"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 6, 2011

Hana Tatizo

Kinachoshangaza ni kwamba wanandoa wanapokutana na matatizo katika ndoa yao, wazo la kwanza kuja ni “kwa sababu nilioana na mtu ambaye si sahihi” inaweza kuwa kwa nyakati fulani au kwa mtu fulani ni sahihi na si sahihi kwa kila mmoja hasa katika karne hii mpya.

Tatizo unawaza kwamba ungekuwa umeoana na mwingine basi tatizo kama hilo lisingekuwepo, huku ni kuota mchana kweupe (illusions), Unajidanganya, halafu mbaya zaidi unamjua hata yule ambaye unaamini ungeoana naye usingepata matatizo haya unayopitia, ni upuuzi !

Unapoanza mahusiano na mtu yeyote mwanzoni huonekana ni kila kitu safi, sasa zoeana, mfahamu, ishi naye ndipo utajua kuwa kuishi na binadamu yeyote unahitaji upendo na kwamba huyo uliyemchagua ni wewe tu duniani unaweza kuvumilia vituko vyake au udhaifu wake tena kwa upendo na furaha na kumpokea kama alivyo.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

No comments: