"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, August 15, 2011

Yana siku zake.....

Wapo wanawake huweza kufika kileleni kwa kusisimuliwa matiti yao tu.

Asilimia moja ya wanawake huweza kufika kileleni kwa kuchezewa nyonyo na waume zao au wapenzi wao.

Hili limewekwa wazi na mwanaharakati wa masuala ya mahusiano aitwaye Marshall Miller na mwenzake Dorian Solot.

Inawezekana mpenzi wako au mke wako ni mmoja wao kama wewe ni mwanaume.

Kuna baadhi ya wanaume wana ugonjwa wa kuyaangalia matiti ya wanawake kiasi ambacho huweza hata kusisimka.

Wakiwa njiani au barabarani au mahali popote wanawake wapo basi kile kitendo cha kumuona mwanamke mwenye matiti makubwa humfanya ajisahau na kubaki kakodoa mimacho hadi kuhatarisha maisha yake kwa akili yake kupotelea kwenye kifua cha mwanamke.

Pia jamii kama ya wamarekani ina ugonjwa wa kupanda matiti kuliko jamii zingine duniani tena matiti makubwa kiasi ambacho hata biashara ya kubadilisha matiti (breast implant) ina vuma na inatengeneza mamilioni ya dola.

Titi la kushoto ni kubwa kuliko titi lile la upande wa kulia.

Hii ni kutokana na chapisho ambalo liliyaangalia matiti 600 ya wanawake ambao walikuwa wanafanyiwa breast Implant au plastic surgery.

Hivyo kama ni mwanamke haina haja kushangaa au kujiuliza ukihisi titi moja ni kubwa au dogo kuliko lingine ila si kwa utofauti mkubwa ambao huleta shaka.

Wapo wanaume ambao matiti yao hutoa maziwa pia.

Ingawa ni mara chache sana hata hivyo wapo wanaume wakati Fulani katika maisha yao hujikuta chuchu zao zinatoa kiasi kidogo sana cha maziwa.

Hii ni kwa Sababu hata wanaume wana homoni (mammary glands) kama walivyo wanawake. Na baadhi ya dawa za kutibiwa (cancer) zina kiasi fulani cha estrogen ambayo husababisha maziwa kutoka.

Wanawake ambao hubadilisha matiti (breast implant) ndiyo hujinyonga zaidi katika wanawake ambao hujinyonga duniani.

Utafiti ulifanywa na chuo kikuu cha Laval Quebec Canada uligundua kuwa kati ya wanawake waliojinyonga asilimian 75 walikuwa ni wale ambao walibadilisha matiti yao.

Sababu ya msingi ya kufanya idadi wa wanaojinyonga kuwa kubwa ni kutokana na kutojiamini, msongo wa mawazo au kutojiamini na maumbo ya miili yako. Wapo wanawake ambao huamiini matiti makubwa huwafanya wajiamini au kuwa na matiti makubwa badala ya madogo huwasaidia kutatua matatizo mengine.

Ukweli usiopingika ni kwamba wanawake ambao hubadilisha matiti yao kwa kufanya implants huwa haiwasaidii sana Kwani Tatizo si matiti bali mitazamo yako ya kutojiamini.

Kulala mlalo wa kuyalalia matiti (kifudifudi) hakuwezi kufanya yapungue umbo (kuwa madogo)

Ingawa huweza kubadilisha mwonekano wake baada ya muda.

Njia nzuri ya kulala ambayo humfanya matiti yako yawe na umbo lililoimarika ni wewe kulala kwa ubavu na weka mto kuyapa support.

Zaidi ya wanawake milioni 2 duniani wana matiti ambayo ni fake (siyo ya ukweli).

Hata kama suala la kubadilisha umbo na kuweka vitu vya ziada (plastic surgery/implants) bado hivi vitendo vina athari za kiafya kwa mwanamke.

Inawezekana huyo mpenzi wako kike ana matiti fake!

Matiti nayo yana mzunguko wake wa siku na siku zake.

Baada ya mwanamke kupata siku zake matiti huwa laini (soft, smooth) na chuchu huwa na msisimko zaidi kwa kuwa estrogen huwa katika kiwango cha juu.

Na mwanamke akiwa kwenye siku zake matiti huwa tender na wakati mwingine huuma na kuongezeka size kwa kuwa homoni ya progesterone huwa katika kiwango cha juu.

Chuchu za wanawake hutofautiana katika size na shape na pia namna zinasimama (directions)

Matiti huongezeka unene mwanamke anapoongezeka umri.

Mwanamke anapokuwa kijana titi hujawa na kiwango kikubwa cha fat, maziwa na collagen, na mwanamke anapozeeka vyote hubadilishwa na fat.

Bahati mbaya ni kwamba kuongezeka huko kwa umbo ndiko husababisha matiti kulala na si kusimama Kwani sasa inakuwa imebaki fat tu na si maziwa.

Kwa Maelezo zaidi kuhusu matiti soma hapa

No comments: