"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 6, 2011

Uwe Mkweli

James (38) ni tajiri (millionaire) alisafiri kwa ajili ya biashara nchi za mbali.

Jane (32) mke wake ni mjamzito, wakati James yupo safarini, Jane alijifungua mtoto ambaye kwa bahati mbaya akazaliwa akiwa na matatizo ya ubongo (mental retarded).

Jane aliamini itakuwa shida, aibu na sifa mbaya kwa familia ya kitajiri kuwa na mtoto zezeta au asiye na ubongo unaofanya mambo kiusahihi hivyo kwa kuwa wana fedha za uhakika akatafuta nyumba sehemu ambapo aliajiri dada ya kumtunza mtoto na Daktari wa kumkagua mtoto na kumpa matibabu na kila anachohitaji bila mume wake kufahamu.

James aliporudi safarini akaambiwa na mkewe kwamba bahati mbaya mimba iliharibika kwa mtoto kuzaliwa amekufa (still born) hata hivyo baada ya muda James alishtukia mawasiliana ya Daktari na mke wake na akahisi hapa kuna kitu si cha kawaida kama si mkewe anachepuka na kutembea na Daktari.

Baada ya kumbana mkewe, mke alikiri kwamba ni kweli alizaa mtoto mwenye mtindio wa ubongo na hivyo alimficha huko sehemu ambapo daktari humhudumia.

Nini kilitokea?

James alimwachia nyumba na kuhama kwenda anakojua yeye na ndoa ikawa hadithi.

Who is stupid here?

No comments: