"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, August 25, 2011

Kileleni!

Katika ndoa sex ni kitu kizuri kinachowafanya wanandoa kuwa mwili mmoja kwa maana ya kuwaleta karibu.

Jambo kubwa ambalo huleta raha ya kiwango cha juu kwa wanandoa wakati wa tendo la ndoa ni suala la kufika kileleni (orgasm)

Kila mwanandoa anaweza kufika kileleni Ingawa si kila mmoja, kufika kileleni kwa wengine si issue rahisi hasa kwa wanawake Ingawa kwa wanaume ni kitu rahisi hata kitendo cha mwanaume kuwa na penetration na kuingia kwa mke wake basi anaweza kujikuta anafika kileleni, Ingawa hilo haliwezi kumfanya mwanamke kufika kileleni.

Kufika kileleni ni nini?

Ni kitendo cha kufikishwa juu kabisa katika raha ya sex, msukumo wa kiwango cha juu wa raha ya tendo la ndoa ambalo huishia kumwacha muhusika ajisikie yupo relaxed na mwepesi. Kwa mwanamke kufika kileleni huwa kwa sekunde kadhaa ambazo huendana na kujisikia relaxed na msukumo wa kutamani kama kunyanyuka ili kupokea kitu au kutoa hata hivyo kama mwanamke ataendelea kusisimuliwa huweza kujikuta anafika kileleni tena Ingawa hii ni kwa wanawake wa umri fulani.

Je kuna aina ngapi za kufika kileleni kwa mwanamke?

Kimsingi kuna aina mbili za mwanamke kufika kileleni na hizi aina zinajikita kutokana na aina ya msisimko anaoupata (stimulation).

Kwanza ni kifika kileleni kwa njia ya kusisimuliwa kisimi chake (clitoral) kwa mwanaume kukisisimua kwa kuchezea kwa njia Tofauti anazozijua au wanazoelekezana wakati wa tendo la ndoa.

Pili ni kufika kileleni kwa njia ya uke (vaginal) na hii mara nyingi hutokea kutokana na mwanaume kuingia na kutoka kwa mawimbi huku akigusa eneo la G-Spot

Uzuri ni kila aina ya kufika kileleni ina ladha yake na wanawake wenye uzoefu wa hizi aina wanafahamu Tofauti yake.

Ni wanawake wachache sana hufika kileleni kwa kitendo cha Mr. Happy kuwa ndani ya uke hata hivyo ni rahisi mwanamke kufika kileleni kwa kuchezewa kisimi/kinembe chake kwa namna zote (touching/rubbing or kissing)

Je, ni milalo ipi husaidia mwanamke kufika haraka kileleni?

Kwanza ni ule wa mwanamke kuwa juu ya mwanaume na pile ule wa mwanamke kulala kwa tumbo lake na mwanaume kumuingia kwa nyuma.

Je ni mambo gani yanaweza kuathiri mwanamke kufika kileleni?

KWANZA

Mara ngapi mwanamke anapata sex, ili mwanamke kufika kileleni anahitaji kuwa na sex ya mara kwa mara (use it or loss it). Mwanamke anapokaa kwa muda mrefu bila sex ndivyo anakuwa mgumu kusisimka na mgumu kufika kileleni period.

PILI

Lazima mwanamke awe relaxed na hana stress au tension. Ili mwanamke apate raha ya mapenzi ni lazima awe comfortable na mazingira yaliyopo na pia mahusiano au ndoa yake bila trust na mwenzi wake mwili unajifunga na ngumu kufungua.

TATU:

Hii inamuhusu mwanaume ambaye anahusika na huyu mwanamke anayetakiwa afike kileleni Kwani anatakiwa kuwa caring na anayefahamu kumsisimua mwanamke asisimke kiasi cha kutosha na kumsaidia kufika kileleni kwa kusoma upepo unavyovuma.

Pia ni vizuri kwa mwanamke mwenyewe kujitambua na kufahamu mwili wake vizuri na zaidi kushirikiana na mume wake kuwa wazi kumweleza kile anaona kinampa raha na kitapelekea kufika kileleni.

Je, unahitaji sex inayosisimua katika ndoa soma hapa

No comments: