"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 6, 2011

Maembe

Naitwa James na mke wangu anaitwa Jane, nipo nyumbani nafanya kazi zangu na mke wangu Jane ameenda kwa Daktari ili kujua inakuwaje mbona amejikuta asubuhi mambo si ndivyo kama kuchoka si kuchoka, anajisikia kichefuchefu na kuna dalili lile zoezi letu la kupata first born limewezekana.

Jane amerudi na Daktari amemwambia mke wangu ana mimba ya wiki mbili na ndani ya miezi tisa tutakuwa na mtoto.

Nipo excited ila nawaza sana namna ya kuwa baba na kuitwa baba, mikikimikiki ya nepi usiku na mchana.

Ni wiki sasa naona mke wangu iwe mchana iwe usiku iwe lunch, breakfast au supper yeye anataka ale embe na kibaya zaidi lisiwe limeiva sana wala lisiwe halijaiva sana.

Anafakamia maembe kiasi cha kunifanya nihisi anaweza kuzaa maembe badala ya mtoto.

Kinachonishangaza hata moon yake inabadilika kila wakati, dakika moja ni chakalamu na dakika inayofuata ni balaa, mkali kama nyuki na ngumu kuishi naye, alikuwa anapenda juice ya machungwa, nanasi sasa hataki hata kusikia harufu yake, cha ajabu hataki hata juice ya maembe wakati anapenda kula embe (lisilo bichi sana na ambalo halijaiva sana).

Akiniona nafakamia juice basi ananiambia kwamba kwa nini sijali hisia zake.

Kibaya zaidi sasa hata majirani hawapendi inafikia muda anataka tuhame muda huohuo na kila ninapojitahidi kumwambia haitawezekana anaiita mimi ni selfish na kwamba kila ninachojali ni mimi mwenyewe na si yeye.

Mara ananiambia anahitaji ale mishikaki na mimi naondoka kiguu na njia hadi km 4 kufuata mishikaki ili mzazi mtarajiwa ale, ile nikifika nyumbani tu na kufungua ili nimpe ile mishikaki anabadilika ghafla eti nimetumia muda mrefu mno na sasa hahitaji.

Sasa ameanza mtindo anaamka saa tisa au nane au kumi usiku na kuniomba tuongee, namuuliza na huu usiku wa manane tuongee kitu gani, majibu ananipa analalamika kwamba sijali tena kuongea na yeye na kwamba nilichokuwa napenda ni kumtia mimba.

Finally, mtoto wetu akazaliwa na kila kitu kikaanza kurudi katika hali ya kawaida

Hakuna maembe tena!

No comments: