"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, August 22, 2011

Ukweli wao!

Mshauri maarufu wa masuala ya ndoa M. Gary Neuman alifanya Utafiti kwa kuwauliza wanaume 200 ambao kati yao walishachepuka nje ya ndoa zao na wengine walikuwa hawajawahi kuchepuka (cheat) na lengo lake lilikuwa ni kufahamu kwa nini hawa wanaume huchepuka nje ya ndoa zao.

Mara nyingi watu wanaotaka kujua kwa nini wanaume wana cheat huwauliza wanawake hata hivyo Gary Neuman aliamua kuwauliza wanaume wenyewe ili wajieleze kwa nini wanachepuka (cheat) na pia alitaka kuwauliza je nini kingefanyika basi wasinge thubutu kuchepuka.

++++++++++++++++++

Asilimia 48 ya hao wanaume walikiri kwamba kutoridhishwa kihisia (emotions) ilikuwa Sababu ya msingi kuchepuka.

Wengi huamiini kwamba mwanaume ili kutoka nje ya ndoa yake hufuata sex tu, wanaamini kinachomfanya mwanaume kuwa na furaha ni sex.

Ukweli ni kwamba hata wanaume ni viumbe wa hisia (feelings/emotions), wanapenda wake zao wawashukuru, wawape sifa wanazostahili kutokana na juhudi zao za kifamilia na masuala ya ndani ya ndoa (appreciation).

Tatizo kubwa ni kwamba wanaume hushindwa namna ya kuelezea hisia zao kwa wake zao na matokeo yake mahitaji yao ya kihisia hupitwa bila kupewa kila wanahitaji.

Nini mwanamke anatakiwa kufanya kwa mume wake:

Ni kumpa appreciation idara zote na hiyo ni silaha

++++++++++++++++++++++

Asilimia 66 walikiri kwamba hujisikia hatia (guilt) wanapochepuka (cheat)

Si kwamba wanaume wanaochepuka ni wanaume ovyo tu bali kuna asilimia 68 ya wanaume hawakuwahi kuota kama kuna siku watachepuka na pia husikitika kwamba afadhari wasingethubutu kufanya.

Hii ni kudhihirisha kwamba kujisikia hatia wakati wa kuchepuka hakuwezi kuzuia asichepuke.

Tabia kubwa ya mwanaume ni kiumbe ya kitu kimoja kwa wakati (compartmentalization, single task) kwa maana kwamba hata kama anajisikia hatia bado huwa na uwezo wa kufurahia sex na anajua atashughulikia hiyo hatia baadae Kwani kujisikia hatia na kufurahia sex na yule mwanamke ni vitu viwili kwake na Tofauti.

Hii ina maana gani kwa mwanamke yeyote?

Hii ina maana kwamba hata kama mume wako anaapa kwa kila anachokijua kwamba hatachepuka, usidhani kwamba hawezi kutokea badala yake Mnatakiwa kuchukua hatua muhimu kutengeneza ndoa mnayoihitaji.

++++++++++++++++++++++++

Asilimia 77 ya wanaume wanaochepuka wana rafiki wa karibu ambaye alichepuka.

Mwanaume kuwa karibu na rafiki ambaye si mwaminifu huwezesha aone kuchepuka ni kitu cha kawaida na sahihi.

Kichwani mwake kuna kuwa na ujumbe kwamba “huyu rafiki yangu ni mtu mzuri na bado anaweza kuchepuka na kumdanganya mke wake, hivyo wanaume wazuri wote tunaweza kuchepuka.

Ingawa si rahisi kumkataza mwanaume au mume wako asitumie muda wake na rafiki zake ambao macho yao ni kwenye malinda ya wanawake unachoweza ni kumsaidia kutumia muda wake na hao marafiki katika mazingira ambayo si hatarishi kama vile michezo na si night clubs au bar.

Nini mwanamke anaweza kufanya katika hili.

Ni kujenga mahusiano ya jamii ambayo mume huwa rafiki na mtu wa kufurahishana kijamii kama vile kuangalia match za mpira pamoja au kufanya pamoja kile mume wako anakipenda.

Jenga mazingira yanayofanya ndoa kuwa mpya kila leo.

+++++++++++++++++++++++++++

Asilimia 40 ya wanaume wanaochepuka walikutana na huyo mwanamke kazini.

Mara nyingi mwanamke anayechepuka naye ni yule ambaye anampa sifa, ana kuwa karibu naye kwa kile anahitaji na ana msifia kwa juhudi zake katika mambo anayofanya.

Ndiyo maana ni muhimu sana mwanaume kujiona ana thamani nyumbani.

Pia wewe mwanamke unatakiwa kuwa makini kwa yule mwanamke wa kazini kwake ambaye anamtajataja mara nyingi kuliko wanaume wenzake huko kazini.

Nini cha kufanya kwa mwanamke ukigundua kuna mwanamke anamtajataja?

Jambo la msingi ni kuweka mipaka tena kwa upendo na uwe makini kufahamu kama anachelewa kazini kwa Sababu yupo na huyo mwanamke, au anasafiri na huyo mwanamke au anaenda lunch au dinner na huyo mwanamke na si wanaume wenzake.

Au muulize yeye atajisikiaje kama na wewe mwanamke utafanya hao na mwanaume mwingine.

+++++++++++++++++++++++++++++

Asilimia 12 ya hao wanaume walikiri kwamba ni kweli wanawake waliochepuka nao walikuwa ni warembo kuliko wake zao.

Hii ni asilimia ndoa sana na ina maana kwamba mwanaume hatoki kwa Sababu anaamini akiwa na mrembo basi atapata sex nzuri, ukweli ni kwamba anachepuka kwa Sababu ana pengo la kihisia ndani yake.

Anajiona yupo connected na mwanamke mwingine kuliko wewe mke wake na sex hupata msaada (lift) kupitia hiyo connection.

Kama una wasiwasi na mume wake kuchepuka basi focus katika kuimarisha mahusiano na kupendana na kuwa connected kuliko kuonekana una sura na urembo wa uhakika au kujua ulale vipi (chumbani)

Sijasema usipendeze au mume wako hahitaji sex bali unatakiwa kuweka mkazo katika upendo na ukaribu wa mapenzi kwanza na kumridhisha hisia zake kwanza ndipo sex.

+++++++++++++++++++++++++++

Asilimia 6 tu ya wanaume wanaochepuka walichepuka siku ile ya kwanza kukutana na huyo mwanamke.

Hii ina maana kwamba wanaume wanaochepuka huonesha dalili mapema kabla ya tukio lenyewe.

Angalia hizi alama

Kwanza hutumia muda mwingi nje ya nyumbani, anaacha kukuuliza kutaka sex, anaanza kuwa mkali bila Sababu ya msingi, anaanza kutojibu simu zako au sms.

Badala ya kumkoromea, unatakiwa kuchukua hatua za kuimarisha mahusiano yako na yeye kwa upendo mpya zaidi.

Pia wapo wanaume ambao hata ufanyeje wao kuchepuka ipo tu.

Hata hivyo wapo wanaume ambao ni makini na smart sana kiasi cha kuwa kazi ngumu sana kuwakamata au kujua kwamba wanachepuka.

Soma hapa


No comments: