"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 6, 2011

Chagua Vema

Suala la kuchagua mtu wa kuoana naye ni hatua rahisi ya muhimu katika process ya kuingia katika ndoa.

Jambo la msingi ni kuweka mkazo au msisitizo zaidi katika sifa za binadamu alivyo ndani yake kuliko kuangalia vitu alivyonavyo na anavyoonekana. Pia sifa za akili zake (mental) ni muhimu kuliko sifa za mwilini (physical).

Sifa za ndani za kibindamu si rahisi sana kubadilika kama sifa za nje na vitu alivyonavyo ambavyo hubadilika.

Pia tusisahau kwamba katika suala la kuchagua mke au mume wa kuishi naye katika ndoa suala la bahati lipo na hapa hakuna maswali.

Hata hivyo suala la kukubaliana kuoana na mwanaume au mwanamke ambaye ni cha pombe ukiamini mkioana ataacha au utambadilisha ni suala ambalo Unajidanganya.

Pia kwa mwanaume kuoana na mwanamke kwa sababu tu anaonekana mrembo na kupuuzia sifa zake mbaya, ni kujimaliza mwenyewe.

Tumia muda kufahamu maisha ya nyuma ya mtarajiwa wako, fahamu namna mahusiano yake ya zamani yalikuwa, isije kuwa bado yanaendelea.

Kwani kupuuzia vitu vya msingi kama hivi unaweza kujikuta unalipa gharama kubwa ya maisha yako.

Tafuta kama kuna vitu mnafanana ambavyo wewe unapenda kufanya kwani migogoro mingi huanza pale kila mmoja anapofanya kile anakipenda na mwenzake hapendi.

Na ndoa hujengwa na kushikwa na vitu vidogo sana katika maisha ya hao wawili.

Je, vile wewe vinakuchekesha na mwenzako hucheka?

Je, mnapenda vitu vinavyofanana?

Ndiyo maana ndoa za Hollywood huwa hazidumu kwa sababu mkazo ni kwenye vitu na sura (material things) ambavyo havina sehemu katika kufanya ndoa kuwa imara.

Kabla hujakubaliana kuoana na huyo mtu unatakiwa kujiuliza, hivi ni kweli ninampenda kweli huyu mtu kuliko mtu yeyote duniani?

No comments: