"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 6, 2011

Nilaleje?

Linapokuja suala la kupata mtoto (conception) wengi huongea mengi hasa ni mlalo upi (love making position) unafaa zaidi ya mwingine.

Je, mlalo mzuri kwa mwanamke ni upi?

Ingawa kuna tafiti chache sana kwenye hili suala jambo la msingi ni kufahamu nini huwa kinafanyika kule ndani baada ya mwanaume kuachia sperms mle ndani.

Hahitaji kuwa mtaalamu wa kuzungusha mwili ili kuwa na matokeo bora ya kutengeneza mtoto bali ni ubora wa zile mbegu na mazingira ya kule zinapandwa.

Kimantiki mlalo wa baba na mama (missionary position) unatosha kabisa kutengeneza mtoto Kwani huwezesha mpenyo wa uhakika (deep penetration) kwa mbegu kufika mwanzo au katika eneo la mapokezi (anterior) tayari kusafirishwa kwenda ndani na pia mwanaume kuingia kwa nyuma (rear entry/doggy) hupelekea mbegu kwenda moja kwa moja nyuma ya cervix (posterior) na kuhakikisha mtoto anatengenezwa.

Kumbuka ubora wa mbegu ndicho kitu cha msingi Kwani mbegu kawaida husafiri umbali wa wastani wa km 45 kwa saa na chini ya hapo disaster.

Jibu rahisi Hakuna umuhimu sana kwenye milalo kama suala ni kutengeneza mtoto mlalo wowote mtoto hupatikana kama mbegu ni bora.

Je, ni vizuri kulala baada ya tendo?

Wataalamu wanasema ni vizuri kulala (horizontal) baada ya tendo pale tu kama wakati wa kutengeneza mtoto mama alikuwa juu ya mume wake au mama alikuwa amesimama, hii ni kusaidia kuzipa mbegu gravity ili ziogelee vizuri kwenda kiwandani hata hivyo kama mbegu zilizotoka ni bora (healthy) bado zita swim na kupanda mlima wowote na kufika kiwandani tayari kwa kujichanganya na yai kufanya mtoto.

Je, kufika kileleni ni muhimu katika kutengeneza mtoto?
Ingawa mbegu huweza kuvuja na kwenda zake hata kabla ya kuruhusiwa wakati mwanaume ameshasisimuka, bado suala la mwanaume kufika kileleni ni muhimu ili kuzipa mbegu mwendao kasi unaotakiwa.

Tafiti mpya pia zinapendekeza mwanamke afike kileleni wakati wa kutengeneza mtoto Kwani ile contraction wakati wa kufika kileleni husaidia kubeba mbegu kwenda kiwandani na hii huwa nzuri zaidi kama baba na mama watafika kileleni pamoja.

Nahitaji mtoto wa kike au kiume je kuna aina ya milalo inafaa kwa kila jinsia ya mtoto.

Hata kama kuna imani nyingi na hadithi nyingi kuhusu milalo na jinsia za watoto ukweli ni kwamba milalo haina uhusiano na jinsi ya mtoto.

Kinachofanikisha jinsia ya mtoto ni timing ya siku mwanamke anapokuwa fertile na mara ngapi sex wanafanya katika hicho kipindi ambapo mwanamke anakuwa fertile.

Je, ni mara ngapi nifanye sex kupata mtoto?
kama nilivyoeleza hapo juu timing ndo wimbo wa mchezo wa kutengeneza mtoto. Kuongeza nafasi ya kupata mtoto ni vizuri baba na mama kufanya mapenzi siku moja au mbili kabla ya mama kuwa fertile au siku ileile ambayo mama anakuwa fertile.

Pia ni vizuri mama kufanya mazoezi ya recording ya mzunguko wake ili kujua lini anakuwa fertile ndipo wafanye timing.

Au mnaweza kwenda madaktari au maduka ya masuala ya mambo ya uzazi na mkanunua Ovulation Prediction kit na mkawa nacho nyumbani.

NB:

Ewe mwanamke usicheze na sperms kama huna mpango wa kushikwa mimba, kitendo cha kushikwa sperms na mikono yako then ukagusa ndani ya uke wako kwa vidole ambavyo viligusa sperms unaweza kushika mimba, au hata kama umevaa kufuli kitendo cha sperms kucheza ndani ya 18 hata kama una kufuli zina u-genius zinaweza kusababisha mimba.

Kaa mbali na sperms kama huna mpango wa kupata mimba!

Maelezo zaidi soma hapa

2 comments:

Anonymous said...

KWENYE N.B.
Je, kumchezea au kumsugua mke kwa jujuu na mr. happy kama ni siku yake ya mimba yaye majimaji yanayowatoka wanaume yanaweza kupenya ndani ya uke na kusababisha mimba? P.M.

Lazarus Mbilinyi said...

PM,

Ndiyo anaweza kupata mimba. Kama wewe na mpenzi wako hamna mpango wa mimba mchezo huo unaweza kusababisha mimba. Usimchezee Mr. Happy eneo hilo kwani anaweza kufanya kile hujamtuma as long as huwa anakuwa happy na hiyo shughuli.

Upendo daima