"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, August 16, 2011

Moto Umezima


SWALI
Mimi na mume wangu tumekuwa kwenye ndoa sasa ni mwaka wa 11, maisha yetu ni mazuri sana kila eneo la ndoa yetu isipokuwa suala la sex. Najiona kukumbuka sana namna moto wa mapenzi (passion) ulikuwa huko nyuma na sasa kila kitu kinaenda ovyo Linapokuja suala la sex.
Je tufanyeje ili mambo yarudi kama zamani?
Ni mimi Edna
JIBU:
Swali lako ni zuri na si mara ya kwanza kuulizwa hapa.
Pia nikupongeze kwa kufikisha miaka 11 pamoja Kwani maisha ya mahusiano siku za leo ni Tofauti sana.
Jambo la msingi ni kufahamu kwamba umekuwa na ndoa nzuri kwa miaka 11 kwa Sababu kila siku mmekuwa mnajitahidi kufanyia kazi ndoa yenu na pia maisha ya sex yameanza kuelekea kwenye velanda ya ICU kwa Sababu mmejisahau na kuacha kufanya vile mlikuwa mnafanya huko nyuma.
Inawezekana mnafanya kila kitu kwa kuzoeana na mazoea kuanzia kabla ya kuingia chumbani hata wakati mkiwa chumbani.
Je, unawezaje kurudisha moto wa mapenzi wewe na mumeo?
Jambo la msingi ni namna kila mmoja anajitoa (committed) kuwa wa motomoto kimapenzi na suala zima la maisha ya mapenzi kwa pamoja.
Baada ya kujitoa suala linalofuata ni kupanga, panga na fikiria vitu ambavyo mnaweza kufanya pamoja, vitu vipya, kuwa wabunifu wa nini mfanye pamoja na kile kitendo tu cha kufanyia kazi yale mnataka kufanya pamoja tayari kitaanza kuwapa furaha na msisimko wa pamoja kimapenzi.
Sasa Hakuna moto wa mapenzi kwa kuwa ule moto mmeuzima au umeenda kulala usingizi mzito, ni muda wa kuwasha na kuamka, jaribu vitu vipya, jaribu mlalo mpya wakati wa sex, jaribu kwenda kufurahia miili yenu sehemu Tofauti na hapo chumbani kwenu, jaribu muda Tofauti wa sex, jaribu kugusa sehemu Tofauti katika mwili wakati wa kufanya maandalizi na fanya yote kwa upendo na kwa kupokea na kutoa.
Jaribu kusafiri au kutembelea sehemu mpya pamoja kama mke na mume (mbuga za wanyama, beach au hotel)
Pika pamoja, cheza pamoja, piga story pamoja, mlishe chakula mpaka ashibe, kumbatianeni, shikaneni, mwambie maneno matamu ambayo hujawahi kuyasema, mtie moyo, msifie, mpende nk
Mapenzi motomoto hayaji yenyewe lazima muwe wabunifu na wavumbuzi
Uwe mbunifu, mbunifu, mbunifu, mbunifu, mbunifu…………

2 comments:

Anonymous said...

Ahsante sana mpendwa kwa elimu unayotupa ujawa mchoyo kushirika na sisi katika kuula huo mkate mtamu.

Lazarus Mbilinyi said...

Asante sana na Ubarikiwe