"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, September 19, 2011

Ujuzi katika Ndoa

Kama wewe ni kizazi cha Adam na Hawa basi suala la ndoa linakuhusu sana na ndoa ni kitu beautiful, Kwani huleta mahusiano ya kutosheleza yanayowaunganisha watu wawili mke na mume.

Inapendeza kwamba Mungu amemuumba mtu maalumu kwa ajili yako.

10. UJUZI WA KUTATUA MATATIZO

Kama wanandoa hawana ujuzi wa kutatua matatizo inaweza kusababisha ndoa kuwa ngumu sana hasa miaka 2 ya kwanza katika ndoa.

Kuwa na ujuzi namna ya kutatua matatizo katika ndoa ni kufahamu namna ya kuzozana kwa kuelezana ukweli kwa upendo, kufahamu ni wakati gani wa kukaa kimya au kuzungumza.

9. UJUZI WA KUMWEKA MWENZI WAKO NAMBA MOJA

Kumbuka katika ndoa kuna wewe, mwenzi wako na Mungu.

Jambo la msingi ni uhusiano wako na Mungu wako (siyo kazi ya Mungu, au kwenda kanisani bali uhusiano wako na Mungu, then mwenzi wako (mume au mke) ndipo wanakuja watoto na mwisho kazi.

Kama mke wako anafuata baada ya watoto, mama yako au baba yako au ndugu zako au rafiki zako au TV au Manchester United au chochote kile basi ndoa yako haina jipya na ipo siku mwenzi wako ataona hana maana katika ndoa yenu.

8. UJUZI WA KIMAISHA

Ni muhimu sana kila mwanandoa kufanya vitu ambacho vitakuwa msingi wa maisha ya baadae (future) pia kila mwanandoa analo jukumu la kujiuliza ni namna gani anaweza kuwa mwanandoa mwema miaka 10 au 20 ijayo.

Kila mwanandoa analojukumu la kujiuliza nifanye vitu gani ili niwe mwenye mvuto hata miaka 10 ijayo.

Je, niende shule?

Je, nianzishe biashara?

Je, nifanyeje kumpa support mwenzi wangu katika kazi zake au taaluma yake?

7. UJUZI WA KUSAMEHEANA

Unapokuwa kwenye uchumba, mchumba akifanya kitu cha ajabu unaweza ukaachana naye na kumsahau kabisa, hata hivyo kwenye ndoa unatakiwa kusamehe na kusahau sasa hivi.

Mwenzi wako anapofanya kitu na kujiona amekosea, atakuomba msamaha Kwani ni kweli yeye ni binadamu na ana mapungufu na hayupo sahihi mara zote.

Muda ule ambao unakuwa hutaki kusamehe mahusiano huacha kukua na hudumaa.

Kama huna uwezo/moyo wa kusamehe basi kwenye ndoa usiingie; jibakie single milele.

6. UJUZI WA KUWA MBUNIFU

Kwenye ndoa tunaishi pamoja na kuonana kila siku, tunalala pamoja, kula pamoja, oga pamoja nk.

Bila kuwa mbunifu kuwa na “fun stuff” ndoa huzoeleka na kuchosha.

Tafuta vitu ambavyo mkifanya pamoja vitawafanya kuwa na kitu kipya.

Wapo wanandoa ambao akioa au kuolewa basi Hakuna jipya, Hakuna ubunifu kila mwaka vitu ni vilevile, badilika fanya vitu Tofauti kama hujawahi kwenda sehemu fulani nenda na mkeo au mumeo, have fun!

5. UJUZI WA MTAZAMO CHANYA

Jifunze kuwa na mitazamo chanya kwenye tabia za mwenzi wako. Ni kweli kuna vitu unavipenda kuhusu yeye na kuna vitu ambavyo unavichukia kuhusu yeye, hata hivyo ukweli ni kwamba vitu vizuri unavyovipenda kuhusu yeye ndivyo vimekufanya uoane naye na kwamba vina nguvu kuliko vile ambavyo huvipendi kuhusu yeye.

Weka mtazamo (focus) kwenye vile vitu ambavyo vinawafanya ninyi wawili kuwa kitu kimoja.

Ukimnyoshea kidole kimoja mwenzi wako, basi unatakiwa kujinyoshea vidole 5 wewe mwenyewe.

4. UJUZI WA KUJIAMINI

Lazima uamini kwamba ndoa yenu itadumu na Hakuna kitu kinaitwa talaka na talaka haitakubalika.

Ni muhimu sana ujiamini kwamba mwenzi wako ( mume wako au mke wako) anakipenda sana kama wewe unavyompenda yeye hata kama haoneshi kwamba anakipenda.

Fahamu hivyo na amini hivyo.

Kwa njia hii huwezi kuyumbishwa na upepo wa mashaka na hofu wakati kunajitokeza kutoelewana.

Kwa njia hii itakuwa rahisi kuirudisha ndoa kwenye mstari.

3. UJUZI WA KUJIFUNZA

Wakati mwingine katika ndoa huwa tunajidanganya sana kwamba tunawafahamu vizuri wenzi wetu hata hivyo baada ya muda tunaanza kushangaa na kujiona tumeoana na mtu ambaye amebadilika sana na Tofauti na wakati ule mnaoana.

Hata hivyo kujisikia mume wako au mke wako amebadilia na kuwa binadamua mwingine si Sababu ya kuachana au kupeana talaka.

Kama huna ujuzi wa kumsoma au kujifunza kuhusu mwenzi wako basi hukutakiwa kuoa au kuolewa au hukustahili kuoa au kuolewa naye.

2. UJUZI WA KUJUA NAMNA WENGINE WANAWAONA/WANAJIFUNZA

Kama umeoa au kuolewa na unajifanya hujaoa au kuolewa ni kweli dunia na viumbe wake wanakuona ni kweli hujaoa au kuolewa pamoja na umri wako kwenda.

Unatakiwa kuonekana wewe na mwenzi wako ni watu wenye furaha na amani na kweli iwe furaha na amani ya kweli siyo fake.

Mnatakiwa kuwa na smile la kweli na liwe na kweli si fake.

Lazima uwe makini na kufahamu wengine wanawaonaje kama wanandoa na hiyo itakusaidia kujiweka sawa kuhakikisha kunakuwa na kicheko katika ndoa yenu.

1. UJUZI WA NAMNA YA KUGOMBANA

Hakuna ndoa ambayo wanandoa hawajawahi kupishana au kupingana au kutoelewana au kutokukubaliana katika jambo fulani au tabia fulani.

Pia ni muhimu sana kufahamu kila mnagombana au Sababu ya kitu kinafanya kuwe na msuguano.

Unatakiwa kuwa na ujuzi wa kufahamu kwamba kugombana kokote kusiwe kwa masaa kadhaa, au siku kadhaa au miezi kadhaa.

Pia ni muhimu sana kuangalia namna unabishana au unaongea wakati wa kutokukubaliana na jambo lolote.

Pia focus katika kulishambulia Tatizo lenyewe na siyo mwenzi wako.

5 comments:

Anonymous said...

hello kaka. samahani nahitaji msaada na ushauri wako, mimi ni mwanamke nipo kwenye ndoa miezi sita sasa, ni mjamzito wa miezi minne, swali langu ni je mlalo gani unafaa zaidi wakati wa tendo la ndoa? je "kifo cha mende" kina madhara kwangu na kwa mtoto. Mimi sina tumbo kubwa mpaka sasa, tafadhali nielimishe kuhusu haya. Na pia mbona nikifanya style ya chuma mchicha uke wangu unaingiza upepo? Kazi njema ndugu yangu

Anonymous said...

Kadri siku zinavyoenda tumbo litaongezeka na utahitaji kuwa makini na milalo na mlalo mzuri ni kulala upande (uso kwa uso au uso kwa mgongo) na kuendelea kufaidia mapenzi na mumeo umpendaye. Pia yakupasa kuwa makini na miezi 3 ya mwisho kuhakikisha kila kitu kipo sawa ndipo mjirushe kimahaba.

Kuhusu kuingia upepo kwanza inatokana na umbile lako kwamba ukiwa kwenye hiyo style unakuwa exposed zaidi na upepo kuweza kupenya na huna namna zaidi kuwa makini na kujirusha kunakuruhusu hewa kupenya au tumia style ambayo una uhakika upepo haupenyi au mwambie mpenzi wako kwamba asishangae mlio wa wakati upepo uatoka na zaidi muendelee kufurahia mapenzi.

Anonymous said...

Hi fantastic blog! Does running a blog similar to this take a great deal of work? I have no knowledge of coding however I was hoping to start my own blog in the near future. Anyhow, should you have any ideas or tips for new blog owners please share. I know this is off topic but I just wanted to ask. Many thanks!

Anonymous said...

hey there mbilinyi.blogspot.com blogger found your website via Google but it was hard to find and I see you could have more visitors because there are not so many comments yet. I have discovered site which offer to dramatically increase traffic to your site http://xrumer-services.net they claim they managed to get close to 4000 visitors/day using their services you could also get lot more targeted traffic from search engines as you have now. I used their services and got significantly more visitors to my site. Hope this helps :) They offer most cost effective services to increase website traffic Take care. Roberto

Anonymous said...

It’s difficult to get educated people on this topic however you sound like you know what you’re talking about!
Thank you for this post. I definitely agree with what you are saying.
Keep us posted.

My website; go to this website (http://google.com)