisikia hatia na kufurahia sex na yule mwanamke ni vitu viwili kwake na Tofauti.

Hii ina maana gani kwa mwanamke yeyote?

Hii ina maana kwamba hata kama mume wako anaapa kwa kila anachokijua kwamba hatachepuka, usidhani kwamba hawezi kutokea badala yake Mnatakiwa kuchukua hatua muhimu kutengeneza ndoa mnayoihitaji.

++++++++++++++++++++++++

Asilimia 77 ya wanaume wanaochepuka wana rafiki wa karibu ambaye alichepuka.

Mwanaume kuwa karibu na rafiki ambaye si mwaminifu huwezesha aone kuchepuka ni kitu cha kawaida na sahihi.

Kichwani mwake kuna kuwa na ujumbe kwamba “huyu rafiki yangu ni mtu mzuri na bado anaweza kuchepuka na kumdanganya mke wake, hivyo wanaume wazuri wote tunaweza kuchepuka.

Ingawa si rahisi kumkataza mwanaume au mume wako asitumie muda wake na rafiki zake ambao macho yao ni kwenye malinda ya wanawake unachoweza ni kumsaidia kutumia muda wake na hao marafiki katika mazingira ambayo si hatarishi kama vile michezo na si night clubs au bar.

Nini mwanamke anaweza kufanya katika hili.

Ni kujenga mahusiano ya jamii ambayo mume huwa rafiki na mtu wa kufurahishana kijamii kama vile kuangalia match za mpira pamoja au kufanya pamoja kile mume wako anakipenda.

Jenga mazingira yanayofanya ndoa kuwa mpya kila leo.

+++++++++++++++++++++++++++

Asilimia 40 ya wanaume wanaochepuka walikutana na huyo mwanamke kazini.

Mara nyingi mwanamke anayechepuka naye ni yule ambaye anampa sifa, ana kuwa karibu naye kwa kile anahitaji na ana msifia kwa juhudi zake katika mambo anayofanya.

Ndiyo maana ni muhimu sana mwanaume kujiona ana thamani nyumbani.

Pia wewe mwanamke unatakiwa kuwa makini kwa yule mwanamke wa kazini kwake ambaye anamtajataja mara nyingi kuliko wanaume wenzake huko kazini.

Nini cha kufanya kwa mwanamke ukigundua kuna mwanamke anamtajataja?

Jambo la msingi ni kuweka mipaka tena kwa upendo na uwe makini kufahamu kama anachelewa kazini kwa Sababu yupo na huyo mwanamke, au anasafiri na huyo mwanamke au anaenda lunch au dinner na huyo mwanamke na si wanaume wenzake.

Au muulize yeye atajisikiaje kama na wewe mwanamke utafanya hao na mwanaume mwingine.

+++++++++++++++++++++++++++++

Asilimia 12 ya hao wanaume walikiri kwamba ni kweli wanawake waliochepuka nao walikuwa ni warembo kuliko wake zao.

Hii ni asilimia ndoa sana na ina maana kwamba mwanaume hatoki kwa Sababu anaamini akiwa na mrembo basi atapata sex nzuri, ukweli ni kwamba anachepuka kwa Sababu ana pengo la kihisia ndani yake.

Anajiona yupo connected na mwanamke mwingine kuliko wewe mke wake na sex hupata msaada (lift) kupitia hiyo connection.

Kama una wasiwasi na mume wake kuchepuka basi focus katika kuimarisha mahusiano na kupendana na kuwa connected kuliko kuonekana una sura na urembo wa uhakika au kujua ulale vipi (chumbani)

Sijasema usipendeze au mume wako hahitaji sex bali unatakiwa kuweka mkazo katika upendo na ukaribu wa mapenzi kwanza na kumridhisha hisia zake kwanza ndipo sex.

+++++++++++++++++++++++++++

Asilimia 6 tu ya wanaume wanaochepuka walichepuka siku ile ya kwanza kukutana na huyo mwanamke.

Hii ina maana kwamba wanaume wanaochepuka huonesha dalili mapema kabla ya tukio lenyewe.

Angalia hizi alama

Kwanza hutumia muda mwingi nje ya nyumbani, anaacha kukuuliza kutaka sex, anaanza kuwa mkali bila Sababu ya msingi, anaanza kutojibu simu zako au sms.

Badala ya kumkoromea, unatakiwa kuchukua hatua za kuimarisha mahusiano yako na yeye kwa upendo mpya zaidi.

Pia wapo wanaume ambao hata ufanyeje wao kuchepuka ipo tu.

Hata hivyo wapo wanaume ambao ni makini na smart sana kiasi cha kuwa kazi ngumu sana kuwakamata au kujua kwamba wanachepuka.

Soma hapa


Sunday, August 21, 2011

Usijaribu!

SWALI:

Hello mimi ni dada ninayeishi Iringa nina umri wa miaka 18 kwa bahati mbaya mpenzi wangu amenipa mimba na kutokana namna alivyo baba yangu Naamini akifahamu kwamba nina mimba ataniua Kwani mimi ni mwanafunzi.

Nimeongea na boyfriend wangu tumekubaliana tukaitoe.

Hata hivyo bado najiuliza kama kutoa mimba (abortion) ni kitu sahihi?

Na je, nifanyeje Kwani nipo kwenye njia panda.

MAJIBU:

Mdogo wangu pole sana kwa yaliyokukuta hasa kitendo cha kujiingiza kwenye masuala ya mapenzi badala ya kukomaa na shule kwanza.

Sikufichi umeshachanganya mambo na kuna gharama utalipa kwa maamuzi yako uliyoyafanya.

Jambo la msingi ni kwamba sidhani kama kuna anayehusika na utoaji mimba anayeweza kukwambia ukweli kuhusiana na kutoa mimba (abortion)

Kutoa mimba ni uuaji (murder) na kutoa hiyo mimba kutakufanya uishi kama muuaji sawa na wauaji wengine wanaoua watu na hiyo hatia itakaa moyoni mwako miaka yako yote hapa duniani.

Ukweli ni kwamba kovu la hisia za kutoa mimba zitakuwinda maisha yako yote na hatia (guilt) hutisha.

Utajisikia huzuni, hasira pale ikitokea mtu anaanza kuzungumzia suala la utoaji mimba (abortion) pia unaweza kujikuta una hisia mbaya unapowaona watoto wadogo hasa wale watakaokuwa umri sawa na yule mtoto uliyemuua kwa kutoa mimba yake pia unaweza kujikuta hapendi kabisa kushika watoto au kuwagusa watoto wenye umri sawa na yule ambaye angekuwa mtoto wako.

Ulipokuwa unafanya mapenzi na huyo boyfriend wako uliamua, na hamkutumia njia yoyote ya kuzuia mimba na ulijua wewe na boyfriend wako kwamba hicho kitendo kinaweza kusababisha mimba, hivyo basi wewe na boyfriend wako mnawajibika kwa ajili ya kuhakikisha huyo mtoto (kiumbe kisicho na hatia) anatunzwa tumboni na kuzaliwa salama na mnamtunza kama wazazi.

Pia ufahamu kwamba madhara ya kutoa mimba ni zaidi ya unavyofikiria, kuna wanawake hupoteza maisha wakati wa kutoa mimba na wengine huugua kiasi cha kufa.

Inawezekana ni kweli baba yako atakasirika sana kusikia una mimba, pia Naamini mzazi mwenye busara hawezi kumuua binti yake kwa kuwa ana mimba ya mjukuu wake. Naamini baba yako atakasirika na mwisho atakusamehe.

Kama ulikuwa unawaza kwamba siku moja utakuwa na mtoto baada ya ndoa au harusi kubwa, ni muhimu na busara kuanza kufuta hayo mawazo na badala yake tunza hiyo mimba na mtoto atazaliwa na maisha yataendelea kama kawaida.

Hakuna Tatizo linalotokea hapa duniani ambalo ni jipya yote yalikuwepo na maisha yanaendelea.

Inawezekana katika kutoa mimba ukapoteza kizazi au uzazi na siku moja ukaolewa na kushindwa kupata watoto na utajisikiaje utakapomwambia mume wako mpenzi kwamba huweza kupata mimba kwa kuwa ulimuua mtoto ambaye alikuwa tumboni mwako?

Inawezekana kwako kupata hiyo mimba ni bahati mbaya, hata hivyo mbele za Mungu huyo mtoto si bahati mbaya (accident) bali ni mpango wa Mungu kwamba azaliwe duniani na mtoto kama mtoto hana kosa ila wewe na boyfriend wako.

Je, ingekuwaje kama wazazi wako nao wangekuua ungali tumboni mwa mama yako?

Jiulize ni namna gani wangekosa unavyocheka, unavyo smile, unavyotoa machozi, unavyowapenda na vitu vyote vinavyowapa furaha ya maisha.

Achana kabisa na wazo la kutoa mimba.

Kumbuka kutoa mimba ni dhambi ya uuaji na hapa Tanzania pia ni kosa

Unajua?

Wapo wanawake huweza kufika kileleni kwa kusisimuliwa matiti yao tu.

Asilimia moja ya wanawake huweza kufika kileleni kwa kuchezewa nyonyo na waume zao au wapenzi wao.

Hili limewekwa wazi na mwanaharakati wa masuala ya mahusiano aitwaye Marshall Miller na mwenzake Dorian Solot.

Inawezekana mpenzi wako au mke wako ni mmoja wao kama wewe ni mwanaume.

Kuna baadhi ya wanaume wana ugonjwa wa kuyaangalia matiti ya wanawake kiasi ambacho huweza hata kusisimka.

Wakiwa njiani au barabarani au mahali popote wanawake wapo basi kile kitendo cha kumuona mwanamke mwenye matiti makubwa humfanya ajisahau na kubaki kakodoa mimacho hadi kuhatarisha maisha yake kwa akili yake kupotelea kwenye kifua cha mwanamke.

Pia jamii kama ya wamarekani ina ugonjwa wa kupanda matiti kuliko jamii zingine duniani tena matiti makubwa kiasi ambacho hata biashara ya kubadilisha matiti (breast implant) ina vuma na inatengeneza mamilioni ya dola.

Titi la kushoto ni kubwa kuliko titi lile la upande wa kulia.

Hii ni kutokana na chapisho ambalo liliyaangalia matiti 600 ya wanawake ambao walikuwa wanafanyiwa breast Implant au plastic surgery.

Hivyo kama ni mwanamke haina haja kushangaa au kujiuliza ukihisi titi moja ni kubwa au dogo kuliko lingine ila si kwa utofauti mkubwa ambao huleta shaka.

Wapo wanaume ambao matiti yao hutoa maziwa pia.

Ingawa ni mara chache sana hata hivyo wapo wanaume wakati Fulani katika maisha yao hujikuta chuchu zao zinatoa kiasi kidogo sana cha maziwa.

Hii ni kwa Sababu hata wanaume wana homoni (mammary glands) kama walivyo wanawake. Na baadhi ya dawa za kutibiwa (cancer) zina kiasi fulani cha estrogen ambayo husababisha maziwa kutoka.

Wanawake ambao hubadilisha matiti (breast implant) ndiyo hujinyonga zaidi katika wanawake ambao hujinyonga duniani.

Utafiti ulifanywa na chuo kikuu cha Laval Quebec Canada uligundua kuwa kati ya wanawake waliojinyonga asilimian 75 walikuwa ni wale ambao walibadilisha matiti yao.

Sababu ya msingi ya kufanya idadi wa wanaojinyonga kuwa kubwa ni kutokana na kutojiamini, msongo wa mawazo au kutojiamini na maumbo ya miili yako. Wapo wanawake ambao huamiini matiti makubwa huwafanya wajiamini au kuwa na matiti makubwa badala ya madogo huwasaidia kutatua matatizo mengine.

Ukweli usiopingika ni kwamba wanawake ambao hubadilisha matiti yao kwa kufanya implants huwa haiwasaidii sana Kwani Tatizo si matiti bali mitazamo yako ya kutojiamini.

Kulala mlalo wa kuyalalia matiti (kifudifudi) hakuwezi kufanya yapungue umbo (kuwa madogo)

Ingawa huweza kubadilisha mwonekano wake baada ya muda.

Njia nzuri ya kulala ambayo humfanya matiti yako yawe na umbo lililoimarika ni wewe kulala kwa ubavu na weka mto kuyapa support.

Zaidi ya wanawake milioni 2 duniani wana matiti ambayo ni fake (siyo ya ukweli).

Hata kama suala la kubadilisha umbo na kuweka vitu vya ziada (plastic surgery/implants) bado hivi vitendo vina athari za kiafya kwa mwanamke.

Inawezekana huyo mpenzi wako kike ana matiti fake!

Matiti nayo yana mzunguko wake wa siku na siku zake.

Baada ya mwanamke kupata siku zake matiti huwa laini (soft, smooth) na chuchu huwa na msisimko zaidi kwa kuwa estrogen huwa katika kiwango cha juu.

Na mwanamke akiwa kwenye siku zake matiti huwa tender na wakati mwingine huuma na kuongezeka size kwa kuwa homoni ya progesterone huwa katika kiwango cha juu.

Chuchu za wanawake hutofautiana katika size na shape na pia namna zinasimama (zikisisimliwa) katika mwelekeo.

Matiti huongezeka unene mwanamke anapoongezeka umri.

Mwanamke anapokuwa kijana titi hujawa na kiwango kikubwa cha fat, maziwa na collagen, na mwanamke anapozeeka vyote hubadilishwa na fat.

Bahati mbaya ni kwamba kuongezeka huko kwa umbo ndiko husababisha matiti kulala na si kusimama Kwani sasa inakuwa imebaki fat tu na si maziwa.

Kwa Maelezo zaidi kuhusu matiti soma hapa

Tuesday, August 16, 2011

Moto Umezima


SWALI
Mimi na mume wangu tumekuwa kwenye ndoa sasa ni mwaka wa 11, maisha yetu ni mazuri sana kila eneo la ndoa yetu isipokuwa suala la sex. Najiona kukumbuka sana namna moto wa mapenzi (passion) ulikuwa huko nyuma na sasa kila kitu kinaenda ovyo Linapokuja suala la sex.
Je tufanyeje ili mambo yarudi kama zamani?
Ni mimi Edna
JIBU:
Swali lako ni zuri na si mara ya kwanza kuulizwa hapa.
Pia nikupongeze kwa kufikisha miaka 11 pamoja Kwani maisha ya mahusiano siku za leo ni Tofauti sana.
Jambo la msingi ni kufahamu kwamba umekuwa na ndoa nzuri kwa miaka 11 kwa Sababu kila siku mmekuwa mnajitahidi kufanyia kazi ndoa yenu na pia maisha ya sex yameanza kuelekea kwenye velanda ya ICU kwa Sababu mmejisahau na kuacha kufanya vile mlikuwa mnafanya huko nyuma.
Inawezekana mnafanya kila kitu kwa kuzoeana na mazoea kuanzia kabla ya kuingia chumbani hata wakati mkiwa chumbani.
Je, unawezaje kurudisha moto wa mapenzi wewe na mumeo?
Jambo la msingi ni namna kila mmoja anajitoa (committed) kuwa wa motomoto kimapenzi na suala zima la maisha ya mapenzi kwa pamoja.
Baada ya kujitoa suala linalofuata ni kupanga, panga na fikiria vitu ambavyo mnaweza kufanya pamoja, vitu vipya, kuwa wabunifu wa nini mfanye pamoja na kile kitendo tu cha kufanyia kazi yale mnataka kufanya pamoja tayari kitaanza kuwapa furaha na msisimko wa pamoja kimapenzi.
Sasa Hakuna moto wa mapenzi kwa kuwa ule moto mmeuzima au umeenda kulala usingizi mzito, ni muda wa kuwasha na kuamka, jaribu vitu vipya, jaribu mlalo mpya wakati wa sex, jaribu kwenda kufurahia miili yenu sehemu Tofauti na hapo chumbani kwenu, jaribu muda Tofauti wa sex, jaribu kugusa sehemu Tofauti katika mwili wakati wa kufanya maandalizi na fanya yote kwa upendo na kwa kupokea na kutoa.
Jaribu kusafiri au kutembelea sehemu mpya pamoja kama mke na mume (mbuga za wanyama, beach au hotel)
Pika pamoja, cheza pamoja, piga story pamoja, mlishe chakula mpaka ashibe, kumbatianeni, shikaneni, mwambie maneno matamu ambayo hujawahi kuyasema, mtie moyo, msifie, mpende nk
Mapenzi motomoto hayaji yenyewe lazima muwe wabunifu na wavumbuzi
Uwe mbunifu, mbunifu, mbunifu, mbunifu, mbunifu…………

Monday, August 15, 2011

Yana siku zake.....

Wapo wanawake huweza kufika kileleni kwa kusisimuliwa matiti yao tu.

Asilimia moja ya wanawake huweza kufika kileleni kwa kuchezewa nyonyo na waume zao au wapenzi wao.

Hili limewekwa wazi na mwanaharakati wa masuala ya mahusiano aitwaye Marshall Miller na mwenzake Dorian Solot.

Inawezekana mpenzi wako au mke wako ni mmoja wao kama wewe ni mwanaume.

Kuna baadhi ya wanaume wana ugonjwa wa kuyaangalia matiti ya wanawake kiasi ambacho huweza hata kusisimka.

Wakiwa njiani au barabarani au mahali popote wanawake wapo basi kile kitendo cha kumuona mwanamke mwenye matiti makubwa humfanya ajisahau na kubaki kakodoa mimacho hadi kuhatarisha maisha yake kwa akili yake kupotelea kwenye kifua cha mwanamke.

Pia jamii kama ya wamarekani ina ugonjwa wa kupanda matiti kuliko jamii zingine duniani tena matiti makubwa kiasi ambacho hata biashara ya kubadilisha matiti (breast implant) ina vuma na inatengeneza mamilioni ya dola.

Titi la kushoto ni kubwa kuliko titi lile la upande wa kulia.

Hii ni kutokana na chapisho ambalo liliyaangalia matiti 600 ya wanawake ambao walikuwa wanafanyiwa breast Implant au plastic surgery.

Hivyo kama ni mwanamke haina haja kushangaa au kujiuliza ukihisi titi moja ni kubwa au dogo kuliko lingine ila si kwa utofauti mkubwa ambao huleta shaka.

Wapo wanaume ambao matiti yao hutoa maziwa pia.

Ingawa ni mara chache sana hata hivyo wapo wanaume wakati Fulani katika maisha yao hujikuta chuchu zao zinatoa kiasi kidogo sana cha maziwa.

Hii ni kwa Sababu hata wanaume wana homoni (mammary glands) kama walivyo wanawake. Na baadhi ya dawa za kutibiwa (cancer) zina kiasi fulani cha estrogen ambayo husababisha maziwa kutoka.

Wanawake ambao hubadilisha matiti (breast implant) ndiyo hujinyonga zaidi katika wanawake ambao hujinyonga duniani.

Utafiti ulifanywa na chuo kikuu cha Laval Quebec Canada uligundua kuwa kati ya wanawake waliojinyonga asilimian 75 walikuwa ni wale ambao walibadilisha matiti yao.

Sababu ya msingi ya kufanya idadi wa wanaojinyonga kuwa kubwa ni kutokana na kutojiamini, msongo wa mawazo au kutojiamini na maumbo ya miili yako. Wapo wanawake ambao huamiini matiti makubwa huwafanya wajiamini au kuwa na matiti makubwa badala ya madogo huwasaidia kutatua matatizo mengine.

Ukweli usiopingika ni kwamba wanawake ambao hubadilisha matiti yao kwa kufanya implants huwa haiwasaidii sana Kwani Tatizo si matiti bali mitazamo yako ya kutojiamini.

Kulala mlalo wa kuyalalia matiti (kifudifudi) hakuwezi kufanya yapungue umbo (kuwa madogo)

Ingawa huweza kubadilisha mwonekano wake baada ya muda.

Njia nzuri ya kulala ambayo humfanya matiti yako yawe na umbo lililoimarika ni wewe kulala kwa ubavu na weka mto kuyapa support.

Zaidi ya wanawake milioni 2 duniani wana matiti ambayo ni fake (siyo ya ukweli).

Hata kama suala la kubadilisha umbo na kuweka vitu vya ziada (plastic surgery/implants) bado hivi vitendo vina athari za kiafya kwa mwanamke.

Inawezekana huyo mpenzi wako kike ana matiti fake!

Matiti nayo yana mzunguko wake wa siku na siku zake.

Baada ya mwanamke kupata siku zake matiti huwa laini (soft, smooth) na chuchu huwa na msisimko zaidi kwa kuwa estrogen huwa katika kiwango cha juu.

Na mwanamke akiwa kwenye siku zake matiti huwa tender na wakati mwingine huuma na kuongezeka size kwa kuwa homoni ya progesterone huwa katika kiwango cha juu.

Chuchu za wanawake hutofautiana katika size na shape na pia namna zinasimama (directions)

Matiti huongezeka unene mwanamke anapoongezeka umri.

Mwanamke anapokuwa kijana titi hujawa na kiwango kikubwa cha fat, maziwa na collagen, na mwanamke anapozeeka vyote hubadilishwa na fat.

Bahati mbaya ni kwamba kuongezeka huko kwa umbo ndiko husababisha matiti kulala na si kusimama Kwani sasa inakuwa imebaki fat tu na si maziwa.

Kwa Maelezo zaidi kuhusu matiti soma hapa

Monday, August 8, 2011

Happy birthday Lazarus..

Leo nimetimiza miaka kadhaa.
Nashukuru upendo wa mke wangu Gloria na watoto wangu Emmanuel (8) na Karen (2) walionipa na kunifanya niwe na furaha, bila ninyi vitu vingine havina maana na thamani kwangu.
Pia nawashukuru familia na marafiki zangu wote kwa upendo wenu na maombi yenu, kwani ninyi mnanifanya nijifunza kuwa mtu bora duniani.

Mungu akubariki

Lazarus P. Mbilinyi

Sunday, August 7, 2011

Nibusu Hivi.......

Tofauti na michezo mbalimbali, Linapokuja suala la kubusu ukitaka unaweza kuwa mzuri na maarufu kwa mpenzi wako ukitaka. Hata hivyo kuvutiana (attraction) kimapenzi na upendo ndicho kiungo muhimu hii ina maana kama Hakuna attraction busu ni tupu halina ladha.

Kubusu ni njia ya kuonesha upendo, mapenzi, kwamba unamjali na unampenda na njia nyingine ya kukiri na kusema “Nakupenda” unavyozidi kuwa na feelings na huyo mpenzi wako ndivyo na busu linavyozidi kuwa tamu.

++++++++++++++++++++++++++++++++++

Unibusu Hivi!

Kwanza nikumbatie, Hold me Please!

Pili, unaponibusu nataka busu laini, bila ulimi kwanza bali lips zangu na zako, busu lips kwa kuanza na ya chini kwa kupalaza . Sihitaji ulimi wako ndani ya kinywa changu ninachohitaji kwako sasa ni lips tu, kwa muda mrefu, laini, tamu, niangalie usoni.

Nikikolea ndipo nitaashiria nataka nini……………………….

Tatu, usafi ndiyo wimbo bora wa kubusiana, kabla ya kunibusu kwanza jiulize je, harufu yako ya mdomo inafanana na pepperoni pizza?

Kama hujaelewa, nina maana Nahitaji kinywa chetu harufu sana.

Umeshindwa kuwa na gum, pipi, au hata kupiga mswaki na ukanukia safi na ni raha.

Usitanie kwa kinywa chako kinachonuka unanifanya niwe turned offffffff.